Kuzidishiwa Pesa

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,829
2,387
Nimegundua nimezidishiwa pesa km laki 2, aidha benki au tigo pesa. Nahitaji kurejesha. Nitajuaje narejesha sehem sahihi? Nikitoa sadaka kimantiki itakuwa nimerudisha? Siamini katika pesa za hivi, nishaurini maana kuna familia ya mtu huenda ikataabika.
 
Mkuu nitumie mimi hilo fungu lininasue kwenye majanga.
 
We kaa nazo watafuatilia kwa mawakala waliokosea na zitarudishwa au utapewa maelekezo ya namna ya kuzirejesha.
 
Ukirudisha atakayezipokea anakupiga na makofi kwa kukuona mjinga
 
Ziache humohumo kwenye simu kampuni itazirejesha zilikokosewa kisha watakutaarifu
 
Mrejesho; Nimepita kwa jamaa wa Tigo Pesa, amesema yeye hesabu yake ipo sawa. Ninahisi ni NBC Bank nilipopita. Huko nitaenda kesho. Tamaa mbaya saana hawa watu wanaweza kutaabisha hata familia zako. Kwahiyo ni vyema kufikiria kama ingetokea kwako.......
 
Back
Top Bottom