Kuwa mpole hauijui kesho yako

madeinmusoma

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
322
386
Ilikuwa majira ya saa tano asubuhi mwaka 1988 wakati Mike Tyson anamuajiri Donald Trump kama mshauri wake wa masuala ya kifedha na mipango... Leo "boss" Tyson hana hata nafasi ya kumsalimia mwajiriwa wake pale White house!!

Mwaka 2005 Diamond alisafiri kwenda Tanga kuomba kuperform kwenye show ya Q-Chilla. Mabaunsa wakamtimua. Alipojaribu kuwaelewesha wakambeba juu juu na kumchania Tshirt na kumtupa nje. Bahati nzuri Q-Chilla alijulishwa kuhusu purukushani hizo, na alipoenda akasema aruhusiwe kuingia na apewe nafasi ya kuperform. Leo wale mabaunsa pengine wanatamani kuwa mabaunsa wa Diamond lakini haiwezekani.

Joseph Kabila aliwahi kuelezea kuwa kipindi anaishi Tanzania aliwahi kushushwa kwenye basi porini huko mkoani Iringa kwa sababu hakuwa na nauli ya kutosha. Alijaribu kumuomba konda amshushe angalau mahali penye mji lakini hakumuelewa. Akamtelekeza porini. Akatembea kwa mguu hadi Nyololo ndipo akapata msaada. Leo yule konda pengine anatamani kupata nafasi walau ya kumuomba msamaha Kabila lakini haiwezekani. Hakujua kama aliyemshusha porini angekuja kuwa Rais wa nchi.

Mwanzoni mwa miaka ya 1980's Meneja wa hoteli moja ya kitalii huko Hangzhou, alimnyima kazi Jack Ma. Baadaye Jack Ma alianzisha kampuni ya Alibaba na kumuajiri mtu huyo aliyemnyima kazi kuwa Meneja masoko wa online auction hosting ya Alibaba.

Maisha ni kama sarafu iliyotupwa angani, huwezi kutabiri itadondokea upande upi. Hakuna anayedumu kwenye madaraka milele. Hakuna anayekuwa tajiri milele. Hakuna anayekuwa maskini milele. Vyote hivi ni vya muda tu. Ni suala la majira na nyakati.

Mtu unayemdhihaki leo na kumuona sawa na takataka, inawezekana ndiye atakayeamua hatma ya maisha yako kesho. Hakuna ajuaye kesho. Mheshimu kila mtu bila kujalisha yupo katika hali gani leo kwa sababu huwezi jua kesho atakuwa wapi. Mtumishi wako wa leo anaweza kuwa boss wako wa kesho, kwa sababu kwenye maisha hakuna kinachodumu milele.

Tumia nguvu zako, utajiri wako na mamlaka yako kwa hekima ukijua kuna kesho. Siku zote simamia haki. Usimdhulumu mtu, usimnyanyase wala kumkandamiza mwenzio kwa sababu tu ya mali, nguvu au madaraka uliyonayo.

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe aliwahi kusema "Heshimu kila Kona ya taulo lako, kwa sababu sehemu utakayoitumia kufutia kalio asubuhi unaweza kuitumia kufutia uso jioni."
 
Kuna rafiki yangu huyo siku Mungu akisema amtembelee katika mwili wa kichaa,kapuku au mtu dini kabisa 💯atafukuziwa mbali mnooo..
Hii kitu huwa inanitesa sana anapenda kutreat watu kinamatabaka.

Usimdharau yoyote anaekatiza kwenye maisha yako.labda awe na vitendo ovu.
 
Kama mpo wote hapo mwambie namsalimia
 
Very wise words and a reminder to us all. Maisha hayatabiriki na binadamu tungepewa uwezo wa kujua kesho zetu tungeheshimiana sana sana.
Tumejisahau mno kuheshimu mtu haigharimu hela wala muda ni suala la mtazamo tu...
 
Ilikuwa majira ya saa tano asubuhi mwaka 1988 wakati Mike Tyson anamuajiri Donald Trump kama mshauri wake wa masuala ya kifedha na mipango... Leo "boss" Tyson hana hata nafasi ya kumsalimia mwajiriwa wake pale White house!!

Mwaka 2005 Diamond alisafiri kwenda Tanga kuomba kuperform kwenye show ya Q-Chilla. Mabaunsa wakamtimua. Alipojaribu kuwaelewesha wakambeba juu juu na kumchania Tshirt na kumtupa nje. Bahati nzuri Q-Chilla alijulishwa kuhusu purukushani hizo, na alipoenda akasema aruhusiwe kuingia na apewe nafasi ya kuperform. Leo wale mabaunsa pengine wanatamani kuwa mabaunsa wa Diamond lakini haiwezekani.

Joseph Kabila aliwahi kuelezea kuwa kipindi anaishi Tanzania aliwahi kushushwa kwenye basi porini huko mkoani Iringa kwa sababu hakuwa na nauli ya kutosha. Alijaribu kumuomba konda amshushe angalau mahali penye mji lakini hakumuelewa. Akamtelekeza porini. Akatembea kwa mguu hadi Nyololo ndipo akapata msaada. Leo yule konda pengine anatamani kupata nafasi walau ya kumuomba msamaha Kabila lakini haiwezekani. Hakujua kama aliyemshusha porini angekuja kuwa Rais wa nchi.

Mwanzoni mwa miaka ya 1980's Meneja wa hoteli moja ya kitalii huko Hangzhou, alimnyima kazi Jack Ma. Baadaye Jack Ma alianzisha kampuni ya Alibaba na kumuajiri mtu huyo aliyemnyima kazi kuwa Meneja masoko wa online auction hosting ya Alibaba.

Maisha ni kama sarafu iliyotupwa angani, huwezi kutabiri itadondokea upande upi. Hakuna anayedumu kwenye madaraka milele. Hakuna anayekuwa tajiri milele. Hakuna anayekuwa maskini milele. Vyote hivi ni vya muda tu. Ni suala la majira na nyakati.

Mtu unayemdhihaki leo na kumuona sawa na takataka, inawezekana ndiye atakayeamua hatma ya maisha yako kesho. Hakuna ajuaye kesho. Mheshimu kila mtu bila kujalisha yupo katika hali gani leo kwa sababu huwezi jua kesho atakuwa wapi. Mtumishi wako wa leo anaweza kuwa boss wako wa kesho, kwa sababu kwenye maisha hakuna kinachodumu milele.

Tumia nguvu zako, utajiri wako na mamlaka yako kwa hekima ukijua kuna kesho. Siku zote simamia haki. Usimdhulumu mtu, usimnyanyase wala kumkandamiza mwenzio kwa sababu tu ya mali, nguvu au madaraka uliyonayo.

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe aliwahi kusema "Heshimu kila Kona ya taulo lako, kwa sababu sehemu utakayoitumia kufutia kalio asubuhi unaweza kuitumia kufutia uso jioni."
japo sio lengo la uzi, ila Trp ni bilionea kuanzia muda mrefu sana hata kipindi hiko alikuwa ni mshauri tu na sio mwajiriwa wake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom