Mama alikuwa anaandaa chips kwa ajili ya watoto wake wawili Jasmini na Lazaro. Watoto walikuwa wanabishana nani atachukua sahani ya kwanza ya chipsi. Mama akagundua mzozo huo, akaona wakati huo ni vema akawafundisha maadili mema akawaambia: "Lazaro kama angekuwa Yesu leo hapa ndani angemtanguliza mwenzake kwanza."
Lazaro: "Naomba leo Jasmini awe Yesu ili anitangulize mimi nipate chips kwanza!"