Kuvunjwa kwa baraza la mawaziri!

Rayase

Member
Jun 12, 2009
82
3
Ndugu wana Jf niinajaribu kufikiri suala la katiba ya ichi yetu, nimeshindwa kuelewa vema. Rais anavunja cabinet wakati gani, lini? swali msingi sana kwanini bunge livunjwe afu cabinet ibaki na one condition ya kuwa cabinet member ni kuwa mbunge? je hawa mawaziri walioshindwa kwenye kura za maoni nguvu yao iko wapi! naomba tujadili ili niweze kuelewa maana uchambuzi wa sheria its not my professional!
 
Wizara zote inatakiwa ziwe chini ya makatibu wakuu sasa hivi kwani hawa jamaa (mawaziri) sasa hivi wote wako vitani wakipigania maisha yao. Lakini ukiangalia kwa ndani zaidi, hata rais na makamu wake, pamoja na waziri mkuu wote wako vitani. Kwa ajili ya fairness hawa wote ilitakiwa warudi ground zero ili wasitumie clout ya madaraka kujiongezea chances za kushinda kura, especially katika culture zetu zinazoamini strong man (hatujafikia level ya kuamini strong system). Lakini hii maana yake itakuwa nchi itabaki kwa kipindi fulani bila uongozi kwa sababu cabinet ndo biggest decision making body ya nchi. Kwa hiyo logically wanabaki mawaziri wanaoelea (hata rais) hadi hapo watakapokabidhi kwa viongozi wapya baada ya uchaguzi. I'm not a constitutional layer, I'm just thinking logically.
 
Hivi huyu anayejiita Jaji Mkuu au Mwanasheria mkuu wanafanya kazi gani? Wanawaachia hawa mawaziri waendelee kutumia mali za umma kwenye kampeni zao,vilevile kupata posho za vikao wakati kwa sasa hawana maamuzi yoyote wizarani. Hii katiba nadhani ni ya watu wajanja wachache tu, wanaichezea kama chekundu cheusi
 
kwa mara ya kwanza nimegundua mabo yafuatayo
a) mwanasheria mkuu wetu wa sasa ni mwanasiasa na kuna uwezekano mkubwa uelewa wake wa sheria ni mfinyu sana hasa kwa majibu aliyotoa hivi karibuni na kwa kiasi kikubwa hajui kitu
b) jaji mkuu wetu ana elewa vizuri sheria tatizo lake ni woga wa kutekeleza majukumu yake kwa kuogopa waliomteua hivyo maamuzi yake mengi ni ya woga woga kama kesi ya mgombea binafsi nk.

matokeo yake, Nchi inapotea katika giza totoro
 
Back
Top Bottom