Mbowe ni Mbumbumbu wa Historia ya Nchi yake au Ukaidi tu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe ni Mbumbumbu wa Historia ya Nchi yake au Ukaidi tu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Jan 28, 2011.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Huu ndiyo ukweli na haihitaji kufanya utafiti wa ndani kujuwa hili kwa Mh.Freeman Mbowe, Mwenyekiti m-babe wa chadema, kiongozi wa upinzani bungeni na mfanyabiashra wa kibepari Tanzania akiwa ni Mkwe wa muasisi wa chadema, mzee E.Mtei ni mbumbumbu wa historia ya nchi yake ama mkaidi tu .
  Mbowe ni mbumbumbu wa historia ya Tanzania au mbishi tu, kusema la haki sina hakika na elimu yake siwezi kusema chochote katika hilo lakini kwa kauli yake mwenyewe kathibitisha kuwa hana uelewa wa kutosha wa baadhi ya mambo ya msingi ya historia ya nchi hii ua ubishi tu.

  Kwa kauli yake Mh. Mbowe amesema au amenukuliwa kusema kuwa " ... Mh. Idriss Abdulwakyl Nombe (late), alikuwa na elimu ya darasa la saba...".
  Marehemu Mzee Wakyl alikuwa rais wa Zanzibar wa awamu ya nne na makamo wa rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania 1985-90.

  Awali nilidhani kuwa Mh. Mbowe ameghafilika,hivyo waungwana wakamkumbusha Mh. Mbowe kuwa kauli yake aliikosea na kiungwana tu awaombe radhi familia ya marehemu kwa kauli yake hiyo ya bahati mbaya. Kwakuwa ukweli ni kuwa Mzee Idriss Abudulwakyl alikuwa ni msomi wa ngazi ya chuo kikuu Makerere Uganda, chuo kile kile alichosoma Nyerere na wasomi wengine wa Tanzania,hilo Mh. Mbowe halijuwi wala hajawahi kulisikia na akadai kuwa anataka kufanya utafiti ndiyo aombe radhi.
  Mbowe ameenda mbali zaidi kwa kukataa kuwa amekosea na kushikilia msimamo wake wa kukataa kuomba radhi wanafamilia ya mzee wakyl na hata taasisi alizotumikia.
  Mh. Mbowe amesahau kuwa Wakyl alikuwa kiongozi wa kitaifa, ambaye anastahili heshima na hadhi kama viongozi wengine wa kitaifa waliotangulia mbele ya haki.

  Anaposhikilia kauli yake ya kumbeza, kumdharau na kumtoa thamani kwa kauli kama hiyo ajuwe kuwa anawatukana na kuwatoa thamani wananchi ambao walimuamini kuwa kiongozi wao na kumuheshimu wakati na baada ya uongozi wake.

  Ushauri wa bure kwa Mbowe, kuwa ukaidi wake hauwezi kumfanya masikini wa fedha kusema kweli, lakini heshima yake kama kiongozi wa kitaifa asiyeheshimu viongozi wenzake wa kitaifa itapotea na wananchi watamdharau.

  Namkumbusha kuwa kutafuta uaduwi na watu si vyema, asisahau jinsi Mh Mizengo Pinda alivyoivua heshima yake kwa wazanzibari kama nyoka anavyovuwa kanzu yake, kwa Zanzibar Pinda si chochote si lolote hata viongozi wa chama chake huku wanamuona "kojoz" tu.

  Hivyo, mbowe asitake hayo yamkute, chama chake hakijuulikani huku, naye anahitaji kishike dola, akubali kuwa amekosea na kuwaomba radhi si CCM bali wanafamilia wa Mzee Idriss na wananchi wa Zanzibar na Tanzania ambao wanawaenzi na kuwaheshimu viongzi wao wa kitaifa.
   
 2. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Wapemba bwana..
   
 3. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Nimeona chuki binafsi, shudu, na ukame wa fikra. Kajipange upya!
   
 4. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Kama Mbowe ni mbumbumbu, we Ukwelikitugani ndiyo unaijua kwa kiasi gani. Kumfahamu mtu, kama Abdulwakil, haaminishi kwamba unaijua historia nchi. Fikiri kwanza kabla ya kuandika.
   
 5. A

  Awo JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Hakuna u-waziri kivuli this time, so deal with it.
   
 6. S

  SUWI JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Washauri pia ilkulu wamwombe msamaha Dr Slaa kwa kumwita amechanganyikiwa kwa sababu historia inaonyesha Slaa ni Dr na si kweli chiz, waambie na wao ni mambumbumbu wa historia na wababe!!!!!!!!!!!!!!!!! la sivyo huna jipya chuki tu zinakusumbua... :peace:
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Well mkuu Junius kusema ukweli sioni kuto kujua kwa Mbowe elimu ya Mh. Idriss Abdulwakyl Nombe kama kiashirio cha Mbowe kuto kujua historia ya nchi. Elimu ya marehemu mzee huyu ina umuhimu gani kwenye historia ya nchi? Nadhani hiyo ni personal history ya marehemu na wala haina significance yoyote kwenye historia ya nchi.

  Nita kacho kubaliana na wewe ni kwamba kama kweli Mbowe kasema elimu ya huyu mzee ni la saba na kama kweli marehemu mzee huyu alikua kumbe msomi wa chuo basi Mbowe ana takiwa aombe radhi. Kama kweli kakosea sioni sababu ya kuto kuomba radhi kwa sababu hata hivyo kitu chenyewe siyo politically damaging. Tena itamuongezea heshima kama ata kiri makosa.

  All in all mkuu I think umekuza hili swala kwa kulifanya ni swala la historia ya nchi lakini nakubaliana na wewe kuhusu kuomba msamaha.
   
 8. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  crap
   
 9. n

  ngoko JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MwanaFalsafa1, umenena kweli
   
 10. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa maana hiyo asipoomba radhi anashtakiwa au? Historia ya nchi hii ina mambo mengi sana kuliko kumfahamu abdulwakil. Zaid ya hapo kuifahamu historia ya nchi haina maana kwamba unafahamu kila kitu. Mbowe anaweza kufuta usemi wake baada ya kugundua ukweli sio lazima aombe radhi kwa uzito unaoutaka.
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  MwF1,
  Ni sawa, lakini Mbowe ni Mw'kiti wa chama cha kitaifa, hivyo ni kiongozi wa kitaifa, kutojuwa kwake habari za viongozi wa kitaifa waliopita kunalenga upeo fulani wa ufahamu wake wa historia ya nchi yake, kama angelisema kwa Nyerere au Kawawa ungemuonaje? ujuwe hii ni sawa na kusema kuwa Nyerere alifanyakazi na kiongozi mbumbumbu, kitu ambacho kinaashiria msemaji haelewi historia ya mtu anayemsemea kwa mujibu wa hadhi na ngazi yake ya uongozi (Waziri, Makamo wa rais na rais).

  Mkuu, elimu ya za viongozi wetu wote ni muhimu kwa historia ya nchi yetu (sielewi kwanini umesema "elimu ya mzee huyu"), ndiyo maana Watanzania wakahoji elimu ya mgombea mwenza wa chadema katika uchaguzi ulipita inawapa wasiwasi.

  Unapoomba dhamana za kitaifa suala la elimu siyo personal history/issue bali ni haki ya unaotaka kuwaongoza kujuwa na kukupima uwezo wako. Nadhani utakuwa shahidi tulipokuwa tunahoji elimu feki za baadhi ya webunge wa bunge lililopita kwa maana hiyo hiyo, na kama ingekuwa ni suala lao binafsi kusingeonekana umuhimu wa kujuwa elimu zao.
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hahah ahaha ahahah, vijembe vingine vinaumiza si utani............
   
 13. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Post thread ingine utoe maoni yako ni vipi tunaweza epuka kulipa dowans
   
 14. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kwa kauli yake Mh. Mbowe amesema au amenukuliwa kusema kuwa " ... Mh. Idriss Abdulwakyl Nombe (late), alikuwa na elimu ya darasa la saba...".

  Kwani ukiwa na elimu ya Makerere unakuwa huna ile ya darasa la saba??
  Kama ndivyo alifikaje university??

  Hahahahaaa
   
 15. M

  Mchili JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Inatosha msameheni Junius
   
 16. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Junius mbona viongozi wote wa Zanzibar wanapotosha juu ya historia ya kweli ya mapinduzi ya Zanzibar, mbona mpaka leo hawataki kutambua kuwa Okello ndio alikuwa kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar na Si mzee Karume, mbona hadi leo hawasemi kuwa uhuru wa kweli wa Zanzibar ni ule wa mwaka 1963 wa waziri Shamte na sio mapinduzi ya 1964? je wote hawa ni mbumbumbu wa Historia? na je hawa hawapaswi kuomba radhi watanzania wote kwa kuwadanganya miaka yote hii?
   
 17. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mbona Mbowe alishalizungumzia hili suala na kuwaomba radhi wote ambao welikwazika kwa kauli yake hiyo.
   
 18. d

  dos santos JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  junius umesema kweli ila tatizo umemgusa ki mungu wa wachaga huyo kwa taarifa yako huwa hakosei mbele ya wagalatia wasio na akili. Nilisema hata akinya hadharani watashangilia,na kumpongeza
   
 19. BWANYEENYE

  BWANYEENYE Member

  #19
  Jan 28, 2011
  Joined: Jun 2, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Junius umewagusa hapo utaishia kuambiwa kila aina ya maneno na hapa wameanza tu subiria baada ya mda utajuta kwa nn uliwambia huo ukweli........POLE SANA
   
 20. d

  dos santos JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  junius umesema kweli ila tatizo umemgusa ki mungu wa wachaga huyo kwa taarifa yako huwa hakosei mbele ya wagalatia wasio na akili. Nilisema hata akinya hadharani watashangilia,na kumpongeza
   
Loading...