Kuwa halisi kwenye Uchumba

Pyepyepye

JF-Expert Member
Jan 6, 2017
1,940
3,829
Katika mahusiano ya uchumba unatakiwa kuidhihirisha tabia yako halisi ikiwemo madhaifu yako, ili mwenzi wako ajue nini anachokwenda kukutana nacho katika maisha yenu ya ndoa, ili ajipange namna ya kuyaishi madhaifu hayo.

Ndoa nyingi zimeponzwa na tabia za kuigiza ambazo hulenga kuuficha ukweli na uhalisia wa mtu binafsi hasa mapungufu ya wanandoa hawa enzi za uchumba wao.

KUMBUKA:
"Kwa kuwa wewe halisi, kila kitu kinakuwa halisi"
 
Hii ni fact kabisa

Kuna mdada fulani ameolewa kwetu ni tabu tupu
Mwanzo alikuwa na tabia nzuri sana
sasa mwaka huu mwanzoni kafanikiwa kuolewa na huyo ndugu yetu bhana

Yani ni hataki kuona hata wakwe wakienda kwake na amemchana kabisa mume wake kuwa yeye anaweza kuishi na ndugu zake tu kwasababu ndio wanaifahamu tabia yake
 
Aiseee nahisi wenye sifa halisi watakuwa wachache saana.....

Ila Bora waonyeshe ili mtu ujue whom your dating....Maana sometimes hatuoi tabia
 
Tulikua na kashem ketu flan hv kanatokea hukoo kanda ya ziwa... Broo alikua amezama ile ile na kiukweli she was vr innocent mkarimu na wife material kwa muonekano... Kuna siku nlipta maeneo kumchek bro nkamkuta nkaakaa nae kidogo nkaona anaongea sana na simu mda mrefu halaf anaongea kilugha... Nkamuuliza bro huyu vp akaniambia ndio alivyo ashamzoea... Nkamwambia try to work on it nmedoubt kitu... Tafuta siku kaa nae akianza kuongea kilugha mrecord then tafuta rafik yko wa kabila lake muombe akutafsirie akakubali kufanya hvyo na kupeleka hyo audio kwa watu zaid ya wawili ili kujiridhisha kwamba hamna upotoshaj wa hyo tafsiri.... Akagundua hua anachepuka na binamu yake ambae yy na broo wanafahamiana na wanaitana bwana shemeji kumbe wanakula wote mzigo na mambo mengne mng tu ya aibu... Akakata shaur na kuamua kumuacha sahv yupo zake single anajitafakari jins kuanzsha mahusiano mapya
 
Ukweeli humuweka mtu huru, huwezi kuigiza kwenye suala muhimu kama la ndoa
 
Back
Top Bottom