Kuwa kile unachohitaji na itakuwa

Kuwa kile unachohitaji na itakuwa

- Kwa sababu tu watu wengi wanafuata njia fulani,haimaanishi kwamba ni njia sahihi.

- Ukitutizama kwa makini sisi binadamu,utagundua kwamba kuna mambo mengi sana tunayafanya kama wanyama waliofunzwa.

- Kuna mambo mengi tunafanya kwa kufuata mkumbo.Na hatuelewi hata kwanini. Tumejikuta tu tunafanya au kukubali hali fulani za kimaisha bila ushahidi wala uzoefu wa moja kwa moja.

- Kwa bahati mbaya,kufanya mambo kwa mazoea au kufuata tu mkumbo kwa hofu ya kuonekana tofauti katika jamii, wengi wetu huzitupilia mbali ndoto zetu pia.Huua vipaji na kuathiri maisha yetu kwa ujumla.

- Sio siri kwamba kuamua kufanya jambo tofauti na mazoea au mtizamo wa jamii,ni jambo gumu na kwa wengine linalotia hofu na kuleta msongo wa mawazo. .

- Uoga ni chanzo kikuu cha kukata tamaa. Sio fedha wala kipaji wala kutojuana na watu fulani au kuwa na uwezo wa kipekee.

- Ndio maana,kwa mfano,utakuta mwanamke anavumilia ndoa yenye kila karaha. Anateseka kwa vipigo,matusi,manyanyaso na anaendelea kuipigania kwa sababu tu ya hofu ya “kuwa tofauti”. Halikadhalika wanaume.

- Kwa namna hiyo hiyo kuna watu wanaendelea kuzikumbatia kazi au mwajiri asiye na tone la utu. .
Anaogopa kujaribu kitu tofauti.


- Anaogopa kujinasua kutoka kwenye mtego wa kuwa tofauti.Uoga unamfanya azizike ndoto zake kwa kujiambia mambo lukuki yasiyo na ukweli wowote zaidi ya kugubikwa na uoga.

- Habari njema ni kwamba,kama ulivyojifundisha kukubali kunyanyasika,kuheshimu usipoheshimika na kunyanyasika,unaweza pia kujifunza maisha mapya. .

- Unaweza kujifunza kujiamini.Unaweza kujifunza kujitetea utu na nafsi yako.Unaweza kujifunza kusema hapana kwa manyanyaso na mateso. Unachotakiwa ni kuanza kubadili fikra zako.

- Kubadili fikra hakuhitaji kuwajua watu fulani,kuwa na fedha au uzoefu. Hapo hapo ulipo hivi sasa unaweza kuanzia.

- Kabla hujaenda kulala au punde tu unapoamka asubuhi, unaweza kuwa huru kwa kuanza kuwaza kama mtu aliye huru.

- Kumbuka yanapokwenda mawazo au nafsi,na mwili hufuata. Unaloliwaza hutokea au kuwa kweli.
Anza leo. Usiogope kuwa tofauti. Usiogope kupita njia ambayo wengi hawapiti.


NIMEICOPY SEHEMU, HOPE INAWEZA KUKUSAIDIA CHANGAMOTO UNAZOKUMBANA NAZO[/QUOTEnimeongeza kitu ahsante mkuu
 
Back
Top Bottom