Kwa haya waliyofanya CHADEMA leo hii hapa MASASI ni funika BOVU......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa haya waliyofanya CHADEMA leo hii hapa MASASI ni funika BOVU.........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mzee wa njaa, Jun 4, 2012.

 1. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Baa zote zilifungwa na shughuli zote katika Wilaya ya Masasi zilisimamishwa muda kutokana na Mkutano wa Chadema aliokuwa ukifanyika katika ya Wilaya ya Masasi siku ya tarehe 3 - Mei - 2012.

  Hii inaashiria ya kwamba CCM Mwaka 2015 hawatakuwa na nafasi tena kuongoza nchii yenye hali mbaya kiuchumi. Kwa kweli watu wamehamasika sana kuhusu maelezo yaliyokuwa yanatolewa na viongozi wa Chadema.

  Peoplesssssssssssssssss Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeerrr.
   
 2. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pichaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 3. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hizi ni habari njema kwangu
   
 4. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka sikuwa na Camera ngoja nizitafute nitakuwekea tu.
   
 5. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nani walikuwepo na waliongelea nini mkuu na tulio mbali tufaidi.
   
 6. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu fanya editing kidogo kwenye post yako ya kwanza. Sema ni jana Jumapili na si leo Jumatatu tayari. Pia tarehe si 3 Mei 2012 bali ni 3 Juni 2012.
  Asante.
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Baa zote zimefungwa, kweli chadema inapendwa.
   
 8. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,647
  Likes Received: 5,240
  Trophy Points: 280
  hudhuria kwenye Maktaba ya Taifa.
   
 9. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe kuwa mwamko wa wananchi kwa sasa ni mkubwa sana katika masuala ya siasa. Hata hivyo wakati haya yanatokea ni vyema tukajifunzo kutokana na makosa yaliyopita ambapo kuna baadhi ya viongozi waliamini kuhudhuriwa kwa mikutano yao na watu wengi ni mafanikio na baadaye kuja kubainika siyo hasa baada ya kura. Ili kuwezesha mageuzi ya kweli pamoja na kuelezea madhambi ya magamba, vyama vya upizani vielimishe vijana kujiandikisha kupiga kura bila hivyo hakuna ushindi. Nasema vijana kwa kuwa naelewa fika mapinduzi ya kweli yapo kwa vijana hao ndio watakaowezesha ushindi kwa upande wowote ule. Kwa hiyo wito wangu pamoja na mambo mengine hakikisheni vijana wake kwa waume wanahamasishwa kujiandikisha kupiga kura.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,784
  Trophy Points: 280
  Hizi ni habari njema kwa Watanzania maana CDM kinazidi kuthibitisha kwamba si chama cha Wachaga tu kama ambavyo magamba wanataka Watanzania waamini hivyo.
   
 11. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Ngoma inogile, Nape alikuwa Songea kujaribu bahati yake.
   
 12. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,792
  Likes Received: 3,879
  Trophy Points: 280
  Hapa ndipo watanzania wengi mnapokosea na kuwalaumu na kuwakatisha tamaa wapiga kura! kwenye chaguzi nyingi naweza kusema kuanzia 1995 hadi sasa wananchi waliunga mkono upinzani kuanzia kwenye mikutano hadi kwenye sanduku la kura! walipokosea au tuseme walipojisahau ni kutokulinda kura zao!Waliiamini sana tume ya uchaguzi bila kujua ni taasisi ya CCM! Hii imedhihirka kwenye uchaguzi wa 2010 maeneo ambayo watu waliibana tume kama Arusha, nyamagana,ilemela, Iringa mjini na juzijuzi Arumeru mashariki CCM ilishindwa! Kwa hiyo kwenye hizi kampeni za M4C wananchi waelezwe wazi kuwa wanatakiwa washiriki kampeni, wakapige kura na kuzilinda hadi matokeo yatangazwe!!
   
 13. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  habari njema hizi
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Nape,rejao,ritz machozi yanawa dondoka
   
 15. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...umenena yaliyo ya kweli...sina cha kuongeza coz ukweli u-simama wenyewe!...
   
 16. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwani watanzania wengi si mnapenda kukaa bar kuwavizia mafisadi wawadanganye na chupa mojamoja, mkirudi mmeridhikaaa. Ulitaka wafunge Misikiti uanze kuandamana na kuchoma makanisa. Ondoa Utapiamlo wako hapa
   
 17. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,060
  Likes Received: 6,508
  Trophy Points: 280
  Tena CDM wamechelewa sana kwenda huko,
  kule wamesahaulika kabisa, utajua kuwa siyo TZ.
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Baada ya M4C kueleweka sasa ni wajibu wa kila mzalendo kulinda kura 2015.
   
 19. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Pamoja na hilo, tupiganie kupata tume huru ya uchaguzi itakayoendesha na kusimamia uchaguzi huru na wa haki mwaka 2015 bila maagizo toka ikulu, uwt au ccm makao makuu.
   
 20. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Lini hiyo?
   
Loading...