Kuwa makini na mafaili ya Adobe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwa makini na mafaili ya Adobe

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kilongwe, Sep 14, 2010.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Siku za hivi karibuni kumetokea habari kuhusu mwanya uliopo kwenye Adobe Acrobat na Adobe Reader ambao unawawezesha mahacker kutengeneza code na kuziweka kwenye mtindo(format) wa pdf huku wakizipamba kwa jina zuuuuri,pindi ufunguapo tu basi imekula kwako kwani hizo code zitajirun na kushusha minyoo na virusi kwenye kompyuta yako itakayomuwezesha hacker kuitawala kompyuta yako bila wewe kujua.

  Hii ni hatari mno kwani wengi wetu tumekuwa tukiamini kuwa hauwezi kukutana na virusi au minyoo kwenye faili kama la Adobe.

  katika kukabiliana na hili Adobe wametoa ushauri wa kiusalama kwa watumiaji wawe makini katika kipindi hiki wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa tatizo.

  AfroIT inawashauriwanajamii kuwa makini la hili pia kufuata ushauri uliotolewa na Adobe APSA10-02, Vilevile unaweza kutumia Microsoft's Enhanced Mitigation Toolkit (EMET) ambayo inakuwezesha kujilinda na uvamizi kama huu ambao kwa lugha ya kitaalamu tunauita uvamizi wa siku ya sifuri(Zero-day exploit),hii ikimaanisha mianya ayopatikanika kwenye programu bila mtengenezaji kujua.

  Unaweza kupata maelezo ya ziada kwa kutembelea Microsoft Security Research and Defense blog.

  Timu nzima ya AfroIT itakuletea update pindi mbalimbali za masuala ya kiusalama.
   
 2. nankumene

  nankumene JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2016
  Joined: Nov 12, 2015
  Messages: 4,255
  Likes Received: 3,398
  Trophy Points: 280
  thanks mkuu
  ,lakin why hawa hackers wanapitia sana dobe......naona warning nying sana online mda mrefu tu
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2016
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  thanks dude tupo pamoko...
   
Loading...