Kuwa masikini siyo sifa na siyo kipimo cha uadilifu

Kuwa masikini siyo sifa na siyo kipimo cha uadilifu

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
15,743
Reaction score
39,800
Habari wana JF

Kuna dhana potofu kwamba umasikini ni kielezo cha uadilifu. Hivyo basi, kiongozi masikini yaani asiye na mali kabisa au asiye na mali nyingi ni muadilifu. Kwangu mimi hii ni dhana potofu.

Uadilifu una vigezo vyake ambavyo vinapimika, ikiwa ni pamoja na tabia njema. Kiongozi masikini au asiye na mali nyingi anaweza akawa si muaminifu au muadilifu, yaani mla ruswa lakini akawa hana uwezo wa kutunza hiyo miamala ya rushwa na mwisho wake akawa masikini.

Kinyume chake wapo viongozi ambao walikua waaminifu wakatumia vipato vyao vizuri kuongeza mitaji, wakatunza miamala yao wakawa matajiri.

Kwa muktadha huo, umasikini siyo uadilifu na siyo sifa njema. Umasikini ni ishara kwamba haukutumia rasilimali zako vizuri au haukubahatika kupata rasilimali wezeshi na hivyo ukabaki kuwa mtu wa kawaida.

Hivyo basi, naomba tujitenge na dhana potofu, na umasikini usihusishwe na uadilifu.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom