Kwa Akili Yangu ya Wanzuki Nikafumaniwa Mchana Kweupe...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Akili Yangu ya Wanzuki Nikafumaniwa Mchana Kweupe...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 30, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Nilikuwa nina kama miezi mitatu tangu kuoa kwangu. Ilikuwa ni Juni 2005. Mke wangu alikuwa akiniamini sana na hata wazazi wake, hasa mama yake, kwani alinifundisha shule ya msingi, wakati akiwa mwalimu. Mwaka huo wa 2005 alishastaafu.

  Siku hiyo nilikuwa nyumbani na mke wangu alikuwa meenda kwao. Ilikuwa ni mapema bado, kama saa nane mchana, kwa hiyo sikutegemea angerudi wakati ule kwani tulikubaliana kwamba, angerudi jioni. Nilikuwa nimekaa sebuleni nikiangalia TV.

  Mara simu yangu ikaita. Nilipunguza sauti ya TV hadi ziro na kupokea simu. Ilikuwa inatoka kwa msichana ambaye nilikuwa nimeanza uhusiano naye kama mwezi mmoja nyuma. Ukweli hadi leo najiuliza niliweza vipi kufanya jambo kama lile, kwani sikuwa kabisa mpenda wanawake na nilikuwa pia naheshimu ndoa yangu.

  Nilipokea simu na kuanza kuzungumza naye. "Usijali mpenzi kesho nitakuona….. Nani, First Lady? Hana neno huyu na wala hawezi kunishtukia, kwani ananizimia sana. Nimemshika kwa kweli. Unajua nini, ulichelewa kidogo tu kujitokeza kwangu, lakini pale madhabahuni miezi mitatu iliyopita ungetakiwa kusimama wewe, siyo yeye……" Niliendelea kubwabwanya mwanaume na maneno yalikuwa yananitoka kama muimba taarabu wa mipasho.

  "Lakini hata hivyo halijaharibika neno. Huku nimefungwa pingu za kanisani, lakini moyo wangu uko kwako mpenzi. Nakuhakikishia kwamba, nikiwa nawe, kila kitu kinabadilika, kinakuwa supa mwanawane. Naanza kumchoka wife, kwani hata nikiwa naye naiona sura yako kwake…………" Nilihisi nywele zimenisimama kisogoni ikabidi ninyamaze na kugeuka nyuma.

  Nilishtuka kwa njia ambayo ingeweza hata kuniuwa kwa shinikizo.
  Nilimwona mke wangu na mama yake wakiwa wamesimama. Nilijifaragua kutaka kuwakaribisha lakini walivyokuwa wananitazama, mwenyewe nilinywea, sauti ikakauka. "Ulikuwa naongea na nani?" mke wangu aliniuliza .

  Nilibabaika kabla sijajibu……. "Ni …….ni… kuna jamaa yangu mmoja…." Sikumaliza kwani niliwashwa kibao cha maana shavuni na mke wangu.Halafu alinivaa na kunitupa chini. Nilikuwa sina nguvu kabisa, nilikuwa b.w.e.g.e hasa.

  Kweli kufumaniwa ni kubaya.
  Mama mkwe aliingilia kati kwa kuamua kumwondoa mwanaye ambaye alikuwa akinitandika kisawasawa pale chini. Wapangaji upande wa pili wa nyumba nao walifika na kutuamulia .Mama mkwe alimshika mkono bintiye na kumwambia, "twende, acha kila kitu humu ndani, usichukue chochote. Inatosha kwa haya tuliyoyaona."

  Waliondoka na bintiye wakiniacha pale chini nikijizoa zoa na kusimama huku nikipepesuka.
  Wapangaji wa nyumba upande wa pili walicheka kwa pamoja kicheko cha kebehi na kumalizia halo halooooo…..Walioneka wazi kufurahia dhahama ile, kwani tulikuwa tukiwasema sana mimi na mke wangu kwamba ndoa zao ni za kuunga kwa gundi.Najua mnataka kujua ilikuwaje baada ya pale………

  Acheni umbea, fanyeni kazi……………


  Lakini ngoja nikate kiu yenu ya umbea. Ni kwamba, baada ya pale, tuliyamaliza na mke wangu na alinisamehe baada ya kumweleza ukweli wote.

  Kusema kweli tangu siku hiyo nimebadilika sana. Nikiona mwanamke nisiyemjua ananichekea chekea na kujipendekeza kwangu…….. nafunga viatu vizuri na kutimua mbio…………..LOL

  Kuna watu najua wataninanga hapa kama nini…………………….!
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hii hainihusu mimi kabisaaaa.....................
   
 3. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Mie natakaa kukuuliza swali moja tu mzee Mtambuzi...vipi kile kichapo kutoka kwa mama ngina kilikuwa cha ukweli eeeee?
   
 4. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Unko duh! mungu atunusuru kumbe kufumaniwa kubaya sanaa? umetota uso ukawa mdogoooooooo! Lol.
   
 5. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,315
  Likes Received: 2,601
  Trophy Points: 280
  hilo hatuliiti fumanizi Mtambuzi, vijana huwa tunauita msala
   
 6. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Stori za kutunga hazifai hata kidogo bwana Mtambuzi!!!!
   
 7. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Hahaah lol
   
 8. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dah hilo ni soo. Pale nywele ziliposisimka kugeuka nyuma,,,, Mimi ningezimia! Hahaha! Aisee kucheat sio dili, ni upuuzi na ni kujitafutia magonjwa, laana!
   
 9. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Tunga na wewe mkuu.
   
 10. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,943
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  rafiki yangu mmoja mkubwa huliita VANGA
   
 11. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  dah...hatari hiyo kama ni kweli..
   
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Mama nae ana moyo, mmmh!
   
 13. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  mwanaume wa ukweli maishani mwako sharti ufumaniwe (angalao mara moja),sharti udaiwe (utaishije bila madeni?) na sharti ukumbwe na visanga (kufukuzwa kazi,kuibiwa,kudhulumiwa,kufumwa na hausgel etc),huo ndo uanaume na ukipitia visanga ndo unakomaa ati.
   
 14. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kweli ni akili ya wanzuki, changanya na mataputapu............
   
 15. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #15
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Unajishtukia nini Mtambuzi? Inakuhusu sana! Usianze kusingizia Jitambue.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  duuu mkuu bishanga hahahahah!
   
 17. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Aah! Nilikuwa sijaambiwa hili kwenye kitchen party.
   
 18. MMDAU

  MMDAU Member

  #18
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HAYA masimu tena sana sana haya ya kichina yametuharibia sana ndoa zetu pamoja na kutupotezea uaminifu
  ila mtambuzi ni kweli kichapo ulikisikia maana mm hata maumivu nisinge yasikia mbaya zaidi mama mkwe kashuhudia wapangaji nao. kama ni kweli basi mlihama pale hatakama kodi haijaisha kwani kila wapangaji wakikuona ungesilia

  "heheheheeeeeeeeeee halooooooooooooooooooooo halo ya mtambuzi ndani ya fumanizi"
   
 19. M

  Mhamashiru Member

  #19
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo umekutwa unaongea Je ungefumwa ndo uko....... kwenye majamboz!!! Kichapo kingekuwaje????
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,217
  Trophy Points: 280
  eri hata ulifumaniwa kwenye simu kuliko ungekutwa live.....
   
Loading...