Kwa hili CCM wana wakati mgumu, Awamu hii

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
408
Kwa mujibu wa katiba ya znz ya mwaka 2010,znz inatambulika kama nchi yenye wimbo wake,bendera yake na amiri jeshi mkuu. Suala la kuchakachua maoni ya wananchi kweny BMK,likiwemo la kuondoa serikali 3 litawaumiza siku zote. Na niseme wazi tu kuwa hamtapata nafasi ya kulisemea mahali popote. Na niwaonye tu kuwa,kama mnajipenda,msizungumzie suala la katiba mpya hata siku moja kuelekea uchaguzi mkuu.
Nina maswali ambayo mwanaccm anatakiwa anijibu.
Mosi,kama katiba ya ZNZ inaitambua zanzibar kama nchi,hawa watangaza nia wanapata wapi ujasiri wa kwenda kuomba udhamini wakati ile ni nchi nyingine?
Pili,kama wazanzibar wanaitambua zanzibar kama nchi,je wanapata wapi uhalali wa kuomba kura bara? Unawezaje kuwa rais kutoka nchi nyingine?
Tatu,rais wa JMT atakuaje rais wa nchi mbili Tanzania bara na Zanzibar?
Nne,waliotangaza nia kupitia CCM watapigaje kampeni nchi ambayo sio raia?
Fursa kwa UKAWA: watumie udhaifu uliofanywa na BMK kuchakachua maoni ya wananchi kuwambia wananchi mchakato wa kudai katiba mpya uko pale pale. Huwezi kuwa rais wa nchi mbili kwa wakati mmoja. Huwezi kuwa mgombea wa urais kutoka nchi ya ng'ambo au nyingine. Iweje raia wa nchi nyingine ya ZNZ awe rais wa nchi nyingine? Iweje tutawaliwe na rais kutoka nchi nyingine?
 
Back
Top Bottom