Kuzidi kwa utegemezi kwenye familia zetu za Kibongo.

The iron batterfly

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Messages
1,902
Points
2,000

The iron batterfly

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2018
1,902 2,000
Habari za mchana wanaJf.Swaumu njema kwa walofunga na lunch njema kwa sie wa imani tofauti.

Iko hivi Kuna rafiki yangu,yeye alizaliwa peke yake upande wa mama yake,Baba yake alimwacha yeye na mamake angali akiwa tumboni kwa mama,so hana mahusiano na upande wa baba yake .Mama yake bahati mbaya alishafariki akiwa shule ya msingi,so kwa sehemu kubwa alilelewa na Bibi na Babu mzaa mama.Uzuri Babu yake alikuwa na ajira nzuri na Bibi alikuwa mjasiriamali mdogo.

Upande wa Bibi na Babu mzaa mama walijaliwa kuwa na watoto saba akiwemo mama yake huyu rafiki yangu.Bahati mbaya mama yake na nduguze wawili waliokuwa wanamsapoti nao walishatangulia mbele ya haki kitambo.Hivyo walibaki watoto wa 4 wa Babu na Bibi yake,wakike mmoja na wakiume wa 3,ambao kwa sehemu kubwa wote baada ya kumaliza elimu ya msingi walikataa kuendelea na masomo ingawa baba yao(Babu yake)alikuwa na uwezo wa kuwasomesha.

Hivyo kwa sehemu kubwa Bibi na Babu yake walijitahidi kumsomesha huyu mjukuu wao,kwakuwa alikuwa na Nia ya kusoma.Wakati watoto wao wale wa 4 wakiwa busy tu mjini wakijaribu hili na lile .Rafiki huyu alifanikiwa kusoma hadi level ya chuo kikuu,na akafanikiwa kufaulu vyema.Wakati huo Hawa watoto wanne wakiwa busy na maisha yao na wakiwa wana watoto kadhaa Kila mmoja.

Baada ya kumaliza elimu ya chuo ,mjukuu huyu alifanikiwa kuajiriwa kwenye kampuni Fulani mkoa Fulani Kanda ya ziwa,na akawa anawasapoti Bibi na Babu yake kwani ndio waliomhangaikia tangu mama yake aondoke duniani.Bahati mbaya hawa Bibi na Babu yake nao wameshatangulia mbele ya haki Sasa,wakiacha nyumba mbili walizoweza Jenga.

Baada ya wazee wale kufariki wale watoto wote wanne wamerejea kwenye mji wa wazee wao,wakagawana vyumba kwenye nyumba moja na nyingine wameipangisha wakipokea kodi,na huyu mjukuu hawampi hata senti.Ila hilo siyo dhumuni la huu uzi.

Tatizo Hawa watoto wanne ambapo ni watu wazima wenye kuanzia miaka 40 na kuendelea,wanamtaka huyu mjukuu,awe anawatumia hela ya chakula,maji,umeme, hospital wakiumwa na kuwasomeshea watoto zao kwani walezi wake (Bibi na Babu)walipokuwa hai alikuwa anawahudumia yeye,ila baada ya kufariki akawakabidhi Hawa watoto nyumba na kuendelea kujiimarisha kwenye mji wake.

Sasa suala ni je ni sahihi,yeye awahudumie hao wajomba na shangazi,ilhali ni watu wazima,hawana ulemavu wowote,wana nyumba hizo mbili za urithi na wanapokea kodi.Wote hao hawafanyi kazi wanategemea hizo nyumba za urithi kuishi.Wanamlaumu kuwa Ana roho mbaya,asipowatumia hela,je ni sahihi?isitoshe wanalalamika kuwa wazazi wao ndio wamemsomesha huyu mjukuu.
 

The iron batterfly

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Messages
1,902
Points
2,000

The iron batterfly

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2018
1,902 2,000
Daah maisha ya kibongo yamekaa ki stress stress tu!! Kama jama anajitambua na ningekua mimi ningefunga vioo kabisa..!! huwa sipendi ujinga kama huo...Aachane nao hao jamaa kabisa...mwishowe jamaa asije akaondoka siku si zake
Wanamchafua Sana kwa ndugu na majirani,Kuna meseji alinionyesha wanamtumia za matusi na kumdhalilisha,eti wasingekuwa wazaz hao asingekuwa hapo,mwingine anamwambia tunaomba Mungu hiyo kazi ufukuzwe, mwingine hamtafuti,akipiga simu ni anataka apewe mtaji,ambao kashawapa Mara kibao wanakula then wanakaa na marafiki wakimcheka na kumwita mjinga,watu wanamfowadia hizo sms.
 

daudthefarmer

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2016
Messages
5,424
Points
2,000

daudthefarmer

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2016
5,424 2,000
Wanamchafua Sana kwa ndugu na majirani,Kuna meseji alinionyesha wanamtumia za matusi na kumdhalilisha,eti wasingekuwa wazaz hao asingekuwa hapo,mwingine anamwambia tunaomba Mungu hiyo kazi ufukuzwe, mwingine hamtafuti,akipiga simu ni anataka apewe mtaji,ambao kashawapa Mara kibao wanakula then wanakaa na marafiki wakimcheka na kumwita mjinga,watu wanamfowadia hizo sms.
huyu rafiki yako simu yake haina blocking batani auabadili namba kwani kuna shida!
 

Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2018
Messages
1,929
Points
2,000

Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2018
1,929 2,000
Du Afrika tuna safari ndefu. Yaani kuna watu wamekaa tu wanasubiri kusaidiwa na wanaona ni haki yao kabisa na wanaweza kukuua usipowasaidia na kibaya zaidi hawanaga shukrani hata ukiwasaidia vipi. Akiwaendekeza yatamshinda. Awasaidie kwenye yale mambo ya dharura kama ugonjwa, lakini kwenye maisha ya kila siku wajitegemee.
 

Titans

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2010
Messages
1,465
Points
2,000

Titans

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2010
1,465 2,000
Nilishajifunza sana hayo makosa. Awafungie kioo tu. Undugu wa kuduanzi huo. Mimi kuna dogo mpaka alitaka kupigana na mimi kisa namlazimisha kwenda shule enzi hizo yupo sekondari. Yaani nilikuwa namfatilia aende shule dah kisa dogo ni mbavu akanikwida kabisa akitaka tuzichape why namfatilia. Mind you huyo ni mdogo wangu kabisa tumbo moja. Hao hata ukiwapa mtaji ni sawa na bure. Kata misaada ishi kwa furaha. Yanayoendelea sasa sisemi.
 

LUBEDE

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Messages
4,242
Points
2,000

LUBEDE

JF-Expert Member
Joined May 7, 2013
4,242 2,000
Hao ndugu ni dini gani?kuna kitu nataka nijifunze hapa..maana kuna ka`utafiti fulani kasiko rasmi nakafanya..nataka ni`conclude na jibu nitakalopata kutoka kwenye hili swali..
 

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Messages
7,288
Points
2,000

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2016
7,288 2,000
Sio kwamba hawapi ila wamemgeuza Kama baba yao Sasa,ilhali ni kijana mdogo aliyepaswa kuomba usaidizi toka kwao.
Hata baba yako kuna stage inakubidi umganduke tu. Kama kusoma ni rahisi hata wao wangesoma mkuu. Hao ni gunia la misumari.
 

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Messages
2,153
Points
2,000

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2018
2,153 2,000
Ushauri muhimu kwa huyo rafiki ako: Achague mtoto mmojawapo kutoka kwa hao ndugu zake ambaye ana uwezo darasani na amsomeshe mpaka pale atakapokomea. Ni ujinga wa kiwango cha lami kuwasaidia hao ndugu wakubwa ilihali ni watu wazima wenye miji yao.

Penye uhitaji wa msaada kweli mfano ndugu anaumwa, ndio atoe support tena endapo huyo ndugu yake kakwama kweli kweli. Yeye kusomeshwa na wazazi wa hao ndugu sio guarantee ya wao kumgeuza chuma ulete.
 

Forum statistics

Threads 1,390,951
Members 528,310
Posts 34,067,712
Top