Kwa Heri Dr Slaa Karibu Lowassa

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,464
Gwajima ametoa dukuduku ametoa maungamo na katoa maisha ya kiroho ya muumini wake! ni kawaida kwa waumini kuwaamini sana wachungaji wao na hata kuwakaribisha mpaka chumnani wakiamini wanatibu roho zao. Gwajima kasaidia kumjua Dr Slaa na matatizo yake ya ndoa na jinsi mwanamke alivyo weza kutawala kichwa cha shujaa.

Kwa heri Dr Slaa umefanya kazi kubwa ya kujenga chama chetu tunakushukuru sana na tunakutakia maisha mema. Mwaka huu mission ya Watanzania ni kuitoa CCM , tunasikitika sana kukukosa binafsi nitakukumbuka daima.Kwa heri Dr Slaa karibu Lowassa.

Dr Slaa amekuwa nguzo muhimu kwa umahiri na ustahimili wa CDM, amekuwa mlezi na mkuzi wa siasa za mageuzi hasa ndani ya chama. Natamani ningepewa dakika zangu tano kabla hujafika Serena ili niweze kugeuza hali.

Najua upo consistence na mambo mengi ila hili wananchi wanataka kuitoa ccm kwanza wanataka shetani huyu wa miguu tisa atoke.

Wote tunajua mgombea wetu alivyo ila kwa hapa tulipo hatuna jinsi tena ni ama yeye au zimwi lituuwe.

Saul alitumiwa na Mungu kuwaokoa waumini wa Mwenyezi Mungu pamoja na kwamba alikuwa akiwauwa. Kuna wakati Mungu anatuletea mkombozi asiye sifa zote ila anaonyesha ukuu na kujizihir=sha kwetu.

Nawe Gwajima umekosa sifa za uaskofu na uomgozi wa kiroho vua joho njoo kwenye siasa umekosa busara huwezi kufanya roho za watu kuwa udalali. Muumini wako alitegemea ungekuwa na kifua cha msitiri ila umeshindwa tatizo sio Dr Slaa ni kila muumini aliyekufunulia maisha yake je iko siku akikuudhi utamwanika hadharani, ndio maana nimeelewa madhebu mengi hayaruhusu makasisi wao kuwa wana siasa. Inatusha kuchanganya haya mawili.

leo tunajua Dr alikuomba chumvi, leo tunajua Mshumbushi huwa anampiga Dr hii ni mbaya sana.

Kwa heri Dr Slaa karibu Lowassa.

Pamoja na yote yaliyotokea nitaendelea kutegemea baada ya october siku moja Dr Slaa atarudi kufanya kazi na sisi atarudi Chadema na kuwa mwenyeiti atakuwa mbele na kuishi nasi.

Inawezekana vizuri, leo Mbatia na Marando ni washikaji, Chadema na Lowassa ni washirika, Chadema na CUF ni chama kimoja, Lowasa na Sumayi wapo gari moja jukwaa moja.

Hakuna uadui wa kudumu kwenye siasa, wala rafiki wa kudumu ni wakati tu.

Nenda Dr pumzika imetosha kushambulia wote wekeni silaha chini tumtoe nduli CCM. Tumewasikia wote ila malumbano haya hayatusadii kwa sasa hatuwezi badili mgombea na hatuwezi rudisha ccm october GEAR imebadilika angani na nyingine ardhini - sisi wa angani tunatua magogoni hakuna jinsi.

Pole Dr Slaa na pole wote mlioathirika na tetemeko. Twendeni ikulu kwa pamoja twendeni ikulu haraka.

Dr SLaa naoma itoshe baba naomba utulie tunakupenda sana na tunakuthamini mno ni pengo kubwa sana CDM kukosa hasa wakati huu.

Tumesikia yote tutayafanyia kazi.

Gwajima tulia imetosha hatutaki tena habari za chumbani imetosha. Sasa tweneni kwa wananchi tupige kazi .

Kura zaidi, ushindi mkubwa - Mabadiliko yanakuja byee byee CCM Byeee Byeee mafisadi.
Cahdema tuna toa toba ya kweli njoo utubu njoo utakaswe.

Kura yako october 25 ni CDM ni Ukawa
 
Mungu anaipenda sana nchi hii ya Tanzania. kwa kutufunulia na kutonesha tusiyo ya jua wala kuyazania. watu wa aina ya gwajima kuwa ndio washauri wa viongozi tulio wa amini na tunaoendelea kuwa amini. eti gwajima ni moja wa washauri wa kiroho na kisiasa wa ukawa, kumchagua mgombea urais wa ukawa ni kuchezea shilingi jirani na tundu la choo.
 
Mkwawa

Mwenzako ameenda kula kuku na bata wewe bado unafikiri atakuwa mwenyekiti! Thubutu. Labda mwenyekiti wa bodi ya shule.
 
Last edited by a moderator:
Mkwawa,ninadhani hapa umemiss point. Gwajima amesemwa na mshirika wake kwamba ni mshenga na mambo mengine mengine mengi tu zikiwemo tuhuma za fedha .

Slaa alihitimisha kwamba wote aliowataja hapo juu wajitokeza wajibu hoja zake. Kitu ambacho kwangu nilikiona na tabia za kishangingi, za kulazimisha mtu atoke hadhaani msutane. Mambo ya kike kike sana yasiyo na mshiko.

Gwajima katoka kujibu kama alivyotakiwa na Slaa. Hapa hutakiwi kumlaumu Gwajima, ulitakiwa uwalaumu anaconda na ccm waliomtuma Slaa aongee ujjinga huku wakijua siyo kweli.

Gwajima hata siku moja hayaongea masuala yaliyofanyika kwenye confessions. Aliyoyaongea na maisha ya nje sana ya kawaida ambayo tena bila Slaa kushurutisha asingeyasema vinginevyo angeyasema awali.

Gwajima ameruka na kuficha maswala mengi sana ambayo hakushurutishwa kuyasema na Slaa.

Gwajima kamtetea sana Dr. Slaa kama umemwelewa.

Amesema siyo yeye.

Tatizo ni yule mwanamke aliyenaye ambaye amejaa ubinafsi ushamba na ushetani.

Tatizo liko kwa yule mwanamke kujaa ukatili na abuse kwa mmewe ambaye haihitaji Gwajima kufahamu ni old and naive kwenye maswala ya mahusiano.

Tatizo liko kwa yule mwanamke na ccm kum isolate na kum humiliate Slaa kiasi cha kumchagulia watu wa kuongea nao, kumfungia Serena hotel na kuzidi ku brain wash.

ULITAKIWA UWAONYE CCM NA ANACONDA waache siasa za mauaji.

HAKI ZA BINADAMU WANATAKIWA WASIMAME KUMTETEA DR. SLAA AMBAYE NINAONA MAISHA YAKE YAKO HATARINI.

DR AMETENGWA NA KUKAMATWA KAMA MATEKA MSUKULE NAYEYE BILA KUJITAMBUA KWAMBA ANAKUWA ABUSED.

KAMA WALITAKA GWAJIMA ASIZUNGUMZE NA KUWAMULIKIA WATANZANIA TATIZO KUBWA LA SONGOMBINGO LA SLAA NI ANAKONDA, WASINGEMWINGIZA KWENYE FAKE SCRIPT YA SLAA NA KUTAKA ATOKE AJIBU.

KAJIBU SASA TENA MNALALAMIKA LINI? AU MLITAKA MATUSI YA SLAA YABAKI KU SUFFICE KAMA KITU CHA KWELI NA CHA NGUVU KATIKA HALI HIYO?

SLAA ANHITAJI MAOMBI YA KUFUNGULIWA. NINA MASHAKA SANA NA HATIMA YAKE.
 
Hata mfanyeje CCM mbele kwa mbele. UKAWA mtaishia kuwa waigizaji tu. Tarehe 25 Oktoba mtaisoma namba mtabaki kuwa wakiwa tu. Nyie porojo tu vitendo hakuna. Mnachonga sana poleni. Nawasihi mje mkubali matokeo msilete vurugu.
 
Hata mfanyeje CCM mbele kwa mbele. UKAWA mtaishia kuwa waigizaji tu. Tarehe 25 Oktoba mtaisoma namba mtabaki kuwa wakiwa tu. Nyie porojo tu vitendo hakuna. Mnachonga sana poleni. Nawasihi mje mkubali matokeo msilete vurugu.

Niko na wasiwasi na uwezo wako wa akili!! Ebu pata muda wa kujitafakari vizuri...
 
Sawa andika utakavyo. Kashifu uwezavyo ila ujue ukweli utaupata hiyo siku itakapofika. Hebu jaribu kuwaza kwa kina usichukulie mambo juu juu. Jaribu kutafakari kabla hujatoa jibu lisilokuwa na mashiko
 
Hivi mnaamini mkakati wa kumleta Lowasa uchorwe na Slaa (bila Mkwe kujua) alafu ghafla awageuke wenzake sababu ya mkewe? Akina Ndesamburo kuonekana kwa Slaa walikwenda kumbembeleza Josephine? ....mbona tunashindwa kutumia akili ndogo tu kujua hizi propaganda za kitoto ...masharti aliyoweka Slaa ili kumpitisha EL yako wazi na kama yangetimizwa then bado Slaa akagoma tungejua kweli kulikuwa na influence. Mtu kaweka masharti muhimu ya kimaadili mkayapuuza baadae mnamtumia mkewe kumchafua ....
 
Inaonesha (fikra zangu) baada ya kushindwa kumshawishi Slaa ukatengenezwa mkakati wa kutafuta ushahidi wa kuaminisha watu kuwa tatizo la Slaa si kusimamia kanuni na maadili bali mkewe ....hapa mtumishi wa Mungu kwa nafasi yake akatumika kuchota madhaifu ya Josephine (anayo kama wanadamu wengine) na kumrekodi ili watu waamini wanayoaminishwa sasa .....siasa hizi ....
 
Inaonesha (fikra zangu) baada ya kushindwa kumshawishi Slaa ukatengenezwa mkakati wa kutafuta ushahidi wa kuaminisha watu kuwa tatizo la Slaa si kusimamia kanuni na maadili bali mkewe ....hapa mtumishi wa Mungu kwa nafasi yake akatumika kuchota madhaifu ya Josephine (anayo kama wanadamu wengine) na kumrekodi ili watu waamini wanayoaminishwa sasa .....siasa hizi ....

Kweli kabisa.

Ilijulikana wazi kuwa Lowassa hawezi kugombea kupitia Chadema pasipo Silaa kuondolewa.

Lissu na Mbatia walishathibitisha kwa wanahabari kuwa Silaa alishapitishwa na Kamati Kuu ya Chadema tangu April 2015.
Hivyo ilikuwa lazima Silaa atoswe..ama kwa hiari au lazima.
Na akawekwa chini ya Ulinzi wa Askari wa Gwajima asitoke hadi baada ya Lowassa kurudisha fomu.

Taarifa ya mlinzi inaonyesha Josephine hakumteka Silaa ndani kwa wiki kadhaa...alikuwa akitoka na kumwacha na walinzi wa Gwajima..lakini Silaa alikuwa havuki geti wala hatapati wageni wasioruhusiwa na walinzi hao.

Ilibidi Silaa "apigwe pini" na "afumbwe mdomo" ili asiharibu "matumaini" katika "safari" ya watu.
 
Mungu anaipenda sana nchi hii ya Tanzania. kwa kutufunulia na kutonesha tusiyo ya jua wala kuyazania. watu wa aina ya gwajima kuwa ndio washauri wa viongozi tulio wa amini na tunaoendelea kuwa amini. eti gwajima ni moja wa washauri wa kiroho na kisiasa wa ukawa, kumchagua mgombea urais wa ukawa ni kuchezea shilingi jirani na tundu la choo.
We unaambiwa baridi ikija vaa koti lakini kwa kichwa chako kigumu unavaa koti ili baridi ije. Tafakari chukua hatua. Huu ni wakati wa mabadiliko, vaa gwanda, wee umekalia kuvaa kijani ili mabadiliko yaje, utasubiri sana.
 
Back
Top Bottom