Kuzomewa na kukataliwa mkuu wa shule ni soni.

nkyandwale

Member
Feb 8, 2011
64
14
Ni jambo la kawaida kwa jamii ya kizazi hiki kumzomea kiongozi anayetoa hoja ambazo hazina mshiko na kujaa pumba kwao.

Hivi karibuni kiongozi, na mshika bango la elimu
aliipata homa ya zomeazomea na akatoa jasho hadi alitamani kufuta jasho kwa koti lake huko Dariasalama na aliondoka chuoni pale kwa ulinzi mkali
.

Kipigo na wembe ule ule umempata Mkuu wa shule ya sekondari x ambaye amepata uhamisho kwenda shule y katika manispaa ya Sumbawnga ailikataliwa na wanafunzi wa shule y mbele ya bodi ya shule. Wanafunzi hao walimzomea na kutamka
kuwa hawamtaki kwasababu shule yake ipo chini ya kiwango kitaaluma.

Kama haitoshi wale wanapokea amri na kutekeleza hawakusita kuwasambaza wanafunzi hawo kwa vitoa machozi na kamasi. Timu yetu inaendelea kufuatiliya hatima ya tukiyo hilo, kwani hayo yametokeya mnamo majira ya saa kumi na mbili jioni ya Ijumaa jana.

Enyi na wanazuoni na wanataaluma, kwa nini mnaendeleya kuwaweka kwapani wasiwo na uwezo wa kuyamudu madaraka? Fikiri tena!
 
Back
Top Bottom