kiufupi mkuu mtu anaeweza kukudukua au kutrack mienendo yako ni mtaalamu wa hali ya juu, na duniani wanahesabika, si kitu rahisi.
kibongo bongo haya mambo yanafanyika kwa style hii
-kutumia wafanyakazi wasio waaminifu wa mitandao ya simu
-mtu kushika simu yako na kukuekea apps ambazo zitaku spy
-kutengeneza phishing websites, hizi ni website fake ambazo zipo kama original, na ukieka username na password wanaziiba na kukufuatilia.
mfano unakuta website halisi inaitwa jamiiforums.com mjanja anaweza tengeneza website inaitwa jamiforums.com (ameeka i moja), wewe bila kujua unaingiza username na password ya jamiiforums hapo ujue umeliwa na huyo mtu atapata details zako.
-apps mbali mbali ambazo umeziingiza mwenyewe kwenye simu zinaweza kuku spy
jinsi ya kujikinga,
-mitandao ya simu ifanye homework zao, kuhakikisha watumiaji wao wapo salama.
-hakikisha mtu hashiki simu yako ovyo ovyo na kukuekea vitu
-nenda setting kisha security kisha device adminisrator hapa by default kunatakiwa kuwe na device manager tu ukikuta kitu chengine usichokijua itoe
-kuna app inaitwa packet capture playstore idownload itakuonesha app zote za simu zinazotumia internet muda huo, angalia app gani usioijua inatumia internet kutoa na kupokea data
-tumia vpn mahala ambapo unataka wasikujue
-tumia adblocker, matangazo mengi yanakuwa ni virusi na spyware hasa website za ngono.
-usiingize username na password kwenye app zisizo official au website usiyoielewa,
na mengine wadau wataongezea