Basi katika pita pita zangu.... nikakumbana na hii story yaweza isiwe ya kweli... lakini kuna funzo twaweza kujifunza.... jamaa mmoja baada ya kusikia stori kuwa muda mrefu wife ake anatembea na ka chalii kamoja kasikokuwa na mbele wala nyuma,(yaan hakana kazi wala hirizi ya kidhungu) akaamua siku hiyo akahakikishe kama ni kweli.... lakini kabla ya kufanya hivyo akaamua kupata ushauri kutoka kwa rafiki yake kipenzi kuwa endapo atakuta ni kweli mkewe anavunja amri ya sita afanyeje....? basi jamaa akamushauri amuone amwasaikolojia wa masuala ya mahusiano ili amujenge kisaikolojia kabla ya fumanizi lake....
Basi akaamua kwenda kumuona mwanasaikolojia maarufu hapa jijini.... baada ya kusikliza maelezo ya jamaa kwa makini mwanasikolojia yule akamushauri kesho yake aende na mkewe ofisin pale... bas bwana kesho yake jamaa akafika ofisini pale akiwa ameambatana na mkewe kipenzi.... bas mwanasaikolojia akaomba aongee na mke wa jamaa faragha...
Docta: wanandoa wengi wamekuwa hawafurahii ndoa zao, hasa wawapo faragha.... kutokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali ambazo zinaweza kupelekea mmoja wapo kuanzisha mahusiano nje ya ndoa.... sasa mama wewe na mmeo manaishije.....?
Mama: yaan docta bila kukuficha mume wangu haniridhishagi kabisa.. yaan yeye huwaga anapaparuka tuu....akishamaliza shida zake analala kama gogo mpaka asubuhi.... hajali kabisa wenzake.... yaani hakuna maandalizi anayo yafanyaga kabla ya kuingia faragha.....
Docta: sasa mama uliwahi kumwambia lakini.... kwa sababu pengine yeye hajui hili...
Mama: nimwambie mara ngapi.... mtu mwenyewe ukimwambia visingizio kibao... mara ooh amechoka, mara ooh...majukumu mengi ooh nini... yaani mambo mengi... me nimeshindwa kuvumila kwa kweli.... ataweza wapi mtu mwenyewe kurudi sa7u amelewa chakarii.. akifika ni kulala kama gogo.... loo! acha watumie wengine.... sasa yeye si kashindwa acha wamsaidie... mtu mwenyewe yule stail ile ile kila siku.... hakuna cha uwanja wa ugenini.... yeye kila siku uwanja uleule mechi yenyewe dakika tatu.....kwisha akhaa....
Bas mtalamu yule akataka kusika upande wa pili wa shilingi... yaani kutoka kwa jamaa mambo yalikuwa hivi nanukuu "mke wangu ni mchafu sana, yaani yeye kila dakika ni kujipoda tuu... nilishamwambia mimi sitaki hayo makorokoro yake sijui waita wigi., mara malashi makali.... yaani yeye akiamuka asubuhi ni kwenda salon kuset nywele, kujipodoa... ndani kuchafu, shuka chafu, kitanda hakijatandikwa... vyombo vichafu vyote... yaan mambo yake bwana... anajijali yeye tuu watoto wangu ukiwaona utashangaa yaan wamechakaa.. kila siku naacha pesa ya kutosha... kila weekend nawanunulia wanangu nguo, viatu na kila kitu.... sasa yeye hata wakichafua nguo, hafui, hawaoshi yaani wakati mwingine bwana daktari naona aibu hata kuja na rafiki zangu yaani.... naamua wakati mwingine nikae tu baa ninyweee... nikifika ninale asubuhi niondoke zangu...yaani huwaga nakuangalia kenye tv unavyo tuhimiza kuwapenda wake zetu yaan huwa nakushangaa naona kama unapoteza mda vile.... yaan kwangu hakuna aman kabisa..."
basi mtaalamu yule akaamua kuwaketisha pamoja, kuwashauri, na hatimaye kila mmoja akakiri kosa lake na kuhaidi kujirekebisha...PLZ KUNA WATU WANATARAJIA KUINGIA HUKO KWENYE NDOA ZINGATIENI HAYA.... nawatakia kila lakheri....