Kuwa makini na mtandao wa Airtel

victory02

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
1,149
1,554
Huu mtandao umekuwa na shida sana hasa kwenye upande wa Airtel money.

Baya zaidi wana wahudumu ambao wana majibu rahisi sana ya tumelipokea tatizo lako ndani ya masaa 24 utapata majibu ila ni uongo mtupu.

Pindi unapowarudia baada ya hayo masaa 24 au zaidi wanasingizia wahudumu tupo wengi ngoja tulishughulikia tatizo lako, kwa kifupi mnakuwa mnaanza upya.
 
ni wapuuzi,kila siku wananitumia kwa siku zaidi ya sms 3 kwamba kifurushi kimeisha na wakati kipo au hata nikijiunga gb 2 hapo hapo wanasema kimeisha ndani ya sek 5
 
Siupendi huu mtandao, huwezi hata kuongea na huduma kwa mteja na pesa za Airtel money ni rahisi kuibiwa
 
Nawashauri mnaopata issue ya kimtandao muweke maeneo husika coz kwa mfano huku Bunju nilipo network iko strong kabisa
 
Airtel hawafai, Mimi ninadai wanirudishie muamala wangu yapata wiki sasa ,wananizungusha tuuu,nilikosea kuingiza namba ya wakala wakati nafanya muamala ,mara Moja nililipoti Kwao wakaniambia wangerudisha pesa yang ndani ya masaa 6 ya Kazi Lkn mpaka Leo wananizungusha tuuu, kila Siku nawapigia simu wananiambia kitu kile kile,yaani wamenikera sana, sijuwi hata nifanyeje.
 
Back
Top Bottom