Kwa hili CHADEMA mmekurupuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili CHADEMA mmekurupuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Apr 20, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wana JF

  Mimi ni mmoja wa watu wanao amini kuwa CHADEMA ni chama makini hata zaidi ya chama chochote kwa sasa hapa Tanzania. Lakini kwa hili mlilolifanya la kutaja list nyingine hapa mmeingia mkenge bila kujua. Siimanishi kuwa mliowataja sio mafisadi ila mmekwenda kwa hisia zaidi bila kuafanya timing haukuwa wakati muafaka kwa kuwa sasa mnaonekana kuwa baada ya kuiona CCM inajisafisha mnatafuta kitu cha kuwachafua ili waendelee kugombana. Hili watu wanaweza kulichukulia kuwa hata waliotumuliwa na ccm si mafisadi kweli kweli bali ni mambo ya kisiasa kitu ambacho si cha kweli. Na hoja ya ufisadi mlioianzisha ambao umeifikisha nchi yetu hapa ilipo ikaonekana ni mambo ya kisiasa haina uhalisia.

  Halafu ni washauri kitu kingine kuwa CCM inapofanya jambo jema kama walivyofanya ya kutimua mafisadi si mbaya makawapongeza kama kweli lengo ni kuwatetea watanzania pia mnaweza kuengeza kuchambua mapungufu ya yale mazuri ccm waliofanya kwa mfano haiwezekani mtu akawafisadi na kufukuzwa na chama alafu akawa mzuri kwenye nafasi ya ubunge. Lakini kukimbilia kuongeza list tena ya watu ambao jamii hasa sisi tuliohuku vijiweni (site) tumeshawaamini kuwa ni wasafi japokuwa wanaweza wasiwe wasafi mmeingia choo cha kike kama msemo wa watoto wa mjini wanavyosema.

  Kwa hili mimi CCM nawapongeza lakini bado wananuka sana kiasi ambacho siwazi kwa sasa kuwapa kura yangu. Lakini something is better than nothing.
   
 2. Panga La Shaba

  Panga La Shaba JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 209
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Mkuu Joblube ni fisadi yupi aliyetimuliwa CCM??,nachojua mimi CCM wamefanya mabadiliko ya viongozi ndani ya chama,lakini hakuna mtu aliyefukunzwa kwenye chama kwa kigezo cha ufisadi,CDM wanachofanya kwasasa ni kuhabarisha uma,tena ikiwezekana kila siku wawe wanatoa list ya mafisadi mpaka uwanja ujae.....
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Nionavyo mimi CDM wamepatia kabisa considering hali ndani ya CCM
  CDM wamezidisha ugumu wa mambo kwa CCM kwani AR,AC,EL wanaweza kujitetea na wasiondolewe kwa hoja ya kuwataka mafisadi wote waenguliwe na kuuzuga umma kuwa kwa sasa ni chama kisafi

  IF NOT FOR THIS FISADI LIST (pamoja na list of shame) CCM wangeliwaondoa mapacha watatu kirahisi

  for sure Dr.Slaa kapuliza kipenga muda sahihi sana kuzuia kuenguliwa kwa mapanda ndani ya CCM ili kibaki na sifa yake ya UFISADI

  slaa hawasaidii mapacha bali amelenga kuenguliwa kwa mfumo mzima wa CCM miaka ijayo.(IF CCM wana nia ya dhati wawaondoe mafisadi serikalini na sio kwenye chama tu)

  Kwa huu wakati lazima mapacha wamepata utetezi muhimu wa kuendelea kuibomoa CCM
   
 4. Muadilifu

  Muadilifu Senior Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  I think there is a point here.
   
 5. F

  Fareed JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ahsante Joblube kwa kuleta thread hii. Ni jambo la msingi sana. Timing is everything. CHADEMA wametumiwa na Rostam Aziz na Edward Lowassa bila wao kujijua. List of Shame hii mpya waitoe baada ya siku 90 walizopewa mafisadi hawa ili tusije kuwasaidia katika mbinu zao chafu za kuzuia wasifukuzwe CCM. Lengo lao ni kuibua tuhuma mpya dhidi ya viongozi wengi CCM ili defence yao kwenye kikao kijacho cha NEC kiwe mbona tumetuhumiwa wengi, ikiwemo Kikwete, Sumaye, Magufuli, na wengine basi hatua zichukuliwe kwa wote.

  Ukweli ni kuwa tuhuma dhidi ya Lowassa, Rostam na Chenge ni very serious, zimeenea nchi nzima na wenyewe ndani ya serikali na CCM wanajua ni za kweli. Wangetakiwa kuwa jela hawa watu, ila bado kuna kulindana serikalini.

  Mimi nilileta thread inayofanana na hii ila moderators kwa "busara" zao waliamua kuitoa na kuificha ndani ya thread nyingine.

  Chonde chonde moderators msifute thread hii wala kuificha ndani ya thread nyingine. Ni muhimu kujalidi suala hili kwa kina kwa maslahi ya taifa.

  Thread yangu iliyotolewa na moderators ni hii hapa:

  CHADEMA yatumika kuwaokoa Rostam, Lowassa wasifukuzwe CCM!

  CHADEMA sasa imeanza kutumika kuwasafisha Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge wasifukuzwe kwenye nafasi zao za uongozi ndani ya CCM.

  Kutumika kwa CHADEMA ni sehemu ya mkakati wa Rostam, Lowassa na wenzake kuzuia wasifukuzwe kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) na nafasi zao nyingine za uongozi.

  Mkakati huo unahusu kuitumia CHADEMA na viongozi wa vyama vingine vya upinzani, kama CUF, NCCR Mageuzi, UDP, TLP na DP ya Christopher Mtikila, kutoa tuhuma za kupikwa kwa viongozi wengi zaidi ndani ya CCM ili ionekane kuwa viongozi wote wa CCM wana tuhuma za ufisadi na si Lowassa, Rostam na Chenge tu.

  Tuhuma hizo za kutengenezwa sasa zimeanza kusambazwa na kina Rostam dhidi ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Jakaya Kikwete, na viongozi wengine waandamizi wa chama ambao wanaheshimika katika jamii, akiwemo John Magufuli, Samuel Malecela, Frederick Sumaye, Samuel Sitta, Bernard Membe na wengine.

  Rostam na Lowassa wanaitumia CHADEMA ili kuzuia kufukuzwa kwenye CCM kupitia LIST OF SHAME mpya ya chama hicho cha upinzani ambayo imewataja kina Magufuli na Malecela. Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilibrod Slaa, ameingizwa mkenge
  na viongozi wenzake ndani ya chama hicho kuitoa LIST OF SHAME mpya bila kujua kuwa mpango huo umepikwa na kina Rostam.
  Rostam na Lowassa kwa kutumia viongozi wa CHADEMA ambao wako nao karibu wamemuingiza mkenge Dk. Slaa aitoe List of Shame mpya ili kuleta mvurugano ndani ya CCM.

  Siyo "coincidence" hata kidogo kuwa CHADEMA waliibuka na LIST OF SHAME yenye majina mapya siku chache tu baada ya CCM kuwataka kina Rostam, Lowassa na Chenge wajiuzulu.

  Inaeleweka wazi kuwa Rostam na Lowassa wako karibu sana na baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA (siyo Dk. SLAA) na wamekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara nao.

  "Wanachotaka kufanya kina Rostam, Lowassa na Chenge ni kuibua tuhuma mpya za uongo dhidi ya Kikwete, Magufuli, Malecela, Sitta, Mwakyembe, Sumaye na viongozi wengine wa CCM ili wapate kujitetea kwenye vikao vya NEC vijavyo kuwa mbona kuna viongozi wengi za CCM wenye tuhuma lakini wanatakiwa wajiuzulu wao tu," alisema mpambe mmoja wa Lowassa.

  Pia, Rostam na Lowassa wamekuwa wakitumia baadhi ya magazeti, likiwemo Tanzania Daima linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, katika mkakati huo wa kuibua tuhuma za kupikwa za ufisadi dhidi ya viongozi wengi zaidi ndani ya CCM ili wajinurusu kufukuzwa.

  Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wiki hii CHADEMA ililazimika kukanusha habari za Tanzania Daima, gazeti la mwenyekiti wa chama hicho, zilizodai kuwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ametajwa kwenye List of Shame mpya ya CHADEMA.

  Lowassa amemuajiri mhariri mkuu wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, kwenye jarida lake la UMOJA na amekuwa akimtumia Kibanda mara kwa mara kutoa habari na makala za kumsafisha Lowassa, Rostam na Chenge kwenye Tanzania Daima.

  Inafahamika wazi kuwa Kibanda ana urafiki wa karibu sana na Lowassa na Rostam na amekuwa akitumiwa mara kadhaa kuwachafua maadui zao, ikiwemo Samuel Sitta, Bernard Membe, Harisson Mwakyembe, na wengine.

  Mafisadi wamekuwa wakipenda kulitumia sana Tanzania Daima mara nyingi kujaribu kujisafisha kwa kuwa linaheshimika kwenye jamii kwa kuonekana kuwa gazeti "huru" kuliko magazeti ya RAI na Mtanzania yanayomilikwa na Rostam.

  Kwa kufuata maelekezo ya Lowassa, Tanzania Daima juzi iliandika habari ya uongo kwa makusudi kuwa CHADEMA imemtaja Sumaye kwenye List of Shame mpya.

  Bado ni kitendawili kikubwa kwa nini Mbowe anamruhusu mhariri wake mkuu, Kibanda, kuwa mwajiriwa wa Lowassa na hivyo kuwa na mgongano wa kimaslahi na kimaadili (conflict of interest/ethical dilemma) katika kazi zake Tanzania Daima.

   
 6. M

  Marytina JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  ni sawa kwa mapacha kubaki ccm ili jina la chama cha mafisadi lisitokomee na hili litaifaidisha CDM kwa chaguzi zijazo
   
 7. Tekelinalokujia

  Tekelinalokujia JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu mi nafikiri imekaa hivi, sisiem walichofanya ni kujaribu kuweka raia sawa maana wameshaona wanapoteza mashiko kwa waTZ, wanasema wamejivua gamba sasa ni wapya, ila siku zote tunasema samaki mmoja akioza wote wameoza, na kwao waliooza ni kibao tuu, kubadili uongozi si isue kivile kama zile mbegu mbaya bado zipo chamani zitaleta influence zake huko ndani, makamu mwenyekiti ametangaza wazi kwamba kweli chama kilitoka nje ya mstari na kujikuta kikifanya fedha kua kigezo cha kupata nyadhifa, sasa ukibadili uongozi na kuwaacha waliooza si bado unajikuta unapambana na vita ileile? so Dr S anawasaidia kua mafisadi ndani ya sisiem (kama walivyokubali wenyewe kua wapo) ni wengi hivyo wasilete kiinimacho chao cha magamba, hata JK aliposhinda urais mara ya kwanza alituambia nguvu mpya ari mpya sijui na kasi mpya vile kumbe haikua kwaajili ya TZ ilikua kwa wajanja wachache huko kwao, sasa habari ya magamba bila kuona mabadiliko kiutendaji na mabadiliko katika kuiongoza serekali kuwapatia waTZ maisha bora hakuna jipya
   
 8. M

  MMASSY JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Nawewe mbona unatuma thtreads ambazo hujatafakari?kama CDM wangetakiwa kufanya hicho unachokisema basi hungekuwa unawapenda kam unavojinasibu.Unafanya hivyo kwa sababu tu wamethubutu kuwataja hadharani wale mafisadi bila kuangalia timing unayosema wewe.Ni bora ukajua kuwa ufisadi hauna sure,timing uaminifu n.k.Wewe ni nani kakuambia kuwa CCM wamewafukuza mafisadi?ni nani kati ya waliofukuzwa wewe unadhani ni fisadi?kama hao wewe unaowaita mafisadi Mwenyekiti wa chama chao kawapa siku 90 kujiondoa wenyewe,huoni anawaogopa?na nikupe tu taarifa kuwa tangia Mwalimu Nyerere ameng'atuka,ccm haijawahi hata siku moja na hakitakuja kuwafukuzaafisadi kwani wale ndio wakuu na makuhadi wa chama hicho.Kinachofanyika na viongozi hawa wa chama ni kama yale ya EPA nayo walipewa siku kama hizo na hadi leo fedha hazijarudi na hakuna aliyejeruhiwa kama sio wale dagaa wachahe.Subiri tu utaona kama watawafanyia kitu.

  CHADEMA HAKIWEZI KAMWE KUPONGEZA UOZO.LABDA UWATAFUTE WALE WALIOFUNGA NDOA NA CCM UWASHAURI HAYO

  NI HAYO TU
   
 9. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  okay!!,that's amazing!!!
   
 10. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni mtazamo wako tu.
   
 11. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Itaje hiyo point, si kila mtu anaiona kama unavyoiona wewe.
   
 12. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hivi ni nani aliyejua Raisi wa Tunisia anamiliki 40% ya uchumi wa nchi iyo na pia ni nani aliyejua raisi wa Misri amejilimbikizia mali ila palipokuwa panazungumziwa ufisadi hakukuwa na hatua yoyote iliyokuwa inachukuliwa sababu wao ndio walikuwa madaraka so ndivyo ilivyo kwa Tanzania wakati Dr Slaa akipambana nao naamini ajakosea ipo siku arobaini yao itafika.
   
 13. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo na wewe umeingia mkenge vilevile.

  kwani magufuli hajashiriki kuuza numba za gavamenti?
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  CHADEMA wanaweza kuendelea kuhangaika na watu ndani ya CCM. Sio vibaya na hasa inapokuwa ni mwaka wa uchaguzi. Baadhi tulitaka watuambie sera mbadala wa hizi za CCM kwenye mambo yanayowagusa mojakwamoja Watanzania kwa mfano:
  -Huduma za jamii.
  -Ugharamiaji wa SIASA na WANASIASA.
  -Uchumi, uwekezaji, uwezeshaji, uondoaji umasikini wa watu na nchi yetu.
  -Mapato, matumizi ya fedha na rasilmali za NCHI.
  Na mengine mengi.
   
 15. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ewe ndugu acha kuyumba yumba kama mbayuwayu, kuwa focused kidogo, DR Slaa alisema majina yalitangazwa kutokana na mazingira husika alipokuwapo (Tabora) na sio huko tu kuna sehemu nyingi sana Tanzania hawajui kama kuna mtu anaitwa ROSTAM, au kuna mafisadi, kwa hiyo Muhimu ukaelewa hilo. Lilikua ni suala la kimazingira zaidi kulenga kufikisha ujumbe kwa watu wa eneo husika na kuongezea majina mengine kwenye list ya mafisadi ile ya Mwembe yanga (List of Shame)
  [FONT=&quot]
  Pia kama ni mfuatiliaji Sio kazi ya Chadema kuwapongeza CCM bali kuwadhoofisha na kuonesha mbadala wa Chama tawala kama kitapewa nafasi ya kuongoza nchi kitafanyaje, ndio kazi ya chama cha siasa tena kisheria kabisa!

  Naona unayumba yumba pamoja na mada yako inaamia kuipongeza CCM, Nashauri ni heri ungeweka Title ya Post yako iwe Nawapongeza CCM. Au Chadema Acheni Wivu!

  NB: Wanaoamini katika Chadema ni watu makini na wenye msimamo, wasioyumbayumba, Wewe JE?[/FONT]
   
 16. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  kaka u have spoken the truth, it was a wrong timing for cdm to mention the names au unless cdm wanataka kuonekana wao ndio wameshinikiza watu fulani kuttimuliwa CCM,Ili baadae ionekanekane kana kwamba bila wao kutaja majina basi jamaa wasingefukuzwa! this is old tactic ni vizuri umeliona hili na umelizungumzia! ishu ya magufuli kuuza nyumba,si swala la leo kwanini leo ndio wanaona ndio ufisadi?? Slaa alipokuwa bungeni mbona hakuonekana kulivalia swala la uuzaji wa nyumba hizo wakati huo alikuwa mbunge mtu ambaye ana dhamana kubwa sana,hizi kelele anazopiga sasa hazina mashiko coz he is just a mere person( just a party secretary)
   
 17. J

  Joblube JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hoja hujibiwa kwa hoja wapi nimeyumba kwa kitendo cha CCM kutambau kuwa ndani yao kunamafisani hii ni hatua na ndio niliyoipongeza. Punguza ushabiki chambua hoja.
   
 18. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  bangi za huko vijiweni unaleta hapa ,,endelea kuvuta bangi,

  KUNA MTU GANI AMBAYE ANAAMINIKA NDANI YA CCM NA SERIKALI YAKE??HUYO MWAKYEMBE NA SITTA WENYEWE NI MAFISADI WA KUTUPA KWENYE MAENEO YAO YA KAZI

  CHOO CHA KIKE UMEINGIA WEWE TENA MBAYA ZAIDI UMEINGIA UKAMKUTA MWANAO WA KIKE
   
 19. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mbona umeangalia upande mmoja tu wa shilingi japo kuna pande mbili?Ngoja nikusaidie kidogo maana JF ni shule yabure,no need for tuition fees.

  Walichofanya Chadema this time could be even more effective than when they made public the first LIST OF SHAME.Kwa upande mmoja,Chadema wameamua kuutangazia umma kuwa ufisadi ndani ya CCM sio tu the so called magamba yaliyovuliwa bali tatizo hilo ni extensive zaidi.Kwa upande wa pili,na hili ni muhimu zaidi,Chadema wameiweka CCM katika wakati mgumu zaidi.Hebu jiulize,je Nape au Mukama wakienda mikoani na kusema "mafisadi lazima wajiondoe2 watakuwa wanamaanisha mafisadi wapi?Wale wa mwanzo,hawa waliotajwa sasa,au wote?

  Na kama by mafisadi wajiondoe itamaanisha akina Lowassa pekee,then nao watahoji "kama mmeamua kutufukuza kwa vile tu tumetajwa na Chadema kuwa sie ni mafisadi,what about hao walioongezwa kwenye list?".Remember,hadi sasa serikali ya CCJM haija-produce ushahidi kuwa Lowassa na wenzie ni mafisadi.So far,chanzo pekee ya ufisadi wao ni kauli za Chadema.In similar way,chanzo pekee cha ufisadi wa akina Malecela,Mangula na Magufuli ni Chadema.

  Kwahiyo wakati unazungumzia timing,unazembea kuangalia ESSENCE ya mkakati huo.Kadhalika,ni muhimu kwako kutambua kuwa mapambano dhidi ya ufisadi,ambayo Chadema imeamua kuyavalia njuga kwa kushirikiana na watanzania wote wazalendo,ni mithili ya kuwa vitani.Adui anapojaribu kuzorotesha mapambano,ni jukumu la makamanda wa vita kuboresha mbinu lakini bila kusima awala kuathiri mapambano.

  Pengine ungeweza kutusaidia zaidi kwa kutueleza ushauri wako as to ungependa Chadema wafanyeje baada ya CCM kuwahadaa Watanzania kuwa imejivua gamba la ufisadi.Did you want or expect Chadema kutuma salamu za pongezi?Na kama Chadema walikuwa na orodha ya ziada ya mafisadi ungependa waitangaze mwaka 2015 au?

  Kwa taarifa yako tu,Chadema wana orodha ndefu zaidi ya mafisadi na wataendelea kui-update ile original ya Mwembeyanga kila unapojiri wakati mwafaka.Lengo sikumfurahisha kila anayesikia,especially mafisadi na wapambe wao.This is a war kila Mtanzania mwenye uchungu wa kweli na nchi yake cant afford to lose.
   
 20. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Your sympathy for CCM is too late. Go repent elsewhere.

  Hakuna cha kuwapongeza CCM kwa usanii wako uchi na ufisadi wanatakiwa waambiwe kila siku wavae nguo na waondoke madarakani au wakakae na wazimu wengine walio uchi. Kwa bahati mbaya hawajali wakishambuliwa huja na hoja "amani na utulivu tuliyo nayo toka uhuru". It is a joke where is Sinapore, Malasia with the same age of uhuru? Kama wanaufisadi ni ule kwa manufaa ya nchi. CCM ni kwa manufaa ya kikundi kidogo cha mafisadi kwa gharama za watanzania. Bravo Slaa bravo CDM Bravo all fighting for change
   
Loading...