Kwa Hili, 2015 ni Mbali sana.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Hili, 2015 ni Mbali sana....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STK ONE, Mar 30, 2012.

 1. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakipenda sana kipindi cha akina Zembwela na Michael Baruti. Zembwela anapenda kusema kuwa "Yasiyowezekana nchi nyingine yoyote ile, Tanzania yanawezekana." Naomba kuongeza kitu, "Yasiyowezekana nchi nyingine yoyote ile hapa duniani, Tanzania chini ya CCM ya Kikwete, Yanawezekana." Mfano kuiba twiga kwenye ndege, kukodisha ardhi kwa Tsh. 200/- kwa mwaka kwa miaka 99. Haya hayawezekani sehemu yoyote ile duniani, ni TANZANIA TU, TENA CHINI YA CCM NA KIKWETE.

  Nimepatwa na uchungu mkubwa sana kutokana na thread ambayo imepostiwa na COMMITED inyohusu kuchukuliwa kwa ardhi ya Mpanda kwa gharama nafuu kuliko unafuu wenyewe. Nakumbuka ilikuwa mwezi wa kwanza au wa kumi na mbili hivi, baada ya Pinda kuzomewa na wananchi wa Mpanda mjini mwishoni mwa mwaka jana, aliamua kumualika Kikwete kwenda mpanda akiambatana na akina Idd Simba wakiambatana na wazungu wa Agrisol zaidi ya mia moja. Pinda alizomewa baada ya wananchi kupinga kitendo cha serikali kupitia yeye (Pinda) kuibinafsha ardhi iliyokuwa inakaliwa na wakimbizi katika maeneo ya Katumba na Mishamo wilayani Mpanda.

  Kuzomewa kwa Pinda kulikuja baada ya yeye kutaka kuwadanganya wananchi kuwa kulikuwa na faida kubwa katika kuwekeza katika ardhi ambayo nimeitaja hapo juu. Lakini kabla ya Pinda, Mbunge wa Mpanda mjini (CHADEMA) Said Alfi, alikuwa amewaambia wananchi kila kitu ambacho kilikuwa ndani ya mkataba wa Agriso na Serikali. Kwa hiyo PInda alipofika Mpanda alitaka kuwadanganya wananchi na ndiyo chanzo cha Kuzomewa. Hili lilipelekea Pinda kumualika Kikwete kuwaleta wale wazungu Mpanda, kwani aliamini kuwa akiwa peke yake asingeweza kusikilizwa.

  Pinda tangu uchaguzi wa 2010 amekuwa akidharauliwa na kuchukiwa sana Mpanda mjini. Japo wanasema kuwa nabii hakubaliki nyumbani, lakini kwa Pinda ni too much. Hasira za wananchi wa Mpanda mjini juu ya Pinda, zilianza baada ya Pinda kuchangia kwa asilimia zote kuchakachua matokeo ya Ubunge Sumbawanga mjini, kwa kumpa ushindi Aish (CCM) ilihali aliyekuwa ameshinda ni mgombea wa CHADEMA. Lakini hili la kuwaleta wawekezaji kwenye ardhi ya Mpanda kwa bei ya kutupa, limewaongezea hasira sana wananchi wa Mpanda na kwa hili, Pinda hawezi kusimama kwa amani kwenye majukwa ya Mpanda mjini na kuhutubia, anaogopa kuzomewa tena.

  Naiona 2015 mbali sana. Nimewahi kuandika hapa jamvini kuwa kuing'oa CCM madarakani kupitia sanduku la kura ni kazi kubwa sana. Mimi kwa mtazamo wangu, bado naamini kuwa CCM itaondoka madarakani kwa shinikizo la wananchi wenyewe. Kama ambavyo anasema Nape kila siku kuwa CCM itatawala milele, namuunga mkono. Kama wanaharakati na wanaCHADEMA tunategemea kuing'oa CCM madarakani kwa njia ya kura, itachukua muda mrefu sana karibia na MILELE ambayo anaisema Nape.

  Najiuliza kama viongozi wa CCM na serikali yao wana akili timamu. Kuuza ardhi ya wananchi kwa hekta moja TSH 200/- kwa mwaka, na Tsh 500/- kwa kila ekari itakayolimwa, ni akili za mtu anayefikiria kweli???? Hii 200 ambayo haiwezi kununua ndoo ya maji ya lita 20 ndiyo ambayo tunalipwa wananchi wa Mpanda kwa mwaka??? Inaumiza sana. Hapa Mpanda kuna eneo linaitwa KAKESE. Eneo hili ni maarufu sana kwa kilimo cha Mpunga, huku tunakodishiwa ekari moja kwa TSH. 50,000/- kwa msimu mmja wa kilimo. Najiuliza, hivi tungewaleta wawekezaji wa ndani ya nchi, wakalima kwa kutumia mbegu asilia, na kuwakodishia ekari moja kwa Tsh. 50,000/- tungelishindwa kuendesha mashamba haya na kuongeza tija ya chakula? Kwa nini ngozi nyeusi tumekuwa tukitegemea sana wazungu kutukomboa katika kila kitu?

  Hivi kweli CCM inaamini kwa dhati kuwa tatizo la chakula litamalizwa na hawa wazungu ambao wanaingia kwa malengo yao? Pinda alituambia kuwa vijana wataajiriwa na kwamba wazungu wataongeza chakula. Lakini Mpanda hatuna shida ya chakula. Hadi sasa tunavuna mahindi ya mwaka huu, bado kuna magari kibao yanabeba mahindi kutoka Mpanda kwenye mikoa ya Tabora, Shinyanga hadi Mwanza. Tunahitaji wazungu kwa lipi? Kweli 200/- kwa mwaka....Pinda akili zake zina akili kweli? Tena bila aibu anajiita mtoto wa mkulima???? Shame on you Mizengo. Pinda hakulelewa na wazaze wake awe na akili za ajabu namna hii.

  2015 ni mblai sana. Kama kweli tunampango wa kuikomboa nchi hii, tuchukue hatua. Nimewahi kumwandikia Dr. Slaa kupitia jamvi hili kuwa Kuiondoa CCM madarakani ni ndoto kubwa sana ambayo haiwezi kutokea katika miaka ya hivi karibuni bila kuamua kutumia nguvu ya umma. Viongozi wa CCM watatutukana sana, Tutatawaliwa na Baba, mtoto hadi mjukuu wa ukoo mmoja na hatutakuwa na lolote la kufanya. japo wengi tunauona mwisho kuwa uko karibu, lakini karibu ambayo tunaiona sisi, ni miaka mingi sana.

  Mmarekani amewekeza sana hapa Nchini. Kuiondoa CCM madarakani ni kuhatarishi maslahi ya Marekani hapa nchini. Nafikiri mnakumbuka jinsi hoja ya DOWANS ilivyoisha baada ya Symbion kununua mitambo ile tena alikuja Hilaly Clinton na kuisifia sana. Hadi leo, hata wale ambao walikuwa wanapiga kelele kuhusu Dowans wametulia kabisa. Hata hawa AGRISOL ni wamarekani, migodi mingi imewekezwa na wamarekani. Kwa hiyo Mmarekani atatumia kila namna anayoweza kuhakikisha kuwa Vibaraka wake wanaendelea kubaki Madarakani ili aendelee kuchuma.

  Bajeti yetu bado ni tegemezi kwa kiasi kikubwa. serikali haina uwezo wa kukataa kusaini mikataba ya miaka 99 kwa shilingi 200 kwa hekari kama huu wa AGRISOL wa mpanda, kwa sababu watanyimwa nyongeza kwenye bajeti. Tunafanaya nini?

  Tumelalamika sana. Tumeongea mengi sana. Tumesema mengi pia. Nini tunafanya kuhakikisha kuwa hali hii haiendelei? Kama tutaendelea kusema U-CCM na U-CHADEMA wetu kwenye mambo ya msingi kama ARDHI, tutalipoteza Taifa hili na siyo Mwna CCM walla Mwana CHADEMA ambaye atabaki salama. Wengi wanaoshabikia CCM huko Arumeru mashariki, hawa wanaoshabikia CHADEMA ni MASIKINI wa kutupwa. Hawana mbele wala nyuma. Hakuna mwenye matumaini hata mmoja. Usione watu wamevaa Kofia za CCM na matshirt ya kijani na njano ukadhani wanapenda, hawana ALTERNATIVE. Hata ambao tunavaa kofia za CHADEMA, hatuna namna nyingine. Tukiendelea kusema CCM, na mimi CHADEMA, ardhi inayochukuliwa na maliasili zinazoporwa siyo za CCM wala siyo za CHADEMA, wala hata siyo za CUF, ni za WATANZANIA. Kuna siku CCM itapita, CHADEMA, CUF, NCCR na vyama vingine vyote vitapita, lakini TAIFA la TANZANIA lisimama milele. Hata kama maliasili zote zitachukuliwa na wazungu, milima ikianguka na nyumba zote na sisi wote kupita, bado TANZANIA itabaki MILELE NA MILELE.


  Tuna kufa masikini, kuishi kwa shida, hatuna matumaini ya kesho na ugumu wa maisha, siyo kwa wana CCM wala siyo kwa wana CHADEMA, wote tumepigika, wote tunanunua kwenye maduka yale yale, wote tunatibiwa kwenye hospitali zilizochoka na madaktari waliokata tamaa. Hata polisi wengi, ukiwatoa akina SAID MWEMA na wenzake wachache, hata wanajeshi, ukiwatoa akina DAVID MWAMUNYANGE na wenzake wachache, wote wanaishi maisha mgumu kama rais wengine. Angalia nyumba za askari polisi, niliwahi kuhisi pengine wanajeshi wanamakazi mazuri, nikiwa Morogoro mwaka mmoja, nikafika Mzinga, kwenye kambi za jeshi na kwenye kiwanda cha KUTENGENEZA SILAHA. Hali ni ile ile, nyumba mbovu, tena niliyefika kwake, alikuwa na cheo cha SAJENTI. Ana nyumba ya chumba kimoja na sebule, tena imechoka mno. Nashindwa kuelewa wanajeshi wamelishwa nini hata wavumillie maisha magumu namna hii?

  MWISHOOO....CCM kuondoka madarakani kupitia sanduku la kura, ni NDOTO, tena TUNAOTA MCHANA tukiwa hatuna hata LEPE LA USINGIZI. Tukiendelea kuimba U - CCM, U - CHADEMA, U - CUF na U - NCCR mageuzi, tutabaki kuwa mtaji wa matajiri wa ulaya na Marekani. Hadi siku ambayo tutaamua kuweza tofauti za dini zetu, kabila zetu, itikadi za SIASA na mengine mengi kando na kulipigania TAIFA letu na maliasili zake. Sina haja ya kusema Mungu ibariki Tz, MUNGU katubariki kila kitu, ni kitu gani ambacho hatuna hapa Tz? Tukisema Mungu tubariki, na wasomali, Sudani kusini, watasemaje? Tunashndwa na Rwanda ambayo imetoka vitani na sasa tunaiona kwa mbali....AIBU SANA.
  Tumeshabarikiwa, tuchukue hatua kuiondoa CCM madarakni na viongozi wake wabinafsi, tusipofanya hivyo, ataingia, LOWASA au HUSSEIN MWINYI 2015, kama ilivyo kwa SIOI SUMMARI huko ARUMERU.

  NAOMBA KUWAKILISHA......
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Ondoa hofu, watatoka!!!! any which way freedom must come. Napeegwa asikutishe, ni sawa na al-sahaf wa sadam huseni
   
 3. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sawa, mkuu, sipingi maoni yako, lakini unaamini kuwa ccm itaondoka kupitia sanduku la kura??
   
 4. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Lete evidence basi...
   
 5. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Nalisifu Andiko lako limegusa sehemu nyeti na muhimu tunayoikoisa watanzania "uzaendo" na tumebaki kuwa mashabiki tu wa vyama vya siasa!!Rafiki yangu mmoja aliona swala aliyetoroka kutoka momela national park akamuua ili ajipatie kitoweo yeye na familia yake jamaa wa mali asili walipopata habari wakamfuatawakamlazimisha ale nyama yote mbichi na ngozi wakampiga sana mwisho alikuja kufia hospitali!!Tukio hilo lillikuja muda mfupi tu kabla hatujasikia twiga na wanyama wengine wamekamatwa KIA na mpaka sasa hakuna aliyeulizwa kitu!! Watanzania hizi maliasili ni zetu au ni wazungu sisi tumepewa dhamana tu ya kuzilinda kwa ajili yao??Sasa wewe mleta mada hebu sasa buni mbnu B baada ya mbinu A ya kuwang'oa kwa kura kushindikana??
   
 6. S

  STIDE JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Wewe ni M*A*T*A*K*O!! Evidence ya nini!!? Yaani mijitu mingine sijui inaishi chooni!!? Kuna kitu gani ambacho mleta mada hakukielezea au ambacho hukifahamu hadi akupe evidence? Au hujui maana ya "evidence?"
  samahani mods mijitu mingine inakera jamani hadi uvumilivu unaisha!! "SAMAHANI"
   
 7. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,933
  Likes Received: 459
  Trophy Points: 180
  Safi sana mijitu inayokatisha tamaa ni kuwatupia kama hivo
   
 8. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  uhuru unakuja kwa watu kujitolea maisha yao kuutafuta, je wewe umejitoa?
   
 9. S

  STIDE JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Mkuu yaani kwa staili hii itatuchukua kitambo kuiona Tanzania tuitakayo!! Yaani madudu yooote aliyoelezea mleta mada eti mtu anataka evidence!! Kwamba hayajui hayo madudu au!!?
  Wakati mwingine huwa nashindwa kuelewa hawa pro-ccm huwa wanawaza nini, sidhani kama kuna raia hapa chini ya jua anajituma ktk kufanya kazi kama Mtanzania lakini hali bado duni kwa sababu ya utawala mbovu chini ya ccm!! Hawa pro-ccm wanatumia nini ktk kufikiri, wanapumbazwa na padiem za buku mbili ili waibiwe mabilioni!!? Wana ubongo gani hawa watu?
  SHAME ON YOU PRO-CCM!!
   
 10. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  umenigusa sana.
   
 11. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mimi nimejitolea, afadhali kufa katika harakati za kuikomboa nchi yako kuliko kufa kitandani kwa malaria!!
   
 12. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kusema ukweli wana Rukwa hawahitaji wawekezaji wa kukodishiwa ardhi, wanaRukwa ni wakulima tokea enzi na enzi. Kinachotakiwa ni kutengeneza miundombinu hasa barabara za kiwango cha lami ili waweze kupeleka mazao yao kwenye masoko. Mfano mzuri ni ghala ya taifa ya mazao ya nafaka pale Sumbawanga mjini, inatia uchungu sana unakuta mahindi yanakaa kwenye bohari mpaka msimu mwingine wa mahindi unayakuta mahindi ya mwaka uliopita. So in short wanaRukwa hawahitaji mwekezaji wa kuwafundisha eti kilimo bora au mwekezaji wa kukodisha ardhi yao, wana Rukwa wanahitaji barabara ziboreshwe waweze kuyafikia masoko kwa urahisi.
   
 13. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Be specific, unataka evidence gani, kwa sababu kuna vingi nimeandika kwenye thread...!
  evidence ya pinda kuchakachua matokeo ya sumbawanga mjini, au evidence ya kuporwa kwa ardhi mpanda, au evidence ya makazi mabovu ya askari polisi na wanajeshi???
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Mar 31, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  umesema yooote lakini hiki kipande ndicho hasa IMANI YANGU.......To remove CCM from power through ballot box..hell no!!

  tukipata jibu nini kifanyike basi ndio ukombozi wenyewe

  tukipitia ballot box tukabadili tume,na aina ya siasa tunazofanya it can be done...kinyume na hapo ni kupoteza nguvu nyingi sana kuongela yasiyokuwepo!!!
   
 15. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vijana tumekuwa tukitumiwa sana katika mambo mengi, mabaya na mazuri. Kwa sasa, population kubwa Tz, (japo sina statistic) ni Vijana. Na vijana ndio ambao tunahangaika na maisha kila kikucha. Ukichunguza sana, utagundua kuwa vijana tumekuwa mtaji wa wazee, kuwapa madaraka na sisi kubaki tukiwa hatuna kitu. Vijana tunaweza kumuweka madarakani mtu tumtakaye, lakini kikundi kidogo cha watu (tume ya uchaguzi na usalama wa taifa) kikaamua nani awe kiongozi wetu, japo hatukumchagua.

  Nini tufanye.....???? Kwanza, tuache kuimba nyimbo za UDINI, U-CHADEMA, U-CCM, U-CUF na U-NCCR. Tukiviweka vyote hivyo kando, tuunganishe nguvu, tuwaelimishe watu ambao bado hawana elimu ya uraia juu ya nini chanzo cha maisha magumu, nini chanzo cha kuporomoka kwa elimu, nini chanzo cha kuzoroka kwa huduma za afrya, nini chanzo cha ufisadi na ni nini chanzo cha laana tuliyonayo ya kushindwa kutumia maliasili tulizonazo Tz. Wakituelewa na kukubaliana na hoja zetu, tunaamua kuiondoa serikali iliyopo madarakani kwa sababu inaongozwa na adui wa nne wa taifa hili, baada ya MARADHI, UJINGA na UMASIKINI ambavyo vilibainishwa na NYERERE, sasa CCM ni ADUI MBAYA kuliko wengine wote, kwa sababu yeye ndiyo chanzo cha UJINGA WETU (Rejea mfumo mbovu wa elimu, ukosefu wa vyumba vya madarasa, wanafunzi kukaa chini na miundombinu mibovu ya ELIMU), yeye ndiyo chanzo cha UMASIKINI WETU, (Rejea matumizi mabovu ya rasilimali, kutoroshwa kwa wanyama, madini, mbao, samaki na kuporwa kwa ardhi), yeye ndiyo chanzo cha KUZOROZA KWA AFYA ZETU, (Rejea ukosefu wa huduma bora za afya, ukosefu wa madawa, ukosefu wa vitanda, akina mama kujifungulia chini na barabarani na takataka nyingine nyingi).

  Kwa hiyo kupigana na UJINGA, MARADHI na UMSINI ilihali tukiwa na CCM, chini ya Kiongozi yoyote yule (Siyo JK Peke yake), ni kazi bure, kwa sababu CCM ndiyo chanzo cha haya yote. TUTOE ELIMU KWA UMMA, KISHA TUAMUE KWA PAMOJA KUIONDOA SERIKALI YA CCM MADARAKANI, VINGINEVYO, WATOTO WETU WATATULAUMU KWA SABABU YANAYOTOKEA SASA YANATOKEA MBELE YA MACHO YETU.
   
 16. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimejitoa sana, kuhakikisha kuwa tunapata haki zetu, lakini ukumbuke kuwa tukifanya mmoja mmoja, hatuwezi kufanikiwa. Chama ambacho kimetawala nchi kwa miaka 50, kina mizizi mingi, kuking'a ni kazi kubwa, ndiyo maana napendekeza njia mbadala ya sanduku la kura, SOMA NILIVYOMJIBU OSOKONI hapa chini.
   
 17. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  SURE, nimemjibu vizuri OSOKONI, pls can try to see my alternative way hereunder?
   
 18. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,791
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Evidence hii hapa:kampuni ya EAST iliyochota tshs 2bn za jiji kujenga machinjio dar chini ya mkiti wake idd simba kisha ikafilisika!unata evidence nyingine?kibaraka wewe
   
 19. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,180
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  Kuna haja gani ya kufanya chaguzi kama ccm itashinda milele?
   
 20. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,521
  Likes Received: 5,666
  Trophy Points: 280
  hii nchi itakombolewa kwa nguvu ya umma tu!! Tunahitaji frontier very aggressive!! Wanasiasa sometimes wanaweka siasa badala ya vitendo!
   
Loading...