Kuwepo tu hisia ya kuwa mke wa Kaizari alikua akisaliti ndoa yake kulitosha kumtalik | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwepo tu hisia ya kuwa mke wa Kaizari alikua akisaliti ndoa yake kulitosha kumtalik

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Feb 7, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tangu ibainike ya kuwa rais mstaafu B.W.Mkapa alitumia ikulu kuendeleza biashara yake, hadhi ya ofisi hiyo machoni mwa baadhi ya raia imeshuka sana kiasi kwamba hivi sasa limekuwa jambo la kawaida kwa rais aliyoko madarakani kushukiwa ya kuwa hata yeye anashiriki katika vitendo vya hujuma kwa nchi yetu. Kwangu mimi hiyo ni hali ya hatari; hatuna budi tuelewe kwamba, rais kama taasisi ndicho kielelezo na kioo cha taifa letu. Hivyo tendo lolote linalo dhalilisha hadhi ya taasisi hiyo alipashwi kuchukuliwa kimzaa mzaa tu. Ni kwasababu hiyo, mimi naaminiya kuwa kauli aliyo itoa rais Kikwete kuikana Dowans haitoshi; kuna haja ya kuunda tume ndogo kuchunguza ni nini chimbuko la msururu wa tuhuma nyingi ambazo zimekuwa zikielekezwa kwa rais.
   
Loading...