Kuwa na wapenzi wawili ni sawa?

Kikuburu

Member
Jul 8, 2016
43
30
Dunia haiishi visa,
Week iliyopita ni dada mmoja yalimkuta,

Ana mpenzi wake waliahidiana mengi ikiwemo kuoana. Dada anafanya kazi na mkaka japo ni 35 ukaka unakaribia kuisha anajiendeleza kimasomo.

Dada huyo anadai kila wakikaa pamoja na mpenzi wake kuna simu inaingia lakini mkaka hapokei, mara kadhaa! Akimuuliza anajibu simple ni msumbufu tu achana naye atapiga akichoka ataachaga. Akija kulala ndo inapigwa hadi usiku wa manane.

Roho ikazidi kumuuma kama ilivyo kawaida ya mapenzi akajitosa akaenda kwa shemela akachukua simu ili akague kwakuwa alikuja gafla akakuta mambo mubashara!

Chat za kimahaba na mdada ndo anaonekana kakolea zaidi maana anatuma sms hata 15 kaka anajibu moja anamuomba shemela amruhusu aje kwake japo siku moja! Shemela akamuambia subiri ukiwa na mda mzuri jumamosi ili tufaidi vizuri weekend Hizo ni mbinu pia maana mpenzi wake yuko karibu. Hapo shemela alishamuaga dada wawatu kuwa ana safari ijumaa atarudi jumapili. Kumbe kuna kisafari alienda kufanya research zake ndo akakutana na huyo mdada mpya

Basi wivu+maumivu+ hasira akachukua simu ya mpenzi wake akachat na dada akijifanya ndo yule kaka na kumwambia nimeoa acha kunitafuta utavunja ndoa yangu na mke wangu keshashtuka! akamjibu ila hukunambia una mke.

Dada yule akachukua ile namba tena akaenda kumtafuta mwenzake nakumpa onyo kali aache kumsumbua mumewe kabla hajamfanyia jambo baya.

Kumbe kama kawaida kaka anamtafutaga usiku ndo akamuambia kanipigia simu mwanamke wakl na simu yako kaniambia nikiendelea kukutafuta ataniua!

Movie ikaisha hivi: mkaka akawa hapokei simu ya mpenzi wake tena, baada ya mdada kumpigia siku kadhaa akamtumia tu ujumbe mfupi Kuwa hawawezi kuendelea kuwa wapenzi kwakuwa amefanya kitendo kibaya sana kuchukua simu bila idhini yake akasoma sms, akafuta zingine, akamtishia mtu maisha bila kujua ni kosa kisheria na hii ni ishara mbaya kwani imemuumiza moyo sasa na hata baadae! Ukizingatia wao sio mke na mume ni wapenzi tu hakuna anayepaswa kuingilia simu ya mtu kiasi hicho.

Akajaribu kumuomba msamaha ili wayazungumze ila kaka kanyamaza kimya hahitaji mazungumzo na kafunga mjadala kihivyo.

Nikampa tu moyo kuwa avumilie yatapita tu, huku akiwa na shauku mpenzi wake apokee japo simu waongee yaishe kwani alimkanya huyo mwanamke kwa lengo la kulinda penzi lao ila mwenzake kapata sababu.

Nikasema nishare na wadau hivi mpenzi anaruhusiwa kucheat bila kuulizwa kisa hamjaoana?? Na ukikamatwa na mpenzi wako unacheat wewe ndo wakukasirika hadi jmuache wewe?

Huyo alikuwa kamchoka tuu jaman.
 
Ukiiba usilalamike kuibiwa.

Kama ni mpenzi wako na hamjaoana huku mnagegedena aki-cheat huko nje usilalamike maana hata wewe naye unaiba kwa kuwa si mkeo.

Ila kama hamgegedani mmevumiliana ili baadaye muoane, hapo una haki ya kustuka.
 
MAPENZI YA SIKU HIZI NI RUKSA KUSHIKANA ILA SIO KUSHIKIANA SIMU


BTW embu nipe namba ya huyo mdada alietoswa nimuulize kitu
 
Hata Hata mm huwa nakereka MTU hujaniona kuchwa kutwa unang'ang'ania simu yng
 
Alishamchoka alikuwa anatafuta sababu ya kumuacha tu
Ila hapo mi naona huyo Dada amezidi kiherehere MTU hajakuoa kwahiyo hapo angekuwa mpole huku anampetipeti jamaa wafunge ndoa
Sasa akishakuwa Wa halali ndio angefanya hivyo alivyofanya
 
Kama unajua una roho ndogo kama yangu Simu ya mwanaume unashika ya nn jamnnnn..as long as unachokitaka kwake unakipata,tatzo lipo wapi!!!
Tukome vihere here..

Mpe pole mwambie next time aache kugusa sim za wanaume.
 
Akili zetu wanaume tunazijua wenyewe kuna jamaa kamuacha dada wa watu kisa kaandika msg kwa herufi kubwa kasema hiyo ni dharau anamuona haoni vizur hadi kumuandikia kwa herufi kubwa!!
 
Alishamchoka alikuwa anatafuta sababu ya kumuacha tu
Ila hapo mi naona huyo Dada amezidi kiherehere MTU hajakuoa kwahiyo hapo angekuwa mpole huku anampetipeti jamaa wafunge ndoa
Sasa akishakuwa Wa halali ndio angefanya hivyo alivyofanya
mtu Kama huyo hafai hata kupetiwa,wala kuwa Mume.
 
Back
Top Bottom