Kupata shule ya kuanza kusoma form 5 ni suala dogo,Shule nyingi atakazoomba ajiunge na form 5 atapata,ila watamuuliza ana plani gani ya kuziba hilo pengo la credit moja ili aweze kukubaliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita.
Kwa kuokoa mda watu wengi huwa WANAJITOA SADAKA,yaani anaanza kidato cha tano huku amejiandikisha kujiangaa kurudia mtihani wa kidato cha nne,Akifaulu na kupata hiyo "credit" ktk huo mtihani wa kidato cha nne aliourudia basi ni SALAMA yake,maana kikifika kipindi cha kujaza fomu za kuomba kufanya mtihani wa kidato cha sita atakubaliwa na atazijaza na zitapitishwa na BARAZA LA MITIHANI (NECTA).Ila kama akifeli na kutopata hiyo credit moja ktk huo mtihani wa kidato cha nne aliourudia,hapo HATOKUBALIWA KUJAZA FOMU ZA KUOMBA KUJIANDIKISHA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA,.na ikitokea wamejaza ki MAGUMASHI hapo shuleni kwake,basi kule Baraza la mtihani watagundua na hawatamkubalia ombi lake,HAWATAMPATIA NAMBA YA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA.Pia uwezekano wa kupata kesi ya ulaghai yaweza kumwandama.
Ila mara nyingi wanaojiandaa kurudia mtihani wa kidato cha nne ili kuzisaka credit zilizopungua huku wakisoma kidato cha tano huwa wanafaulu na kuzipata hizo credit kuliko kujiandaa wakati uko nyumbani.