Kuweni makini na wapiga kura wa mitandaoni

Ayenda M

Member
Jan 4, 2018
97
132
Kukua kwa sekta ya mawasiliano hapa nchini tumeshuhudia mambo mengi pia yakibadilika.

Katika nyanja ya siasa na sheria hapa nchini tumeshuhudia uanzishwaji na upitishaji wa Sheria inayoangazia matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.

Leo hii mtu muoga ni nadra sana kuandika kitu cha kuponda, kukosoa au kuelezea hisia zake kwa serikali kupitia mitandao kama Facebook, Twitter na hata Instagram. Ni wachache sana waliojitolea kuendelea kukosoa yale wanayoyaona hayaendi sawa, ila wapo wengi wanaosifia hata upumbavu wa wakubwa zao. Kwao kosa sio kosa, ujinga ni werevu na upumbavu ni akili. Hili kundi ni kubwa.

Octoba tunaenda kushuhudia uchaguzi mkuu. Hapa ndipo tunaenda kuona nguvu ya mitandao ya kijamii. Kuna kitu kikubwa sana huwa kinanifurahisha, watu wa mitandao huwa tuna dunia au Tanzania yetu tofauti kabisa na watu wa kule kijijini kwetu ambapo shule ipo umbali KM 10, maji unayafuata asb. unarudi jioni, umeme bado haujafika na ubora wa Internet unasoma "E" hata kutuma sms WhatsApp hauwezi na ukiwez lazima usubiri dk 10.

Hii ndiyo Tanzania yenye wapiga kura wengi. Huko ndiko kuna mama haumwambii kitu kuhusu Rais Magufuli. Ukiingia ndani ya nyumba unapokelewa na kanga ya Mzee Mwinyi. Utamwambia nini huyu akuelewe?

Kuanzia mwaka 2015, tumeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya vijana wanaojua kuuliza, kuhoji, na hawakubali kirahisi kushindwa. Vijana hawa ndio sisi tupo mitandaoni. Vijana hawa wamejaa hasira na hawapendezwi na mifumo iliyopo, ila asilimia kubwa hawaendi kupiga kura.

Wapiga kura wengi ni wazee, na akina mama na hata baadhi ya vijana ambao hawakai JF, Twitter au Instagram.

Idadi kubwa ya watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Instagram na Twitter ni wasaka followers na popularity ni wachache sana hujikita kwenye mada wakiwa wanamaanisha. Post yako ya Twitter kupata Likes 6M, Comment 270K na Retweet 5M kisikupe kiburi cha kuwa unaweza kuwa mshindi, hapana.

Wakati tunafanya kampeni kwenye soft copy, tusisahau Hard Copy. Mitandaoni wamejaa watu wengi ambao watakupigia makofi kwenye raha na shida ili kuonesha wako nawe, ila kwenye kivuli cha mitandao mama (Barua, Simu, Sms) wanakuchinja taraaatibu).

Napenda kuwaasa wagombea wa upinzani na Chama tawala, tusogee vijijini na mijini tukakutane na wazee, akina mama na vijana ili tuongeze kura huku akaunti za Twitter, Facebook na Instagram tuzikabidhi kwa wataalamu wetu waendelee kututangaza.

Kura za mitandaoni ni nyingi sana, ila kura za kwenye box ndo zitakupatia cheo na jukumu la kutawala. Ahsante.
 
Back
Top Bottom