mchemsho
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 3,212
- 867
Leo hii jioni katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alikuwa na mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mwanga center Kigoma mjini. Kinana ambae aliambatana na Nape na balozi Ali Karume kama walivyojitambulisha. Lengo la ziara ni kuimarisha chama. Msemaji wa kwanza alikuwa Balozi Ali karume kikubwa alichizungumzia ni muungano, akisisitiza msimamo wa chama wa serikali mbili, amepuuza waziwazi mapendekezo ya tume ya jaji warioba ambayo kimsingi ndio mawazo ya watanzania waliowengi ya serikali tatu, hakuwa na hoja ya maana ya kutetea serial I tatu, just because ni mapendekezo ya chama hotuba yake hiyo fupi haikuwa na msisimko wowote.
Alifutia Nape Nnauye... Kama kawaida yake hakuelezea yanayohusu chama chake, ni mashambulizi dhidi ya chadema, kubwa ni kwamba wafadhili wa chadema wameanza kuhoji ni kwanini wanatoa fedha nyingi na bado chadema haishindi chaguzi mbalimbali ref. Uchaguzi wa kalenga na chalinze, alipoanza kupanda ile mbegu ya ubaguzi wa ukabila, udini na ukanda akirefer watovu wa nidhamu wanavyoadabishwa ndani ya chama mvua kubwa ilianza kunyesha...na kama ilivyo kawaida ya viongozi wengi wa ccm hawaamini Mungu akasema wazee mpo, zuieni mvua.
Baada tu ya kauli ile pamoja na uzushi dhidi ya chadema aliokuwa ameanza kuropoka mvua ilianza kumwagika ya haja huku wazee ambao nape alitumaini wangezuia mvua (kufuru na kejeli) wakitimka mbio na kuwaacha viongozi tu wakiwa jukwaani peke yao.
Hoja yangu ni kwamba CCM na TBC kwa makusudi walizima mitambo yao wakati Tundu Lissu akihutubia na kuwanyima haki ya kikatiba raia wengi wa Tanzania ya kupata Habari na elimu, Mwenyezi Mungu amelipa mara moja huku Kigoma kwa kuachilia mvua kubwa sana ili kuzuia uzushi na chuki visisambae. Wao wana Pesa na TBC sisi tuna Nguvu ya umma na Mungu.