Kwa fursa hizi kwanini huna hela?

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Ni maajabu sana mtu kukosa hela! Na ni ujinga uliokomaa!

Binadamu wana mahitaji mengi sana.Fursa ni kemkem kila mahali na kila sekunde iendayo kwa MUNGU.

1. Umeshindwa kufuga?

2. Umeshindwa kulima?

3. Umeshindwa kuwa 'broker'?

4. Umeahindwa kuuza mkaa?

5. Umeshindwa kuuza vyakula?

6. Umeshindwa kuosha magari?

7. Umeshindwa kufanya collabo na mwenzio mwenye biashara?

8. Umeshindwa kuuza samaki nyama au dagaa?

9. Umeshindwa kufungua kijiwe cha kuziba pancha?

10. Umeshindwa kabisa kuoa au kuolewa na mtu mwenye pesa?

11. Umeshindwa kuuza nguo?

12. Umeshindwa hata kufungua saloon?

13. Umeshindwa kuuza mbogamboga na matunda?

14. Umeshindwa kuuza chakula?

15. Umeshindwa kabisa kumkopa mwenzio na kuanza biashara yako?

Sasa kama huna hela unaishi duniani ili iwe nini?

Maajabu sana!
 
Naona unamradi na salary slip Dat so unadhani ni simple kufanikiwa.
Huku kwetu ukitaka mkopo wa ten% kutoka halmashauri unaulizwa kwanza
UNA KADI YA CHAMA?
noma tupuu yaan.......
 
Unajaua watu wote walio makazini au wenye uwezo uwaona wenzao kitaani kama mafala hivii. Hili ndo tatizo kubwa tulilonalo kama nchi. Hivi unajua kuna watu wanakaa mwezi ajashika buku 10? Unajua kuna watu wanakula mlo mmoja??
point yako Ni ipi sasa hapo?
 
Hivi punde,
Mkuu,
Kama una nafasi ya kujipatia kipato mshukuru Mola.

Kisha, waombee wasio na kitu nao wapate.

Hakuna mwanadamu anyefurahia kuteseka au kukosa kipato ...

Kukosa ajira au kipato kusikie tu kwa jirani yako , na Omba yasikukute.
kwa hyo mtoa mada kakosea kutoa maoni kuhusu fursa alizoziona?
 
Ni maajabu sana mtu kukosa hela! Na ni ujinga uliokomaa!

Binadamu wana mahitaji mengi sana.Fursa ni kemkem kila mahali na kila sekunde iendayo kwa MUNGU.

1. Umeshindwa kufuga?

2. Umeshindwa kulima?

3. Umeshindwa kuwa 'broker'?

4. Umeahindwa kuuza mkaa?

5. Umeshindwa kuuza vyakula?

6. Umeshindwa kuosha magari?

7. Umeshindwa kufanya collabo na mwenzio mwenye biashara?

8. Umeshindwa kuuza samaki nyama au dagaa?

9. Umeshindwa kufungua kijiwe cha kuziba pancha?

10. Umeshindwa kabisa kuoa au kuolewa na mtu mwenye pesa?

11. Umeshindwa kuuza nguo?

12. Umeshindwa hata kufungua saloon?

13. Umeshindwa kuuza mbogamboga na matunda?

14. Umeshindwa kuuza chakula?

15. Umeshindwa kabisa kumkopa mwenzio na kuanza biashara yako?

Sasa kama huna hela unaishi duniani ili iwe nini?

Maajabu sana!
mkuu umeongea ukweli ila sema wanakuzonga kwa sababu Kuna maneno yanaudhi
 
Watu wengi wana business idea ila hawana mitaji.
Lakini kwa baadhi ya fursa zilizoorodheshwa hapo hazihitaji mtaji mkubwa wa kutisha, tatizo watu wengi tunapenda kazi/shughuli za kufanya huku tumevaa tai. Hizi nyingine tunaona aibu kuzifanya.

Wito wangu kwa wasakatoge wenzangu, 'ukitaka kufanikiwa idharau aibu'
 
nalo neno ngoja nifuge kuku ,tatizo ktk maisha hakuna kutumia logarithm
 
Back
Top Bottom