Senior Boss
JF-Expert Member
- Aug 19, 2011
- 3,405
- 3,702
Imekuwa ikisemwa hivyo mara kwa mara. Mimi niliamini huu usemi mwaka 2002., nakumbuka nilikuja Dar kufatilia uhamisho wangu wa shule, nilikaa kwa baba yangu mdogo kwa takribani wiki moja. Huyo mama niliyemkuta hapo alikuwa hapiki mpaka mumewe awepo. Wiki niliiona kama mwaka, hata nilipoaga nilipewa nauli kimanati. Najua wengi tumepitia kwa ndugu kutokana na sababu mbalimbali, kuna walioishi vizuri lakini wengi wanalalamika. Je tatizo hasa nini? Ukiwa ni miongoni mwa uliyetendewa mabaya, umejifunza nini?
Haya mambo yako pande zote zote. Sisi mama yetu alikuwa anatuambia tulale kwenye makochi wageni wakija nyumbani ambao most of them ni ndugu upande wa baba. Kuna waliokuwa wanakuja bila hata malengo; si wa kuondoka leo au kesho lakini tulikuwa tunabanana tu. Wengine wakaja ku win maisha tukawa tunawasikia bombani wala shukurani hawana.
Wengine ni ndugu wa mbali. Wanatangaziana tu huko kijijini; ukienda dar fikia kwa mzee fulani ana nyumba kubwa. Tena wanakuja kwa kushtukiza maana those days hakukuwa na simu za viganjani ni za kukoroga tu. Mnashtukia mtu katia timu. Sisi tulikuwa tuna mind kweli maana tulikuwa hatuko comfortable lakini mama alikuwa mkali kweli yani priority kwake ni wageni. Mama alipoachana na baba walikuwa wa kwanza kushangilia wala hawakuwa wanakumbuka fadhila zake. Binadamu ni wagumu sana kuishi nao.
mmh....watu wengine tukisimulia masaibu yaliyotukuta......tutajaza kitabu......ila cha muhimu....ni kumuombea adui yako aishi siku nyingi.....ili unapofanikiwa ajionee kwa macho yake mawili
Haya mambo yako pande zote zote. Sisi mama yetu alikuwa anatuambia tulale kwenye makochi wageni wakija nyumbani ambao most of them ni ndugu upande wa baba. Kuna waliokuwa wanakuja bila hata malengo; si wa kuondoka leo au kesho lakini tulikuwa tunabanana tu. Wengine wakaja ku win maisha tukawa tunawasikia bombani wala shukurani hawana.
Wengine ni ndugu wa mbali. Wanatangaziana tu huko kijijini; ukienda dar fikia kwa mzee fulani ana nyumba kubwa. Tena wanakuja kwa kushtukiza maana those days hakukuwa na simu za viganjani ni za kukoroga tu. Mnashtukia mtu katia timu. Sisi tulikuwa tuna mind kweli maana tulikuwa hatuko comfortable lakini mama alikuwa mkali kweli yani priority kwake ni wageni. Mama alipoachana na baba walikuwa wa kwanza kushangilia wala hawakuwa wanakumbuka fadhila zake. Binadamu ni wagumu sana kuishi nao.
ni bora kila likizo umpeleke mtoto kwa ndugu ili akajifunze maisha, ukimuacha wiki mbili au tatu akirudi kanyookaaaaaaa. lazima appreciate unachompa. kila akikuangalia anaomba mungu usife leo.
hakikisha unampeleka mbali kidogo ili asiweze hata kudandia gari kurudi home.
Mh. Kaizer unachokiuliza nami nimeshajiuliza sana, mimi nimelelewa kwa mjomba baada ya Baba kutangulia kwenye HAKI.
Na kwa vile tulizaliwa 7 hivyo nduguze Mama na ndugu wa Baba (the late) wakatugawana sisi watoto kumwondolea Mama task work ya maisha, huko kwa Uncle ndipo nilipoyajua haya mnayoyasema, aidha Uncle hakua na tatizo, Mkewe ndiye alikua mwiba wa Nungunungu! Pamoja na yote maisha ya hivyo yana advantage na disadv kwani kwa upande mmoja utapata faida ya kujua Njaa inavumiliwaje utajua Branget linafuliwaje, vyombo vinaoshwaje, deki inapigwaje, utajua kupika n.k.
Watoto wanaokulia kwa wazazi wao wa kibayolojia wenye umri sawa na wanaokulia kwa ndugu walezi hawawezi kua sawa katika kumudu mazingira yanayowazunguka, wale walioko kwa walezi wanakua more active kuliko wanaokulia kwa wazazi halisi.
Inaelekea kila mtu kayapitia haya. Sasa cha kunuia hapa c kwamba mtoto wako asiende kwa mtu, bali usije mtendea hivyo mtoto wa mtu mwingine. Kwa maana hii dunia tunategemeana, ina wezekana ukawa umejidhatiti vya kujitosheleza, lakini kunamatukio yanatokea mtoto anajikuta yupo kwa watu bila kupenda. kila mtu akimjali mtoto wa Mwingine kama wakwake, hakuna mtoto atakaye nyanyasika.
Ukifatilia matajiri wengi hii ndio sabab wanatafuta hela na mafanikio kwa nguvu zote. Kuna kitu au watu kwa namna moja au nyingine anajaribu kuwa prove wrong hence anaweka a lot of effort. Dat mimi ninaweza na nitawaonyesha kwamba ninaweza.
Ni kweli mkuu, ukinyanyasika sana utatia akili tu!!