Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,715
- 729,889
Nimelazimika kuja na mada hii ili kuondoa hofu na upotoshaji uliotaka kufanywa na mgombea mmoja wa nafasi ya kisiasa kanda ya kaskazini baada ya kushindwa vibaya na mpinzani wake.
Huyu jamaa aliwekeza sana kwenye kutoa rushwa takrima na mlungula lakini matokeo ya mwisho kura zake zikawa chache na akakosa kiti cha ubunge....
Kwa hasira na ghadhabu kali akajiapiza kuwa angevunja chungu ili wale wote waliokula vyake wadhurike
Hii ikapelekea mijadala kila mahali wengine wakisema ashitakiwe.... Huyu hawezi kushitakiwa kwakuwa serikali haiamini katika nguvu za giza na uchawi.
Iko hivi kwanza kuvunja chungu kwa nia ya kudhuru ni uchawi uliopitwa na wakati kutokana na maendeleo katika nyanja za maisha. Hivyo automatically kuufanya ufe kifo cha asili au hata kama upo upoteze nguvu yake na mvuto pia.
Aina hii ya uchawi ilitumiwa na mhusika aliyeudhiwa jambo na jamii yake au ukoo wake kuamua kufa na watu wengi kadiri ilivyowezekana....
Na hiki ndicho kilichofanyika:
Kugombana kupo popote lakini watu husuluhishwa na kuyamaliza lakini wengine hubaki na vivyongo hivyo kusubiri wakati muafaka alipe kisasi kunapotokea kusanyiko la msiba au sherehe inayowakusanya ndugu au wanajamii.
Wakati ule hatukuwa na huu utaratibu wa kunywa maji ya chupa bali maji yote huwekwa kwenye mtungi mkubwa na kata na kila mwenye kiu angeingia kwenye chumba husika na kunywa kiasi chake.
Kwahiyo aliyedhamiria kutenda maovu angejificha mahali akavunja chungu akasaga akachanganya na dawa nyingine akanuizua na kwenda kumwaga ule ungaunga wenye manuizi ya kuua na kudhuru, na huanza mwenyewe kunywa na kwenda kujificha ili akifa asionekane. Sasa watakaofuatia wote kunywa hayo maji hawaponi na ni mpaka watu washtuke ndio inakuwa salama ya wengine.....
Hivyo ndivyo ilivyo.
Sasa ndugu yangu Mono sijui alitaka kutumia njia gani???