Mimi binafsi nakubaliana na Mhe. Magufuli kuhusiana na mchanga wa dhahabu unaosafirishwa nje ya nchi. Tunaelezwa kuwa concentrates iliyomo ndani ya mchanga huo ni 0.02 % ya madini mbalimbali ambao kwangu nasema ni UONGO MTUPU. Iweje mchanga huo utolewe Bulyangulu au Geita kwa usafiri mpaka Bandari ya Dar es Salaam halafu usafirishwe kwa meli mpaka aidha Japan, China, Ujerumani na hatimaye kusafishwa kwenye viwanda kwa gharama kubwa kuanzia usafirishaji mpaka usafishaji kwa mchanganyiko wa 0.02% tu?. Hii ni hapana. Pili huko kwenye viwanda wanaposafishia je kuna mwakilishi wetu anayetupa mrejesho kwa kilichopatika baada ya usafishaji?.Ieleweke kuwa kazi hii anaifanya mzungu, kwa uelewa wangu mzungu alivyo maakini hawezi kufanya kazi ya hasara mpaka kuwe na faida. Ushauri wangu kwa Mhe.Magufuli ni kama ifuatavyo:- (1) Kamata watumishi wote waliosimamia mikataba hii bila kumwonea mtu huruma wakueleze walikuwa na maana gani kuhusu usafirishaji wa mchanga wa dhahabu. Bila maelezo ya kina wafikishwe mbele ya sheria. Tatu, Mimi nakushauri Mhe, Rais acha hasira. Wewe ndiyo Baba yetu. Yeyote akikosa chukua muda kutafakari, omba ushauri kwa vyombo vyako unavyoviamini, Mkae na Katibu Mkuu Kiongozi mshauriane. Kutumbuliwa hii huku mitaani inatutisha na inawafanya wenzako wafanye kazi kwa woga japo wanaweza kuwa na jambo zuri la kukueleza. Nakutakia kazi njema katika kutuongoza sisi Watanzania.