kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,307
- 12,602
- Thread starter
- #21
Na huo mzunguuko Wa pili ni baada ya kupangiwa timu vibonde kama shelisheli, Djibouti, Comoro,Timu zetu mara nyingi sana zinaishia mzunguko wa pili katika mashinchindano tofauti kwa miangi sasa na hasa vilabu vyetu vya Simba na Yanga ambavyo vinapata hizo nafasi.
Kumekuwa na utamaduni wa kuzomeana kwa mashabiki wa Simba na Yanga pale mmojawapo anapokuwa anacheza mechi ya kimataifa uwanja wa taifa kiasi cha wageni kupata nguvu toka mashabiki wakati timu inatetea utaifa pale huo umekuwa ni ujinga unaofanywa kurudisha soka la tz nyuma.
Timu wageni huwa wanashangaa kabisa kushangiliwa na mashabiki wanapokuwa uwanja wa taifa kitu ambacho hawakipati nchi zingine zaidi ya wananchi wa nchi yao wanaoishi katika nchi hiyo wanaocheza kwa tz ni tofauti kabisa.
Mashabiki wa Simba na Yanga mjiangalie upya timu zenu zinapocheza uwanja wa taifa mechi za kimataifa...umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.