Kuwadhaarau wataalamu, matokeo yake...

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,559
Amani kwenu,

Hivi kama Serikali ingekubali kukawa na Database ya Taifa kwa wizara zote na Halmashauri zote, tatizo la wafanyakazi hewa lingetoka wapi?

Hivi kama tungewatumia wataalam wa kilimo, kilimo kwanza si ingekuwa mbali? Hivi kama wangesikilizwa viongozi wa Jeshi kipindi cha awamu ya kwanza, vita ya Tanzania na Uganda ingetokea wapi?

Hivi maamuzi yote tunayoyaona pasipokushirikishwa wataalamu, tutarajie nini iwapo hayatakuwa ya tija kwa watanzania? Au tusubiri kuombwa msamaha kama ilivyotokea kwa? Eti asingebinafsisha makampuni ya Umma pasipo maandalizi?

Ni mengi ya kujadili ila sasa.
 
Usimlamu raisi.
Bali ilaumu katiba yako ambayo inazalisha hayo unayolaumu
 
Usimlamu raisi.
Bali ilaumu katiba yako ambayo inazalisha hayo unayolaumu
Simlaumu raisi, wala mtu yeyote!

Naulaumu mfumo ulipo, ambao umeasisiwa na CCM ambapo mwendelezo wake ndo matokeo tunayoyaona sasa. Mwalimu aliwambia wachukue mazuri toka Azimio la Arusha lakini halikuchukuliwa hata moja. Badala yake ni kuendelea kuhubiri uhuru na umoja wakati hata ndani ya CCM hakuna uhuru wala umoja.
Ile miiko ya uongozi ilisaaulika zamani sana. Nakumbuka miaka ya 80 / 90 mtu alikuwa hajipendekezi kugombea uongozi kama ilivyo sasa.
 
Back
Top Bottom