Kuvuja siri & kauli ya Msajili vyathibitisha ukweli wa mtonyaji serikalini kuhusu vifo mikutanoni

By Msuguyumlonje


.CCM tambueni kuwa MUNGU yupo aliyeumba mbingu na dunia.Mmeshindwa kugundua kwamba mnamtumikia shetani?
 
Viongozi wa CDM wanatakiwa wawe makini na kamwe wasikate tamaa, hii ni vita ambayo inavikwazo vingi sana yapo mengi watakayokutanayo huu ni kama mwanzo tuu. hakuna uhuru uanaopatika kwa urahisi.

CCM hawapo tayari kuachia nchi kiurahisi kwani madaraka matamu sana cha msingi ni kukaza moyo, kukubali kuumia kwa ajili ya kuokoa maisha na haki ya watanzania walio wengi.
 

Mh Ndugai alituambia kuwa baadhi ya wabunge hutumia kilevi na kuvuta sigara kubwa kabla ya kuja bungeni.Hivi huyo Tendwo huwa anatumia Kilevi gani kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari?
 
walipanga kuua sasa wameumbuka, maneno ya msajili aloitakiwa kuyatoa baada ya kifo kaedit kidogo... badara ya kukifuta CDM, tutafua vyama vitakavyo sababisha vifo....

Kwenye hotuba ya msajili ambayo aliisoma kwa unyonge,maana malengo yao hayakutimia ali-edit neno CHADEMA na kupachika vyama vya siasa!

Hiyo nia yao ovu ambayo tayari wassira alikuwa ametolea tamko la kuifuta chadema kama week mbili zilizopita walitaka kuitekeleza kupitia tukio la Iringa, lakini kwakuwa Mungu aliisaidia CHADEMA kuepuka huo mtego kwa kutokufanya mikutano ya hadhara police ambao walikuwa wamekaririshwa amri walijkuta wanatekeleza walichoambiwa kwenye mazingira yasiyofaa na wakajikuta wanaumbuka!

Mungu ibariki CHADEMA Mungu ibariki Tanzania.
 
:flypig::flypig:
walipanga kuua sasa wameumbuka, maneno ya msajili aloitakiwa kuyatoa baada ya kifo kaedit kidogo... badara ya kukifuta CDM, tutafua vyama vitakavyo sababisha vifo....

Hekima,Busara na usomi wa cheo cha mzee mh tendwa ameudhalilisha, picha walizopigwa policcm wakimlipua mwandishi wa habari zinatoa jibu nani kaua hii haihitaji uwe umesoma au haukusoma.

CCM wanawatumia vibaya policcm na hivyo wao wanajichonganisha na wananchi wenye kufikiri, ingawa akina Nape, Dr. Nchimbi hilo hawalioni wanachojali mkono umekwenda kinywani, NJAA MBAYA JAMANI
 
Inatia aibu na kufedhehesha mtu mzima kujibu maswali kwa matusi eti kwa sababu ulijibiwa kwa matusi!

Ni kuulize maswali machache!

1: je marufuku ya mikutano yalikuwa kwa cdm tu? Una habari kuwa ccm zanzibar waliendelea na mikutano?

2: je watu wanapo vunja sheria basi haki yao ni kutumia nguvu na kuhakisha wana tolewa utumbo na kupigwa risasi?

3: je una habari kuwa pamoja na picha kuonesha wazi hivyo lakini viongozi wako wame kinzana kwa kauli tofauti wengine wakisema ni wananchi walirusha kitu kizito?

4: je kulikuwa kuna haja gani ya kusafirisha askari toka mbeya na dodoma kwaajili ya kulinda usalama, je wa iringa hawajui kulinda?
 

Wanzuki siyo pombe za kawaida! Kama mtu unakunywa wanzuki hangover yake ndo unaongea pumba kama hizi! Kwani tarehe 2/9/2012 CCM hamkufanya mikutano ya kisiasa, hizo sheria anatungiwa Chadema tu! Nonsense..
 



Mie huwa habari za kwako siziamini kwani nyingi huwa ni za kubuni kwa ajili yakutetea chama chako, kwa kifupi huwa hauko fair kwenye kuripoti kwako, leo hii mnasema usalama wa taifa hamuuamini kesho mnakuja na story za kuwa mmepata habari za kutoka kwa hao hao watu wa usalama, sasa hapo ndipo credibility ya info zenu inapokuwa kwenye walakini mkubwa na za kubuni. Na jf inapokubali habari za namna hii inapoteza mwelekeo, hapa ni jukwaa la uwazi wataje watu hao kwa majina tuwajue.
 

Dalili za serikali zinazoondolewa madarakani ndo hizi hapa! Hawa hawatabakia madarakani, tutawaondoa hata kwa nguvu! Wanatumia dola vibaya!
 
Mimi swali langu kwa Tendwa:
Chama kitakachosababisha mauaji kitafungwa. Mauaji ya Arusha, Morogoro na sasa Iringa yanesababishwa na chama au Polisi? Mbona asitishie kuifungia Polisi?

Swali kwa F****kn chimbi:
1. Nina mashaka na udokta wake. je mbona siko hiyo hiyo Januari makamba alifanya Mkutano huko bumbuli na mwingine ulifanyika huko zanzibar, Huko kulikuwa hamna sensa? au cdm walikaidi amri ila makamba yuko juu ya sheria?
2. iweje wauaji ni serikali ya ccm na polici wake halafu wachunguzi ni haohao?
 
Kama Tendwa ndio anatoa ushauri huu basi inaonyesha kuwa hayuko neutral. Ngoja akifute chama kwenye daftari lakini hakitafutika kwenye mioyo ya watanzania waliokombolewa. Na mapambano ndio yataendelea kuzidi ilivyo sasa

 

Mkuu twende kwa hoja, usitukane.
Kwa habari ya msg ya Dr Slaa kwenda IGP kama ni kweli au la. Tusijadili, maana wote wawili - Slaa na Wema, wamekaa kimya. Alikurupuka tu waziri Nchimbi. Na ndo maana Serikali imekaa kimya. Kile kifaa cha kuingilia mawasiliano kingalipo nchini, tusijadili hilo kwanza.

Yule aliyemshika askari mguu siyo Raia, yule ni marehemu Daudi Mwangosi mwenyewe. Baada ya zile picha kutoka polisi wenyewe na Serikali wamekaa kimya. Maana yake wanaona kuwa pa kutokea pamezibwa sasa wewe usilazimishe majibu. Ndo maana Chagonja ameacha ngonjera.
Tatu, waandishi 2 waliokuwepo pale ambao walitoa ushuhuda kupitia ITV na ambao maelezo yao yanafana kuhusu tukio hilo ndo watakaomaliza tatizo hilo. Hapo hakuna pa kutokea.
Nne, Daudi Mwangosi alikuwa kazini kivyake kama mwandishi ktk eneo la tukio kwa hiyo hata kama alifanya fujo kwa jinsi polisi walivyo wengi wangeweza kumkamata kwa njia za kawaida na siyo kumlipua bomu.
Tano, Mbona mwanzoni walisema wafuasi wa chadema walimpiga kisogoni na kitu kizito? Baada ya picha wamekaa kimya. Mungu anaipenda Tanzania bado

 
Nikwambie tu mimi sijatukana ila mwenzio ndo kanitukana, tuje kwenye msingi, je unahabari kuwa mikutano ya CDM ina record ya kuforce maandamano na kusababisha vifo? Pili. suala la polisi kutumwa kutoka mikoa mbali mbali sioni hata kama ni hoja, kwa sababu tujuavyo polisi wako wachache na hata hivyo wametokea Tz, endapo wangetokea Kenya, uganda au burundi ndo ningeshangaa, kama unakumbuka Pemba walikuwa wanatolewa askari mikoa yote Tz kwenda kulinda amani, sasa unaona ajabu ya iringa na mbeya ambayo ni pua na mdomo.? Kama polisi wametoa utumbo watu ni wapi ilishatokea kwingine kama siyo kwenye mikutano yenu ambayo mnayodai ni nguvu ya kuua ili mpate madaraka. na je unafikiri mtu akishakujeruhi unaweza kumpa nafasi tena ya kuendelea kujeruhi watu. nasema hivyo kwa sababu CDM wakiambiwa fanyeni mikutano wao wanaandama ili kukidhi matakwa yao ambayo ndo tunayoshuhudia sasa hivi. kwa hiyo mi naona ni sahihi kuwastopisha kufanya maandamanio kwa sababu wna record mbaya ya mauaji, hata kama ilitokea polisi wakaua basi ilitokea kama ajali kazini na kwa kulazimishwa na CDM. Fullstop.
 
Umenena vema na umetumia kichwa chako kufikiri vyema, asante sana.
Ukiunganisha maneno ya watu wafuatao utajua tu kuna mpango ulipangwa ili wapate njia ya kutimiza adhima yao

1: chadema hakitafikisha mwaka-wassira
2: serikali itashughulikia vyama vivyo hatarisha amani na utulivu wanchi-wassira
3: chadema wamepanga kufanya vurugu na wasii wanachi wasiende kwenye mikutano yao-Nape
4: cdm wameandaa vijana ili wakafanye vurugu kwenye mikutano yao

5: Nitatumia rungu langu kuvifuta vyama vya siasa vinavyo sababisha vifo- Tendwa

Mungu ni mwema sana na hamtupi mwenye haki!

Mungu ibariki Tanzania, mungu wabariki wapenda mabadiliko, mungu ibariki Tanzania


 


Hapo sasa, sijui watajibuje? ukumbuke Chadema walikuwa wanafanya mkutano wa ndani si hadhara. Bumbuli na Unguja kwema pamoja na kufanya mkutano mkubwa kuliko wa Chadema!!!!
 
Michael, matukio yamefanya homework yangu kutohitajika. Ni wazi uko uhusiano mkubwa sana wa mtonyaji na mtiririko wa matukio. Kuna mdau huku alisema hivi, namnukuu "...mashetani wanafanya kazi zao katika uwazi mkubwa huku wao wakidhani ni ktk usiri mkubwa mno"
 
Wewe hujaangalia hiyo picha vizuri, yule mwandishi unayemsema kamshika kiunoni sio mguuni, yaani kamkumbatia kabisa, swali langu kama hiyo bunduki mnayosema ililipua bomu, Je kwanini huyo askari naye asitolewe utumbo? au tumbo lake la Chuma? Jibu hoja, acha kuzunguka, kiuno siyo mguu. angalia kwa jicho la kawaida usiangalie kiushabiki wa CDM sote tuna machungu na ndg yetu MTz mwenzetu.
 
Hivi pamoja na maelezo yooote bado hujaelewa mantiki ya kuhusisha polisi na mauaji yanayotokea kuwa yalipangwa? Wewe huwezi kuelewa tena maana kuna dalili zote kuwa huna uwezo huo
 

Mkuu Daudi.
Nina majonzi sana baada ya kusoma hii taarifa ya Aweda lakini haka ka mchango kako hapa juu kamenifanya nitabasamu kwa uchungu.

Anguko la ccm ni mpango wa Mungu, na kwa kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu basi naamini hawana mipango mibaya watakayo acha kupanga halafu isivuje. Lazima ivuje tu maana muda na wakati ndio umewadia.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…