Ni hivi; miaka ile ya 1970 wakati Amin alipoipindua serikali ya Obote na Obote kukimbilia Tz. Idi Amin aliichukia nchi yetu sana. Na ktk hilo vijineno vingi sana vilikuwa vikirushwa kati ya watawala hawa wawili, yaani Nyerere na Amin. Chuki hizi zilipelekea vamizi kuu mbili toka Uganda. Katika mojawapo wa vijineno vilikuwa hivi, "Nyerere wewe ni mzuri sana ungelikuwa mwanamke ningelikuoa" Amin huyo. Naye Nyerere alijibu hivi, ' Amin Dada...' Kuanzia hapo tukaanza kumwita kwa jina la Dadaa. Kuna majina mengine kama nduli, joka, nk.