Kwa hili Jenerali Uimwengu umewaacha mashabiki wako njia panda

Ulimwengu ni mwandishi mzuri mkuu, nadhani atakuwa ameandika kama MOCKERY au Joke fulani kumconscietize mkwere afumbue macho hata kama hataki kuyafumbua!
 
Kama Watanzania, tuuone ufisadi mdogo-mdogo wa watu kula posho mara mbili, ndipo turejee kwenye ufisadi mkubwa pia. tujitazame tulikotoka na tulipo, tujitathmini tuendako itakuwaje. Ukiichambua kwa kina barua hiyo. Hutopata watu wasafi katika ofisi za serikali:tape:
 
Ulimwengu kanifanya nikumbuke wale sex tourists wa kike, wanaotoka ulopu kwenda Caribbean kuwatafuta vijana wanaowaambia maneno kwa kuigiza. I love you! i am dying ....., You are my ....., nk.
Akina mama hawa pamoja na kujua lengo la vijana hawa kwamba ni kupata pesa kwa service wanayotoa, bado wanafurahia maana wanasema huko kwao hawapati maneno kama hayo hata kama ni ya kuigiza.

Sasa eti Ulimwengu wetu anarudia sifa za ushindi mkubwa na mengine yoote hayo kwa kuamini bado yana maana kwa mtawala. Anafahamu huyo bosi wa nchi anahitaji kuliwazwa kwa lugha hiyo hata kama siyo kweli. Sijui ni kwa nini hakutaka ku-edit na kuifanya barua iendane na matukio ya uchaguzi wa mwaka huu.

Bado siwezi kumuunga mkono kwa barua ya aina hii. Hata kama aseme sababu gani. Lip service.
 
Mie nadhani mantiki ya barua hii bado inasimama. Badala ya kusoma mstali mmoja au sehemu ya aya na kutafuta mapungufu, ni vema msomaji akajikita kutafakali mantiki ya barua hii ndefu.Kwa mtazamo wangu barua hii ni timamu kwa rais yeyote awaye. Naona kila neno linabeba ujumbe mzito katika picha halisi, hasa unaposoma kwa tafakari ukiwa na "open mind". Ni matazamo tu ....
 
Mimi sino ubaya wa barua hii, tena natamani ningeona hiyo sehemu inayofuata. Ukiisoma vizuri na taratibu ukaitafakari sana utaona maana kubwa aliyo nayo Ulimwengu. Haswa ukijaribu kuacha u-Politiki ukatafuta the positive meaning of the letter you will enjoy mtiririko wake. Ila utajiuliza kwa hakika, huyu mtu anataka ateuliwe kuwa mshauri wake au nini?? Press Sec or so? Maana hadithi za Bulgaria na Roumania zinaashiria nini kwa kirefu namna ile? Halafu hivi kweli mshikamano alio nao mwandikiwa na hao mafisadi ujasiri wa kuuvunja unaweza tokana na barua hii? Kichwa kimeniuma!
 
Ulimwengu ni mwandishi mzuri mkuu, nadhani atakuwa ameandika kama MOCKERY au Joke fulani kumconscietize mkwere afumbue macho hata kama hataki kuyafumbua!

Hapana ni kama waungwana walivyosema. Anawinda kitu kama wawindaji wengine wa siasa za TZ. Mara baada ya Mkapa kuondoka kila wakati alijitahidi sana kuonyesha kwamba, kaja Kikwete mtu wa maana. Kipindi cha Ulimwengu on Monday kiliwinda wale wanaomusifu mkuu huyu. Naona bado hajapata alichokitaka na sijui kama alistahili ile nafasi anayoibaka Salva.
 
Byendangwero,

Nakushukuru sana kwa kutumia uhuru wako wa kueleza tafsiri na hisia zako juu ya jenerali. Ulijua fika kwamba ukiandika kuhusu jenerali kupotoka kifikra kola mtu atahamaki na kufuatilia kwa makini. Umefanikiwa kunihamakisha na nimelazimika kusoma kila kitu kwenye hii thread, kwa kutumia ka-simu kangu kadogo.

Nasikitika umenipotezea sana muda lakini naamini kulingana na michango ya mawazo iliyonitangulia utakuwa umejifunza na kwamba hutarudia tena kutumia haki yako ya kujieleza kusumbua wenzio.

Jambo pekee ambalo nalisemea kwene makala hii ya jenerali ni kwamba hakuwa na muda wa kutosha kui-update. Tukumbuke kwamba umri wa jenerali haurudi nyuma. Anakua kifikra lakini kasi yake ni lazima ianze kupungua. Tunatakiwa kumvumilia na kumsaidia.
 
Nafikiri Ulimengu amerudia barua hiyo ili mheshimiwa aweze kupima mwenyewe kama ametimiza yale aliyoambiwa mwaka 2005.
 
Jenerali anatamani kum evennge BWM through JK, kila ukimsoma ktk makala zake na hata pale anapopata public forum huwa anashindwa kusahau bif yake na Mkapa regime na kibaya zaidi anashindwa kubainisha publicly kuwa alionewa lakini matendo yake yanabeba ujumbe huo. Ninadhani Jenerali anapaswa kuandika kitabu kinachoizungumza Tz mpaka regime ya BWM maana kuna wakati nahisi anasukumwa na mentality ya kidini lakini inakuwa ngumu sana kumconnect directly. All in all tutaendelea kumsoma ili tujifunze ktk +na -
 
ila yeye ktk utangulizi this time amesema kuna marekebisho kidogo ameyafanya na tukumbuke itaendelea next week
 
Nafikiri Ulimengu amerudia barua hiyo ili mheshimiwa aweze kupima mwenyewe kama ametimiza yale aliyoambiwa mwaka 2005.
Njaa mbaya jamani...adui yako umuombee njaa tu.Opportunism at the highest level.
Acha nijibebee mabox mie huku kwa wahindi.
 
Barua zanamna hii zinahitaji kuandikwa kwa watu wenye uwezo wakutafsiri fasihi simlizi vizuri vinginevyo sina uhakika aliye andikiwa barua hii na rafiki yake kama anamuda wa kuisoma na kuchukua maudhui yake nakuyaweka katika picha halisi.pia siamini kama ulimwengu analengo lakuleta mabadiriko yoyote katika taifa hili kupitia barua yake, kwa mfano ameomba msamahaa hata kabla aliyeandikiwa barua hajaisoma kana kwamba akimwudhi,je Ulimwengu unategemea usimwudhi?je hayo uliyo yaandika unategemea yawe na mtazamo chanya kwa huyo rafiki yako?lengo lako ni lipi? kukosoa, kushauri,kutoa mwelekeo au kueleza hali halisi iliyopo? kama lengo lako ni miongoni mwa hayo maswali una ombaje msamahaa?.
Pia unasema kama mheshimiwa rafiki yako atupilie mbali walaka wako kama ataona unamchosha kwa vile nimrefu.Hapo mantiki ya kuandiaka walaka wako ni nini? kama una mwandikia mtu walaka halafu hujari kama atasoma hivi lengo lako linakuwa ni lipi? hapa naona unatimiza wajibu wa nafsi yako lakini sidhani kama una nia dhabiti kama inavyo tafsiriwa nawengi

@kereng'ende

Umeanza vizuri lakini mwisho unajiuliza maswali ambayo majibu yake ushayatoa,naomba usome sentensi ya kwanza ya uliochoandika.
 
Mkuu nafikiri hujaelewa mantiki ya Ulimwengu kurudiaile barua aliyomwandikia JK mwaka 2006 mara tu ya Jk kula kiapo cha kuiongoza Tanzania.

Ukiielewa kwa makini utagundua kwa nini Ulimwengu ameamua kuichapisha tena barua hiyo kwenye toleo la Raia Mwema la wiki iliyopita.

Jaribu kufuatilia makala ama hata mijadala ya Jenerali Ulimwengu na utagundua ni mtu wa calibre gani!!


Umenena! Niliisoma hii barua, ambayo Ulimwengu anatoa tahadhari kuwa ni ndefu! Maudhui ya maandishi yale sio ya kumpamba JK hata kidogo! Anamsihi aishi kwa lile alilotegemewa na wapiga kura. Anamkumbushia jinsi wapiga kura walimwona mkombozi na jinsi hizi njozi zinavyozidi kutokomea. Anamwambia 'sitaki nikufundishe kazi'....nadhani Jenerali amegonga habari yake vizuri na kama JK ni msomaji atagundua rafiki wake wa zamani anamhofia anazidi kuikimbia ile sifa aliyoipata 2005, ya wapiga kura kudiriki kumwita Mkombozi!
 
Mwanamageuko

Kunapointi hapo
Yote hayo ni katika kutafsiri barua ya Jenerali, na sikufichi, barua hiyo ukikaa chini na kuamua kuiandika upya kwa tafakuri ya kina neno kwa neno unaweza kutoa kitabu kizima cha kurasa zisizopungua mia na ushei.

Hebu tazama wale wanaojilipa kwa safari wasizoenda, ni nani anawakemea? Hebu tazama wale wanaowaacha walengwa katika ajira wakawaweka ndugu zao? hebu tazama wale wanaosaini mikataba bila kuisoma na kuangalia madhara yake wakati ujao, ni nani anawahukumu? hebu tazama wale wanao-zuilia waleta maendeleo nchi hii, nani anawajua? hebu tazama wale wanaotumia nyadhifa zao kwa manufaa yao, ni nani aliyejaribu kuwapigia kelele? Na kuendelea....
 
Uzuri wa JF ni tofauti kabisa na vikao vya CCM ambapo watu wanafoka huku mate yakiwatoka, Ndio Mwenyekiti. Hapa watu wanakubaliana kutokukubaliana. Mimi naona tutakuwa hatumtendei haki Ndugu Ulimwengu kama tutamuukumu kwa kutumia kipande kimoja cha barua, nadhani tusubiri mpaka tusome wiki ijayo ndio tutapata maana halisi ya ile barua.

Kutokana na kipande nilichokisoma mpaka sasa, hiki ndio nilichokiona. Ndg. Ulimwengu ameanza kwa kumpongeza Mheshimiwa JK kwa kuchaguliwa kuwa Rais (2005), na amemwambia ya kuwa wananchi wanaexpect nini kutoka kwake. Ikumbukwe mwaka 2005 , wananchi wengi walidhani Kikwete angekuwa mkombozi wao na ndio maana alichaguliwa kwa 81%. Kitu alichofanya Jenerali kwa kutumia hiyo metaphor ya "Mkombozi" ni kuzungumza kitu ambacho kilikuwa obvious.

Ulimwengu hakuishia hapo, anajaribu pia kumwonyesha Rais mteule jinsi alivyokuwa humble wakati wa ujana wake! Lengo kubwa hapa, ni kujaribu kumtahadharisha kwamba dhamana hii aliyopewa na wananchi isije ikambadilisha character yake. Ulimwengu anajua ya kuwa POWER inaweza kumbadili mtu...
 
Nimeisoma hiyo barua yote mwanzo mpaka mwisho, sijaona Ulimwengu alipomuita Kikwete "mkombozi". Sijaona katika barua hiyo aliyoitoa mkuu Questt hapo juu, labda katika maendelezo ambayo hayajawekwa hapa.

Wanaosema Ulimwengu kamuita Kikwete mkombozi naomba muweke hiyo sehemu katika quote nielewe zaidi, labda nimepitiwa.

Lakini pia, pale mnapofikiri Ulimwengu kamuita Kikwete mkombozi, mnaweza kuwa mmekosea na kushindwa kuelewa. Kama alivyosema mkuu mmoja hapo juu, Ulimwengu anaandika "too literary" au "too theoretical" kwa wengi wetu wasomaji wa kitanzania ambao tumezoea kutafsiriwa na kuambiwa "huyu fisadi, yule mbaya, huyu mzuri". Ulimwengu akija na kutotaja mtu na kuongelea sifa za kiongozi mkombozi, na kusema siku hizi kuwa mkombozi ni vigumu sana, na kumtaja Kikwete with diplomatic graces, wengi tunatafsiri kwamba kamuita Kikwete mkombozi. Mimi sijaliona hili, labda mnionyeshe.

If anything Ulimwengu anasema watu walikuwa na high expectations kwamba Kikwete atakuwa mkombozi na miracle worker, raising the bar. Sasa ukichanganya hilo na style yake ya ku meander literary, ni rahisi sana kumtafsiri vingine.
 
Back
Top Bottom