Kuzaa na mtu hakukupi haki ya kufanya naye ngono kila utakapo!

new gal

JF-Expert Member
May 4, 2021
1,558
2,874
Habari zenu wanajukwaa,

Kumekuwa na trend ya kudharau sana single mothers wakidai kuwa lazima aliwe na aliyemzalisha. Hii ni dhana potofu na nafikiri inatengenezwa na hawa waliozaa na wanawake hawa.

Mimi ni single mother niliolewa kabisa tukashindwana tukaachana na mwenzangu kashaoa na ana watoto wengine. Mwaka jana alipiga kimya kwenye ada na matumizi ya watoto wake nikahustle mwenyewe hadi mwaka ukaisha.

Mwaka huu alinicheck kuwa anataka kuwaona wanae nikamwambia ruksa waone. Akaniuliza kuhusu ada nkampa mkeka, akadai hayuko vizuri. Nikamwambia nitamsaidia kukopa ila atakapolipa alipe na riba yake akakubali.

Nikapewa Tshs. 50,000 ya kununua vifaa sikulalamika, nikasema hayupo vizuri kwa sasa. Nashangaa anaanza kusema kamiss misosi yangu nkamwambia siwezi mpikia tena, akasema amemiss mbususu na show kali nkamwambia tushaachana haitakuja kutokea.

Nyie watu; imefika muda wa kulipa (technically nilikadiria sababu ada nishalipa baada ya kusota mwaka jana sikutaka ijirudie nkajipanga). Napiga simu haipokelewi wala message sijibiwi tena.

Kisa nimekataa kutoa show mtu kagoma kuhudumia wanae?? he he.

Nawasihi single mothers wenzangu usikubali kutumika kwa majukumu ya mtu. Kama anafanya afanye hataki pambana.

Nawapenda
 
Back
Top Bottom