Tanzania sasa si mahali salama pa kuishi binadamu! Maana tunasikia wizi kwenye ATM, mara wizi wa mizigo uwanja wa ndege, mara uuaji wa tembo, mara wanyama hai wanasafirishwa, hatujatulia mabilioni yatafunwa TANESCO, mara oooh mabilioni ya uswisi, sasa na makampuni ya simu na yenyewe yameingia kwenye wizi huu? Mmmh, hata kama Mkapa alitoka na kashifa ya EPA, na hisi Kikwete hali yake ni mbaya kushinda ile ya Mkapa. Kama wakati wa Mkapa ziliibiwa bilioni 150, this time hadi anaondoka Kikwete madarakani tutakuwa tumepoteza matrioni.
Hivi ina maana security system ya Tanzania ipoje? Kama watu wanachora dili mbaya za kuiba kiasi hiki, hadi kuna watu wanatengeneza ATM card na kuiba fedha benk watu wanaohusika na usalama wa nchi hawana habari, hivi haiwezekani watu kuunda kikosi cha uasi kwa lengo la kushambulia msafara wa Rais? Au hata kupindua nchi? Ukishaona kuna loopholes za mambo ya kijangiri mengi kufanyika nchini, basi ni dhahiri kwamba nchi haipo salama. Ni vema wenye mamlaka watambue huu ukweli kwamba hata wao hawapo salama kama hali ya nchi ipo hivi.