Kwa haya waliyofanya CHADEMA leo hii hapa MASASI ni funika BOVU.........

Kwani watanzania wengi si mnapenda kukaa bar kuwavizia mafisadi wawadanganye na chupa mojamoja, mkirudi mmeridhikaaa. Ulitaka wafunge Misikiti uanze kuandamana na kuchoma makanisa. Ondoa Utapiamlo wako hapa

Mafisadi wanatoka wapi kama si serikalini? Je, serikali inaongozwa na chama gani? Ukitambua hilo nafikiri utakuwa umesha jijibu mwenyewe pamoja na familia ya vipofu wenzako.
 
Baa zote zilifungwa na shughuli zote katika Wilaya ya Masasi zilisimamishwa muda kutokana na Mkutano wa Chadema aliokuwa ukifanyika katika ya Wilaya ya Masasi siku ya tarehe 3 - Mei - 2012.

Hii inaashiria ya kwamba CCM Mwaka 2015 hawatakuwa na nafasi tena kuongoza nchii yenye hali mbaya kiuchumi. Kwa kweli watu wamehamasika sana kuhusu maelezo yaliyokuwa yanatolewa na viongozi wa Chadema.

Peoplesssssssssssssssss Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeerrr.

Wananchi wamedanganywa vya kutosha. Kilichobaki ni kuwaadhibu ccm kupitia kwenye sanduku la kura 2015.
 
Nakubaliana na wewe kuwa mwamko wa wananchi kwa sasa ni mkubwa sana katika masuala ya siasa. Hata hivyo wakati haya yanatokea ni vyema tukajifunzo kutokana na makosa yaliyopita ambapo kuna baadhi ya viongozi waliamini kuhudhuriwa kwa mikutano yao na watu wengi ni mafanikio na baadaye kuja kubainika siyo hasa baada ya kura. Ili kuwezesha mageuzi ya kweli pamoja na kuelezea madhambi ya magamba, vyama vya upizani vielimishe vijana kujiandikisha kupiga kura bila hivyo hakuna ushindi. Nasema vijana kwa kuwa naelewa fika mapinduzi ya kweli yapo kwa vijana hao ndio watakaowezesha ushindi kwa upande wowote ule. Kwa hiyo wito wangu pamoja na mambo mengine hakikisheni vijana wake kwa waume wanahamasishwa kujiandikisha kupiga kura.

Toa maoni yako kuhusu jinsi ya kuzuia uchakachuaji matokeo usijifanye hujui kilichofanywa na tume ya uchakachuaji!!!
 
Back
Top Bottom