roservelt
JF-Expert Member
- Aug 31, 2016
- 1,418
- 1,510
Kuvujika kwa U.S.S.R chini ya Mikhail Gorbachev.
Habarini wanabodi!!
Mwaka 1922 umoja wa nchi za kijamaa uliundwa (Union of Soviet Socialist Republics). Umoja huo uliundwa na nchi kama Romania, Poland, Czechoslovakia, Russia, Serbia, Yugoslavia na Ujerumani Mashariki.Marekani alikataa kuunga mkono uundwaji umoja huo. Joseph Stalin aliiongoza USSR kuanzia mwaka 1929 hadi1953. Mwaka 1939 Stalin aliingia mkataba wa kutopigana na kulindana na dikteta Adolph Hitler wa Ujerumani. Baadae Hitler aliusaliti mkataba huo na kuandaa jeshi lake zidi ya USSR.
Mwanzoni mwa kipindi cha vita baridi 1940s, Joseph Stalin akiwa rais wa USSR aliwezesha muungano huo kuwa juu kiteknolojia, uzalishaji wa silaha na kiuchumi. Hii ilisaidia USSR kuweka upinzani mkubwa zidi ya Marekani katika vita baridi.
Mnamo mwaka 1980s Mikhail Gorbachev alitawazwa kuwa rais wa USSR. Chini ya utawala wa Gorbachev alifanikiwa kuleta mapinduzi makubwa ya sera za kigeni za USSR. Mnamo mwaka 1985 Gorbachev alifanikiwa kurudisha mahusiano baina ya USSR na Marekani chini ya rais wa Marekani wa kipindi hicho Ronald Reagan.
Mnamo mwaka 1980s dunia ilikumbwa na mtikisiko wa kiuchumi uliosababishwa na kushuka kwa bei ya mafuta.Hii ilipelekea Gorbachev na serikali yake kupunguza nguvu kubwa katika washirika wake wa Ulaya Mashariki na duniani kote.
Katika harakati za kuinusuru USSR zidi ya mtikisiko wa kiuchumi, Gorbachev aliamua kupunguza uwekezaji mkubwa kwenye uzalishaji wa silaha wakati wa vita baridi na kuhamishia uwekezaji kwenye maeneo yenye kuleta faida kiuchumi.
Kufikia mwaka 1980s hadi 1988s USSR ilifanikiwa kupunguza nguvu kubwa kwenye vita baridi zidi ya Marekani. Mnamo mwaka 1989 Gorbachev na George H. W. Bush walitangaza mwisho wa vita baridi.
Mnamo mwaka 1991 USSR ilivunjika , Russia na nchi nyingine zikawa nchi huru zinazojitegemea.
NOTE.
Inasemekana Gorbachev alikuwa pandikizi wa taifa la Marekani, hivyo aliihujumu Russia na kuipa nafasi Marekani kuwa juu hadi leo hii.