Kuzomeana kwa Simba na Yanga katika mechi za kimataifa hakuna faida zaidi ya hasara

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,313
12,613
Usipoutumia vizuri uwanja wako Wa nyumbani usitarajie muujiza ugenini.

Tabia ya mashabiki Wa yanga na Simba kushangilia wageni kwa nguvu zote kwenye mechi zetu za nyumbani inatufanya tushindwe kuvitumia vizuri viwanja vyetu kupata ushindi nyumbani.

Hakuna timu inayofaidika na tabia hii, ni vilio vya kupokezana tu kila siku.
 
Timu zetu mara nyingi sana zinaishia mzunguko wa pili katika mashinchindano tofauti kwa miangi sasa na hasa vilabu vyetu vya Simba na Yanga ambavyo vinapata hizo nafasi.

Kumekuwa na utamaduni wa kuzomeana kwa mashabiki wa Simba na Yanga pale mmojawapo anapokuwa anacheza mechi ya kimataifa uwanja wa taifa kiasi cha wageni kupata nguvu toka mashabiki wakati timu inatetea utaifa pale huo umekuwa ni ujinga unaofanywa kurudisha soka la tz nyuma.

Timu wageni huwa wanashangaa kabisa kushangiliwa na mashabiki wanapokuwa uwanja wa taifa kitu ambacho hawakipati nchi zingine zaidi ya wananchi wa nchi yao wanaoishi katika nchi hiyo wanaocheza kwa tz ni tofauti kabisa.

Mashabiki wa Simba na Yanga mjiangalie upya timu zenu zinapocheza uwanja wa taifa mechi za kimataifa...umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
 
tunakosa kupata timu mbilimbili za kutuwakilisha kwa sababu hii, hawa hawaishii kuzomeana tu, bali pia hata kuhujumiana
 
Tuache pia kutambiana na dharau zisizokua na maana! Mfano jana simba ingeshinda ungemsikia Manara akileta tambo za kijinga na dharau dhidi ya Yanga! Hii ndio husababisha kuzomeana na kushabikia wageni!
Na hizi kauli za kutaka muafaka nyingi zimekuja baada ya simba kutoka angeshinda matusi ya manara tungekosa pakuyaweka kwa kweli kuwaombea simba washindwe ile siku ilikuwa haiepukiki labda tuanze sasa kwa yanga kwenye shirikisho la hasha tuendelee na utamaduni huo huo mbovu
 
watanzania ndio tulivyo,
ebu angalia hata kwenye siasa ndio utapata jibu harisi.
Watu wanaichukia serikali wanaiombea mabaya yatokee hili wao wapate madaraka.
 
Na hizi kauli za kutaka muafaka nyingi zimekuja baada ya simba kutoka angeshinda matusi ya manara tungekosa pakuyaweka kwa kweli kuwaombea simba washindwe ile siku ilikuwa haiepukiki labda tuanze sasa kwa yanga kwenye shirikisho la hasha tuendelee na utamaduni huo huo mbovu
Yanga mlisema simba wasijipendekeze kuwashangilia mechi yao na township,mliamini mtashinda
 
Huko Spain mashabiki wa madrid kushabikia timu pinzani dhidi ya Barca ni jambo la kawaida saaana.

Timu za EPL zote hakuna hata moja zinazopendana, hata Barca alishabikiwa na Man U ampige Chelsea.

Tanzania mpira HAKUNA, kuna uchawi, majungu, kanunua mechi n.k
 
Basi tuendelee tu kama mbwai iwe mbwai mpaka tutakapoitisha mjadala wa kitaifa kujadili hili jambo
Tunatia aibu, wenzetu waliopiga hatua kisoka hawazomeani hata kama hawapendani.

Something must be done actively to stop this. Vinginevyo itabaki kuwa vicious cycle milele.

Kiongozi Wa Yanga alikuwa mpuu...zi alipompinga Manara lakini sidhani kama mashabiki wanatumwa na viongozi wao wazomee, hivyo sio Haji wala kiongozi Wa Yanga atakaezuia watu wasizomeane. Viongozi Wa matawi ya vilabu wanaweza angalau wakaisongeza mbele ajenda ya kuacha kuzomeana kuliko akina Manara.
 
Back
Top Bottom