four eyes
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 905
- 1,406
Nimekuwa nikijiuliza kuhusu huu utaratibu wa kutoa listi ya shule bora kimatokeo Kila matokeo yanapotoka harafu humo zinajumuishwa shule zote.
Humo utakuta shule kama kitonga imeshindanishwa na feza,St marrys imeshindanishwa na shule za kata nk,swali langu ni je hii ni sawa au Kuna Haja ya kutengenezwa category kama za kwenye tuzo mbalimbali ili kuweka uwanja sawa wa ushindani?
Hili nalisema nikisukumwa na ukweli kwamba shule kama feza haichukui tu Kila mwanafunzi Bali hufanya kwanza mchujo mkali wa kupata wanafunzi wenye uwezo mkubwa Kisha hao ndio husajiliwa shuleni hapo hii ni mfano wa usajili unaofanywa na timu kama man city,Madrid au Chelsea.
Utaratibu huu wa usajili hufanywa pia na shule kadhaa zinazotajwa mara Kwa mara ktk orodha za kuongoza kimatokeo Kwa kuchuja na kuchukua wanafunzi wenye uwezo wa juu na kuacha wale watakaoonekana hawana uwezo mkubwa.
Pili baada ya usahili huo kabambe kifuatacho huwa ni usajili ambao pia huwa Bila shaka unawahusu watoto kutoka ktk Familia zenye uwezo mkubwa kutokana na kiasi kikubwa cha ada inayotozwa hapo na mwanafunzi huwekwa ktk mazingira bora sana yanayomfanya kujenga utayari binafsi wa kupata elimu itakayotolewa ambayo pia huwa bora nahutolewa na waalimu wanaolipwa vizuri pia.
Hali huwa tofauti sana upande wa pili wa shule zetu za hali ya chini,usahili wake kwanza si mkali sana na hutoa fursa Kwa wanafunzi wengi kupata nafasi ya kusoma,lakini pia wengi wao hutoka Familia za chini kiuwezo na mazingira ya shule na nyumbani si mazuri,
Hata waalimu wao pia wengi hawana morali ya kufundisha badala yake huthamini tuition zao binafsi zaidi sababu ya mishahara midogo na mazingira mabovu ya kazi
Katika hali kama hii je? Ni sahihi Kwa shule za Aina hii kushindanishwa au zitengwe kama wasanii wanavyotengwa katika tuzo ili kuweka uwanja sawa wa ushindani?