Filipo Lubua
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 339
- 578
Wenzangu WanaJF,
Nikiwa mnazi mkubwa wa mabadiliko yasiyoogopa gharama yoyote, naomba niwe kinyume na hili walilolifanya viongozi wa Chadema katika maandamano ya juzi kwa kile walichokiita kumshinikiza Anna Makinda Angoke kwenye kiti.
Kwa ujumla kila kitu kilifanyika vyema kabisa, hata kutoa namba za Anna Makinda kwa wananchi na dunia nzima bado ilikuwa sahihi. Viongozi wa Chadema, Zitto na Lema, walizisoma namba za Makinda waziwazi bila hata kificho. Hilo bado sioni kama lilikuwa tatizo.
Tatizo kubwa nilionalo ni kwamba, viongozi hawa hawakuwapa elimu wananchi kama namba zile zilikuwa zina umuhimu gani hasa. Wananchi hawakuelimishwa kuwa namba zile zilikuwa za kutuma maoni kwa Anna Makinda, maoni ya busara na yasiyo na matusi.
Katika hali ya namna ile, wananchi wataanza kumtukana Spika Makinda, bila hata kujua kama ni kiongozi mkubwa wa nchi. Wananchi wangetakiwa waelimishwe umuhimu wa kumhitaji Anna Makinda ajiuzulu lakini kwa lugha yenye staha na maneno ya hoja.
Ni wazi kuwa, kwa mfumo wa mawasiliano wa nchi yetu, bado wengi waliweza kutumia kadi za simu zisizosajiliwa na kumvurumishia Spika matusi (kama gazeti moja lilivyokwisha kuripoti).
Yawezekana bado hajatukanwa, ila yawezekana akatukanwa pia. Sharti tukubaliane kuwa watu hawakuelimishwa kuwa kuna madhara (repercussions) iwapo watamtumia jumbe za matusi. Ikiwa jumbe alizokwisha kutumiwa (au atakazotumiwa) zitakuwa zina matusi, hili litahafifisha hoja ya msingi ya Chadema kutaka kumng'oa Makinda (jambo ambalo mimi binafsi nisingependa litokee).
Kwa Chadema kutowaelimisha wananchi namna bora ya kumwandikia Makinda/Ndugai ujumbe, hili ni kosa; na matusi yote atakayotukanwa Makinda (maana kweli watu wamemchukia) itakuwa ni lawama kwa Chadema. Kwa kweli, bila ushabiki, kwa hili Chadema walikosea.
PEOPLES POWER!!