Ng`wanakidiku
JF-Expert Member
- Apr 18, 2009
- 1,195
- 232
Great Thinkers,
Pamoja na ugumu wa maisha kwa watanzania, lakini hatuna budi kumpongeza Mh. Rais kwani kalitumikia taifa ktk mwaka 2011 kwa juhudi zake zote ktk kuhakikisha uchumi unaimarika na pia kudumisha amani. Japokuwa naamini kuna mengi alipaswa kuyafanya, nadhani tumtie moyo na kushirikiana naye ktk kujenga uchumi wetu, kwani yeye peke yake bila sisi wananchi kushirikiana ktk nyanja zote nchi haiwezi kuondokana na mambo yote ambayo tunahisi ni kikwazo ktk kufikia maisha yaliyo bora kwa kila mtanzania. Wewe kama kijana, mzee, mama, dada, au uwe ktk uongozi wa kifamilia (baba au mama au kaka) au uongozi wa kampuni, nadhani tunapenda japo kupongezwa hata kama hatujaweza kufikia lengo tulilojiwekea. Naomba tuungane ktk hili!
Mungu ibariki JF!
Mungu wabariki wana JF!
Great Thinkers daima mtadumu!!
Wenu Ng'wanakidiku!
30.12.2011
00:30 am