Kwa hili Jumuiya ya wazazi CCm mnaendelea kukitia doa chama chenu.

kdom

JF-Expert Member
Jan 23, 2017
238
146
Ni ukweli kwamba jumuiya ya wazazi CCm imeuza baadhi ya shule zake hususani shule ya sekondari Hedaru iliyopo wilaya same mkoani kilimanjaro.

Kitu cha ajabu ni kwamba wafanyakazi zaidi ya 40 katika shule hiyo bado hawajapata kulipwa stahiki zao ikiwemo malimbikizo ya mishahara yao baada ya shule hiyo kuuzwa kwa muwekezaji MWeCAU takribani mwaka mmoja ulopita.

Maana waliahidi kulipa stahiki za wafanyakazi mwezi wa nane mwaka ulopita lakini hadi leo kimya tu,niombe ngazi za juu za chama ziweze kufuatilia hili.

Maana kuna wafanyakazi wamefanyakazi zaidi ya miaka 30 pale na baada ya shule kupungukiwa wanafunzi shule ilishindwa kulipa mishahara kwa wafanyakazi hivo kuishi kwa ukata sana.

Walijua kuwa watalipwa maramoja baada ya shule kuuzwa kama wakivyoahidiwa lakini hari imekuwa tofauti sana kwani hadi sasa hakuna jipya.

Naomba ngazi za juu za chama mjaribu kulitazama hili kwa namna ya pekee maana wazee wanapata shida sana na wanachuki sana na chama.

Huenda mkaendelea kupoteza wapiga kura wenu na kupoteza imani kwa wananchi maana wazee hao wana watoto wao wajukuu na ndugu ambao kwa namna moja au nyingine wanawategemea katika kuendesha maisha yao mf. Wazee hao wanasomesha n. K.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom