Kuweni makini na baadhi ya pharmacies! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuweni makini na baadhi ya pharmacies!

Discussion in 'JF Doctor' started by patience96, Nov 17, 2011.

 1. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nimegundua kuwa baadhi ya wafanyakazi (Pharmacists?) ktk Pharmacies za madawa ya binadamu(private Pharmacies), hawana taaluma yoyote ya madawa ya binadamu! Baadhi yao wamekaririshwa tu na wakati mwingine mambo yakiwa magumu si ajabu ukakuta wanapekua vitu fulani fulani ktk counterbook zao au kupiga simu kwa maboss wao ili kuhitaji msaada.
  Hivi majuzi nilikwenda kununua dawa ya kutibu malaria ktk Pharmacy fulani, kabla ya kwenda pale, nilishaandikiwa na Daktari dawa ya "Artesunate/Thaitanzunate" dawa ninayotumia mara kwa mara. Bahati mbaya sikupata pale Pharmacy; mama mmoja mfanyakazi wa pale alinishauri nitumie "Duo-Cotecxin[SUP]R [/SUP]" kwamba ni nzuri tu aidha haina side effects, sikuwa na option kwani sehemu hile Pharmacy ni moja tu!
  Yule mama alinipatia prescription kuwa dose ya dawa husika ni: 3/3/2 kwa maana ya siku ya kwanza vdonge 3, siku ya pili 3 na siku ya tatu 2.
  Kwa vile sikuwa na imani na mama yule kutokana na mazingira niliyoyaona, niliangalia leaflet ya dawa ile na ilisomeka hivi:

  Weight Age Day 1 Day 2 Day 3
  >40kg >14yrs 3 3 3 e.t.c.

  Nilipomwonyesha yule mama sehemu hii, alipata kigugumizi kisha akaniambia nifanye alivyonielekeza yeye, baada ya kumbana kidogo aliangalia ktk kiji-counter book kisha aliomba muda kigogo ili awasiliane na boss wake. Bahati nzuri sauti ya boss wake nilikuwa naisikia akamwambia yule mama kuwa bei ya dawa ni tshs. 8,000/= (wakati nilishalipa 10,000/=), na dosage ni 3/3/2. Nilichukua namba ya simu ya yule boss na kumpigia, baada ya kumweleza wasiwasi wangu alikiri kuwa yeye ni Nurse nimpe dk 3 ajaribu kuulizia kwa Daktari pale anapofanya kazi (Hospilati teule ya Wilaya)! Majibu ya Daktari yalikuwa 3/3/3! Nilijaribu kumpigia rafiki yangu pale Sekou Toure Mwanza, aliniambia dose ya dawa ile ni 3/3/2! Nilishindwa kushangaa nini kinaendelea!

  Wataalamu wanaofahamu mambo haya, What is the usual mean dose of Duo-Coteccxin[SUP]R[/SUP] for an adult person above 35yrs and above 70kgs of weight ?
   
Loading...