Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,603
- 29,747
Lissu yupo Zanzibar kusaka kura za urais wa Jamhuri.
Nimeanza na dibaji hiyo kwa minajili ya kusema yafuatayo:
1. Katika kunadi sera zake na ahadi za mgombea wa Urais hajawahi kuzungumzia namna atakavyolinda na kuuenzi Muungano ulioasisiwa na mababa wa mataifa ya Tanganyika na Zanzibar.
2. Akiwa Bungeni, Mhe. Lissu aliwahi kuzungumzia Muungano akionyesha kutoukubali na utayari wa kuuvunja.
3. CHADEMA katika harakati zake inakwepa kujadili Muungano wetu.
4. Hawajaweka mgombea wa urais wa Zanzibar na wametangaza kumuunga mkono Maalim Seif ambaye siku zote amekuwa akidai Muungano hauna manufaa na akiupata urais wa Zanzibar atavunja Muingano huo.
Hivyo, endapo Lissu atashinda Bara na Maalim akashinda visiwani basi meza ya muungano itapinduliwa kirahisi kifuta historia tukuka ya Muungano na mshikamano wa kitaifa.
5. CHADEMA haikutangaza awali kumuunga mkono Maalim Seif hapo awali lakini baada ya Seif kuhamasisha wafuasi wake kubeba majambia, mashoka na mundu ili kuleta machafuko, hatua hiyo imeipelekea CHADEMA kuona wamepata mshirika anayeendana na malengo yao.
Ikumbukwe CHADEMA ilipozindua kampeni zake pale Zakhiem ilitangaza maandamano ya nchi mzima kipindi hiki kwa minajili ya kushinikiza hoja zao na kuleta machafuko nchini.
Kwa sababu hii na nyinginezo inapelekea allegations za CHADEMA kujiandaa kuvunja Muungano wetu tukuka.
Hivyo, sisi wapigakura tunajua nini cha kufanya hapo Oktoba 28 ili kuulinda na kuuenzi Muungano wetu.
Msanii JF