Kwa hili la hujuma kwa gaziti la mwananchi ni umafya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili la hujuma kwa gaziti la mwananchi ni umafya.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kurunzi, Apr 19, 2012.

 1. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mwananchi lahujumiwa Dodoma
  GAZETI la Mwananchi linalochapwa na Kampuniya Mwananchi Communications Ltd (MCL), juzililigeuka bidhaa adimu mjini Dodoma baada ya
  watu wasiojulikana, kulihujumu na kununua nakala zote.

  Haijafahamika hasa sababu za mtu au watu hao kukusanya nakala zote za gazeti hilo na
  kuziondoa katika mzunguko, lakini taarifa zinadai lilikuwa na habari ambazo zilikuwa
  zikitishia masilahi yao.

  Katika ukurasa wa kwanza kulikuwapo na habari
  tatu kubwa; moja ikihusu kushamiri kwa vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliomalizika juzi
  usiku.

  Licha ya habari hiyo, kulikuwapo na habari iliyomhusu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, kuhusishwa na kashfa ya uuzaji wa kiwanja kimoja kilichopo Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam.

  Habari hizo mbili ndizo ambazo zinahisiwa zilisababisha watu hao kununua magazeti hayo,
  wakihisi ama zingevuruga harakati zao za uchaguzi au zingewafunua wabunge kuhusu
  kashfa hiyo ya kiwanja.

  Waandishi wa habari wa Mwananchi waliokuwapo katika viwanja vya Bunge walikuwa
  na wakati mgumu kujibu maswali ya wabunge waliotaka kufahamu sababu ya kutokuwapo kwa gazeti hilo mjini hapa.

  Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema, alihoji sababu ya mtu mmoja kuwanyima Watanzania
  wote walioko Dodoma fursa ya kupata habari kutokana na hofu anayoijua mwenyewe.
  “Mimi kila nikiuliza naambiwa kuna watu wamelinunua gazeti lote wamekwenda kulichoma, nikawauliza kwani limeandika nini kibaya dhidi yao? Lakini hawanijibu!”alisema
  Mrema.

  Habari zisizo rasmi zilidai kuwa magazeti hayo yalinunuliwa na mawakala wa kigogo mmoja
  ambaye anahusishwa na uuzaji au ununuzi wa kiwanja hicho kilichopo Barabara ya Nyerere.
  Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, ukusanyaji wa gazeti hilo ulianzia eneo la usambazaji katikati ya mji na kila muuza magazeti aliyekuwa akiuziwa alikuwa akidakwa na
  kutakiwa kuyauza.
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Alhaji Mkulo mwaka huu ataipata. Ila kwa jinsi alivyo mchawi utashangaa bosi wake anamteua kuwa naibu makamu wa Rais na Waziri wa fedha hata kama katiba haitazingatiwa
   
 3. s

  slufay JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Si hujuma bali mwananchi waulize Mwananchi wenyewe usiishi kwa matumaini ndugu na kuhisi tu
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Duh huyo mzee naona kapwaya maeneo ya kusimamia fedha zetu.
   
 5. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Wachapishe tena na tena hiyo habari
   
 6. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Sijakusoma hebu tulia uandike tena labda nitakuelewa.
   
 7. s

  slufay JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  si hujuma lakini kwa siku hiyo biashara ilikuwa nzuri sana, tusiishi kwa hisia tu; huenda mwananchi walitoa nakala chache
   
 8. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kumbe anajisafisha juu huku chini anajinyea
   
 9. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  dawa ndogo, ni mwananchi kuzirudia habari hizo upya
   
 10. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  hakuna hujuma hapo kibiashara... hujuma ni kwa walengwa tu, wananyimana habari

  Dawa ni mwananchi kutoa special edition ya gazeti hilo na kama inawezekana kuweka edition ya weekly hot topic na waitoe ijumaa au jumamamosi
   
 11. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,112
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  mkulo ni mwizi. Mkikumbuka wananchi wa kilosa walisema sio raia lakini ccmafisadi wamemngangania kwa vile wanaiba pmj
   
 12. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Daaah..! Hatari kweli kweli.
   
 13. m

  matawi JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hilo neno kingine liweke hapa jf tulidadavue
   
Loading...