Kwa CCM kauli ya ‘ushindi ni lazima’ inaakisi yafanyikayo

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
Kuna kipindi kauli ya CCM iliyokuwa inasema ‘ushindi ni lazima’ ilikuwa inapigwa vita na wapinzani na kuonekana imejaa nia ovu. Kushindwa kuitafsiri kauli kama ile kwa kuangalia ukweli ulivyo ndicho kilichofanya wapinzani wapinge kauli hiyo iliyokuwa na kila sifa ya ukweli na iliyotathminiwa kutokana na yaliyofanyika. Inawezekana ilipingwa kwa sababu waliyoipinga walijiweka katika mizani sawa ya kujilinganisha na CCM kiuwezo lakini ukweli ukaja kujulikana kuwa hakika ‘ushindi ni lazima’

Leo hii kauli hiyo ya ushindi ni lazima ikitamkwa wa kuipinga labda waamue kupinga kila ukweli. Kila kinachofanywa na CCM katika awamu kinaonekana kwa watanzania. Kuna kila sababu ya CCM kusema ushindi ni lazima kwa sababu imefanikiwa kushindana na matatizo sugu ya watanzania. Leo serikali ya CCM inatembea kifua mbele kwa kufanikiwa kufanya vita na ina kila sababu ya kusema USHINDI NI LAZIMA.

Ikumbukwe vema, wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015 watanzania walipigia kura chama chenye ilani na sera nzuri. Pengine ulikuwa ni uchaguzi mgumu kwa CCM lakini watanzania walikipa ushindi na ndipo tunajivunia kusema kwa CCM ushindi ni lazima kwa sababu tuna sera na ilani ya kutufanya tushinde licha ya magumu tunayopitia.

Leo , kauli hiyo ya ushindi ni lazima tunaitangaza na kuisema kwa kujivunia na kwa sauti kubwa kutokana na viongozi waliopo ndani ya CCM kuanzia kwa mwenyekiti wa CCM taifa mpaka kwenye shina. Mwenyekiti wa CCM taifa ambaye pia ni Rais wa Tanzania anafanya mambo ya kuendelea kujivunia kauli hii kwa wanachama na watanzania.

Ilani ya CCM ambayo ilitoa matumaini kwa watanzania leo inatekelezwa kwa kiwango na uwezo mkubwa na matunda yake kuonekana, ni matunda ya ushindi wa CCM na watanzania wote. Utekelezaji wa ilani kwa kiwango hiki kikubwa na matunda ya utekelezaji kuwa ya watanzania wote inaakisi kauli ya ushindi ni lazima.

Kauli ya ushindi ni lazima leo imefanyika kuwa ya kweli na uhalisia wake kuonekana baina ya watanzania karibu wote. Leo hakuna siasa yeyote ndani ya kauli hiyo kwa sababu matokeo yanaonekana kupitia mafanikio ya awamu hii. CCM ushindi ni lazima kwa sababu haijawahi kushindwa.
 
Back
Top Bottom