Kuweni makini, utapeli mpya umeibuka Dar

Kuweni makini, utapeli mpya umeibuka Dar

Dar ilitokea kama ya kwako. Walivyoenda kituo cha polisi kama ulivyofanya,polisi waliuliza huyo mtu anafananaje.Walivyoambiwa walicheka na kusema hawawezi kutoka ila mhusika amkamate amlete kituoni wao watamweka ndani. Walimkimbiza na watu wakaanza kupiga kelele za mwiziii mwiziiii akasema mi sio mwizi.. mi tapeli... Walimkamata na kumpeleka kituoni lakini akatoka!
 
Jamani kama hii ilishatumwa humu mnisamehe kwa sababu jana imenikuta mwenyewe

Kuna jamaa atakupigia simu akijifanya anakufahamu na atakupa some few detais zako....(kwa sababu hata alivyopata namba yako hujui) kisha atakuambia yukoa kwenye makami ya wakimbizi na kuna dili ya kupata fedha..............atakuambia ujifanye wakala wa madawa na utakwenda kwa wazungu ambao watakupa keshi na uwape dawa hiyo........inasemekana wanataja majina mbalimbali mimi walinitajia demoline liquid.............kweli utaongea na boss mzungu na atakuambia ulete sample ya dawa na atailipia (mechezo unaanzia hapo

Atakuunganisha na boss wake na huyo boss atakuunganisha na mtu hayo madawa yanakopatikana na utaambiwa ulipie sample moja ya dawa hapo ndipo unaliwa kwani wakati unaipeleka hiyo dawa wale ulioambiwa utawakuta hoteli fulani watatoweka.......

Yawezekana habari isifanane sana lakini uki-smell rat achana na hiyo HABARI
 
Halafu wako smart kinoma, wana connetion hadi wizara ya kilimo, waliwahi kunikosakosa na mie, chupuchupu, sema ukiwachunguza kwa kuwaulizia huko wanakojidai kufanya kazi kwa majina yao, unakuta ni magumashi tu. Ni kweli wapo, ila ni rafiki zetu wa karibu ndio wanaotuuza, hakuna geni.
 
harafu wanapokupigia simu, anakutaja na jina lako kabisa!kana kwamba anakufahamu fika.mimi niliwashitukia mapema,wakanitishia maisha!
 
Hahahahaha ......... mi niliwaendea na polisi na kuwakamata wote mwaka jana mwezi wa kumi mana nlikua nishapata info. siku nyiiingi humu humu jamvini.
 
Hahahahaha ......... mi niliwaendea na polisi na kuwakamata wote mwaka jana mwezi wa kumi mana nlikua nishapata info. siku nyiiingi humu humu jamvini.

Safi sana Popobawa,uliwakomesha vizuri kabisa!!!
 
Mimi nilichonga nao kuanzia mpambe aliyejifanya ananifahamu hadi kwa bosi wao mdhungu kwa siku mbili. Hadi wakasafari(ki-magumashi) na ndege ya kukodi toka Kasulu hadi Dar. Nikaenda Shelys kukutana na supplier then NIKAMUMBIA MSHKAJI amabaye alikuwa nadhifu kwamba hii biashara noma tafuta shughuli nyingine ya kufanya hapa mjini( nikamwambia nakusamehe kama JK alivyowasamehe wazee wa EPA) jamaa akasema kwa kifupi tu eti duh poa bro! ,nikampigia simu yule mchonga mchongo nikampa maneno naye akasema poa mshikaji. Nikaachana nao! They are smart but not smarter!
 
Hahahahaha ......... mi niliwaendea na polisi na kuwakamata wote mwaka jana mwezi wa kumi mana nlikua nishapata info. siku nyiiingi humu humu jamvini.
Si mbaya kutujuza ulifanikiwa kwa kiasi gani maana na mm nilitaka kufanya hivyo nikaambiwa na polisi wamo nitapoteza muda
 
Hii imekuwepo miaka mingi iliyopita. Nashangaa bado inaendelea.
 
Kuna rafiki yangu alilia sana pale airpot na akapigwa kilo 5 ila aliyemlengesha anamjua
 
Si mbaya kutujuza ulifanikiwa kwa kiasi gani maana na mm nilitaka kufanya hivyo nikaambiwa na polisi wamo nitapoteza muda

yawezekana!!! mimi nilitaka wanijuze kua namba yangu ya simu waliipata wapi,walipokea kichapo sana kutoka kwa polisi lkn hawakutaja badae niliamua kuondoka na kuwaachia polisi mana niliona wananipotezea muda na nilisharidhika na kibano walichopata kutoka kwa polisi .........
 
Shukran
 
Ukiwa mwizi na mpenda fedha za haraka/haramu ndio watakupata vizuri sana. Wanaopatikana astahili yao kwani hao watu wanatumia weakness ya wapenda utajiri wa haraka kwa njia za mkato.
 
Hawa jamaa kiboko, mwaka jana wametapeli jamaa zangu wawili, milioni mbili kila mmoja; na jamaa zangu ni wajanja wa mjini haswa lakini kwa hawa ngoma ikawa kali;
 
Mimi nilichonga nao kuanzia mpambe aliyejifanya ananifahamu hadi kwa bosi wao mdhungu kwa siku mbili. Hadi wakasafari(ki-magumashi) na ndege ya kukodi toka Kasulu hadi Dar. Nikaenda Shelys kukutana na supplier then NIKAMUMBIA MSHKAJI amabaye alikuwa nadhifu kwamba hii biashara noma tafuta shughuli nyingine ya kufanya hapa mjini( nikamwambia nakusamehe kama JK alivyowasamehe wazee wa EPA) jamaa akasema kwa kifupi tu eti duh poa bro! ,nikampigia simu yule mchonga mchongo nikampa maneno naye akasema poa mshikaji. Nikaachana nao! They are smart but not smarter!

wanapenda sana kutumia kigoma, lakini pia mara nyingine unaweza pigiwa simu ya mzungu namba za sudan etc;
 
Wana JF nimewiwa kuwaarifu kuwa kunautapeli ambao umekithiri sasa ambapo unapigiwa simu kuwa kuna dawa za kuchanja mifugo huko Serengeti(??) hivyo uwasaidie kuzipata jinsi watakavyokuelekeza. Kwa kuwa wako Arusha wewe ukiwa DSM uwasaidie kupata sample kwa mtu watakaekulekeza kwake, Dr Peter (??) ambaye nae atampa kijana wake akutafute uchukue sample baada ya kumwachia deposit ya fedha kiasi kadhaa kama laki 5 au 6 nk.

Wanasema eti dawa yenyewe ni USD 2,800-Naomba uchukue tahadhari au ufanye mipango wakamatwe. Dawa yenyewe ni "gustavic vaccination for animals in liquid form 68f 1000mls".
 
Back
Top Bottom