Sio jeshi la mtu mmoja, anajua anachofanya kwa mtindo huo huo unaomwona naoMbona jamaa yeye kama ni jeshi la mtu mmoja na anajiongelea tu mambo yake ya kisheria kikakamavu. Kuna wakati yanawafurahisha Wanaharakati kunawakati yanafurahisha watawala.
Mimi nadhani kila mtu afanye mambo yake.
Mfano anasema..
1: Lissu kuwa muhaini ni uongo ni kesi ya uongo.
2:Mama ndio role model wake namba moja. Anazikubali sana zile 4R.
Binafsi nampenda nikimuona popote lazima nimsikilie maana akiongea lazima upate kitu kipya kwenye akili. Sio kama yule Mwakabu...
Naona anajua anachofanya, kipindi kile alitumika baadaye amejiresha kwa namna ambayo ni ngumu kujuaMkurupukaji tu huyo....
Hajui kusoma upepo..angetuliza kichwa akajiunga CHADEMA...akagombea Ubunge-Jimbo la Ilemela-Mwanza,wakati wowote alikuwa anashinda tena kwa kishindo.
Msaada na Utetezi, wake wa Kisheria kwa makundi mbali mbali ya Kijamii aliokuwa anautoa..Ulikuwa umeanza kuzungumziwa sana kwenye vijiwe na viunga vya Jimbo hilo lenye maamuzi tasa,ki Siasa.
Na Jimbo hilo lilivyo na makundi tofauti tofauti ya Kijamii yanayosigana mara kwa mara na vyombo vya Dola(Wavuvi,Wamachinga,Mama Ntile,Wanawake-Barmaids-Dada Poa nk.).Kwa Mwelekeo wake huo, alionyesha ku 'FIT IN'.
-Msimamo.wa -'No Reforns No Election'- akashindwa kuendana nao..Akayumba.
Kwa sasa haeleweki kama ni MNYAMA au NDEGE..amekuwa POPO
Nakubaliana na wewe vizuri tu.Kama alikuwa anakubalika, angepita ubunge bila kujali chama kinachomdhamini. Ni kama ilivyokuwa kwa Mfalamagoha Kibasa 1995 Iringa mjini, Mkosamali na Machali 2010
Kwa akili hizo, nawaapia hawa chadema ni hatari kuliko watu wowote hapa Tanzania. Fikiria bwege kama huyu anashika madaraka, Kuna yeyote atakayethubutu kusema lolote?!!! Ukisema tu unapewa majina mabaya na visasi kama hivi.1. Madeleka ni Kada Mtiifu wa CCM
2.Madeleka ni Askali police.
3. Madeleka ni Pandikizi la CCM ndani ya ACT WAZALENDO.
4. Madeleka ni Mpokea Taarifa akumalize.
KUWENI MAKINI SANA NA BINADAMU.
MAANDIKO YANASEMA USIMUAMINI MWANADAMU.
Kama alikuwa anakubalika, angepita ubunge bila kujali chama kinachomdhamini. Ni kama ilivyokuwa kwa Mfalamagoha Kibasa 1995 Iringa mjini, Mkosamali na Machali 2010
Uchaguzi upi?Kama alikuwa anakubalika, angepita ubunge bila kujali chama kinachomdhamini. Ni kama ilivyokuwa kwa Mfalamagoha Kibasa 1995 Iringa mjini, Mkosamali na Machali 2010
Sijapandikiza chuki, nimesema kuweni Makini na MadelekaTujifunze kuheshimu watu wanaojitokeza waziwazi kusema misimamo yao tena ya kupinga serikali uaji kama hii, hata kama hatuwapendi, chukua points chambua baki na kinachokufaa vingine tupa.
Kwa hali ya sasa mtz kusimama na kuzungumza kama huyu jamaa ni sawa na kulalia mtutu wa bunduki wenye risasi zilizokokiwa kabisa! Tuwaheshimu sana na sio rahisi kama kuandika hapa na tukitumia majina fichwa
Huo ambao hakujiunga na CHADEMAUchaguzi upi?
Tahadhari isiyo na viashiria!Sijapandikiza chuki, nimesema kuweni Makini na Madeleka
yule wakili mpiga maji sanaaa?🐒
Atakuwa anamshahara mrefu sana1. Madeleka ni Kada Mtiifu wa CCM
2.Madeleka ni Askali police.
3. Madeleka ni Pandikizi la CCM ndani ya ACT WAZALENDO.
4. Madeleka ni Mpokea Taarifa akumalize.
KUWENI MAKINI SANA NA BINADAMU.
MAANDIKO YANASEMA USIMUAMINI MWANADAMU.
Nadhan huipi muunganiko mzuri mbinu yake ya uwasilishaji. Kuwasilisha ni art sio!Kitaaluma yuko njema sana hilo halina ubishi..Utata ni namna anavyojaribu kui husianisha taaluma yake hiyo ya Sheria na suala zima la Siasa..na uzuri hajaingia kwenye Siasa kwa kificho,alikuwa wazi na dhani 2020 aligombea hata Ubunge Jimbo la Geita Mjini kupitia ACT-Wazalendo.
Matamko yake mengi sasa yamekuwa ni yenye kubeba mkanganyiko mwingi tu.Msikilizaji wake inakubidi uchukue upande mmoja kati ya Mwanasheria au Mwanasiasa .ndipo utamwelewa vizuri .
Sawa Mkuu..ila uwasilishaji kwa Lugha ya kawaida tu na yenye kueleweka kwa wepesi ..ni afya zaidi kwa Mwana Siasa katika kuyafikia malengo yake.Nadhan huipi muunganiko mzuri mbinu yake ya uwasilishaji. Kuwasilisha ni art sio!
Ni sawa na mtu kukusifia kwa namna inayokudhalilisha!
Mf. ni hoja 4R aliisifia kwa namna inahitimisha kuwa basi aliyeileta hajui alimaanisha nini ukilinganisha na hali ya sasa.
Unahitaji kumsikiliza Madereka kifasihi pia.
Mf mwingine ni kumsifia rais kwa kufuta kesi za kubambikiza 1000+ na Lisu yu ndani!
Isitoshe, wafu werevu hunikita zaid katika hoja iliyoko mezani kuliko personality ya aliyeileta(ndo mana tunashauriwa hata kichaa msikilize kwanza mpaka ujiridhishe vinginevyo)
Ukikubali kujikomboa katika utumwa wa akili na ukaafiki kusikia ukweli basi utaelewa kama Madeleka ni mwenzetu tena mwenzetu sana.