GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Kuna siku huyu huyu Mpambe ( aide de camp ) wa Rais Magufuli alionekana akifanya kitendo kisicho cha KIMAADILI hasa kwa nafasi au kazi yake ambapo wakati Bosi wake amezungumza jambo ambalo liliwachekesha wahudhuriaji pale ukumbini kwa MAAJABU kabisa ya mwaka hata yeye pia bila kificho alionekana ANACHEKA japo ( kimtindo ) tukio ambalo lilileta ama kuzua mjadala mkubwa ambao sijui uliishaje.
Leo hii muda mfupi sana wakati Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli anazungumza tena akiwa na uhakika wote ULIOTUKUKA kama kawaida yake alitamka kuwa anatambua uwepo wa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam tena hadi akasema kuwa ni wa CHADEMA lakini kwa mshangao na aibu kubwa wakati Rais anageuka kumtizama huyo Mstahiki Meya huyu Mpambe wake alionekana wazi wazi akimwambia Rais tena kwa kumkatalia kuwa huyo Mstahiki Meya hayupo hapo eneo la tukio na kwa aibu kubwa Rais akamjibu kuwa nanukuu " Mstahiki Meya wa CHADEMA yupo hapa si yule pale...." nikamwona Mpambe wake ameshikwa na butwaa na akanywea kabisa.
Naomba kuuliza maswali kadhaa :
Na kwa wale ambao pengine wataona NIMEZUSHA tu hii kitu nawaombeni tafuteni FOOTAGE ya hii kitu ama kutoka AZAM TV au TBC1 muiangalie yote kisha hiyo sehemu ninayoizungumzia hapa mtaiona kisha mtajiridhisha.
Nawasilisha.......

- Hivi nani huwa anamchagua ADC ( Mpambe ) wa Rais wa nchi yetu?
- Kati ya Mpambe na Rais nani anatakiwa awe KNOWLEDGEABLE na SHARP kuliko mwenzake? ( namaanisha KIUTENDAJI wa KIKAZI au KIMAJUKUMU ya mazingira ya eneo husika ).
- Hivi ADC ( Mpambe ) wa Rais hawezi kubadilishwa kama akioneka ana UTENDAJI dhaifu?
- Kwanini huyu ADC ( Mpambe ) wa sasa wa Rais KIMWONEKANO tu anaoneka HAJIAMINI, HAKUANDALIWA na kama vile ni MGENI katika FANI hiyo?
- Kwanini huyu ADC ( Mpambe ) wa Rais wetu muda mwingi anaonekana ana hema juu juu na hayuko imara kimwonekano?
- Huwa inachukuwa muda gani labda kuwaandaa hawa ADC's ( Wapambe ) wa Marais ili wakianza Kazi zao hizi wasionekane kituko kama huyu wa sasa?
- Kwa aina hizi za UZEMBE anazozionyesha tena katika matukio muhimu kama haya kipi kinafanya hadi leo aendelee tu kubaki na Mheshimiwa Rais asibadilishiwe mwingine?